Kwa 'Uchawi' unaofanyika ambao ni wa 'Kufuru' Wajukuu wa Hayati Mandela watajuta kuwafahamu Wajukuu wa Hayati Nyerere kwa Mkapa Kesho

Mkuu kwa ' Uchawi ' uliofanyika, unaofanyika na utakaofanyika Kesho ( hasa pale Uwanjani ) kwa Mkapa hawa Wazulu wawe makini, wajiangalie kwani wanaweza hata Kufungwa Goli 6 hadi 7.

Huyo Mtaalam ( Mganga ) wa TP Mazembe anachokifanya sasa eneo Moja la Mikocheni alilowekwa Kesho Wajukuu wa Hayati Mandela na Waafrika Kusini wanaweza wasiamini na kile wanachoenda Kukutana nacho.
Kama huyo mganga ni hatari kiasi hicho,TP mazembe wangekuwa wanachukua hilo kombe la CAF kila msimu,Simba Safari imeisha subiri msimu ujao
 
Miaka ambayo hakudhulumiwa walibeba kikombe gani cha CAF?

1621588301765.png
 
Huu uzi utakuwa na wachangiaji wengi sana baada ya mechi. Wengine watakuja kumponda mleta uzi na wengine watakuja kumpongeza mleta uzi kwamba kapita mle mle. Binafsi hili swala sipingani nalo, nilitegemea Simba watafanya kila mbinu ili ipindue meza, kwenye mpira uchawi upo. Nikikumbuka mechi ya juzi juzi hapa kati ya Simba na timu za nje ya nchi ndani ya uwanja wa Mkapa unaona kabisa wapinzani wanavyozidiwa maana mpira wanautafuta kwa tochi na magoli pia hawayaoni. Al Ahly ilipata shida sana utadhani anacheza na Bayer Munich jinsi walivyozidiwa.
 
Kuna Watu niliambiwa kuwa wakilitaka lao wanajua kulipata kwa ' Kuroga ' vibaya tena kwa ' Kufuru ' kabisa nikawa siamini, ila kwa nilichokiona na Kukisikia kuna Mtu aliwacheka Watu Kidharau akiwa ' Benchini ' huenda Kesho akanuna na hata Kulia hadi Kuzimia na hata Kufa pia.

Wewe zitengwe Milioni 30 za Kukusanya Waganga wakubwa nchini na Kumpandisha Mbung'o ( Ndege ) Mganga mkubwa wa TP Mazembe anayezijulia vyema Timu za Afrika Kusini na ' anayeogopwa ' nao sana halafu utoke kwa Mkapa?

Ngoja nianze Kujiandaa ili Jioni leo ' nikakeshe ' zangu Temeke kwa Mkapa kwani nimeambiwa kunaenda Kufanyika Jambo ambalo Mwenyezi Mungu atusamehe tu kwakuwa ni ' Kufuru ' Kubwa ili baada ya Kufuzu tutaenda Kumpigia Magoti ya Kumuomba Msamaha Makanisani na Misikitini.

Kiuchawi Wajukuu wa Hayati Nyerere tumeshapita, ila Kiufundi mwisho wetu umeishia rasmi Afrika Kusini Wiki Moja iliyopita na Wajukuu wa Hayati Mandela wamefuzu.

Halafu Wewe Mlinzi Mmoja wa hapo kwa Mkapa Uwanjani mwenye Jina linaloanzia na Herufi ' S ' mwenye Mahaba na Timu Adui kwa ichezayo Kesho acha huo ' Unoko ' na tulia Watu wafanye yao kwani Mafanikio ya Kesho si tu Klabu hiyo bali ni ya Tanzania na Watanzania. Endelea kujifanya Mfanyakazi bora hapo Uwanjani ' Wakuue ' kabisa kwa ' Majini ' yanayoenda Kutupwa hapo kuanzia Saa 12 Jioni ya leo.

Raha ya Kesho ni 'Vimbwanga' vya Nje.
Kamati ya Ufundi isha fanya yao !
 
Huu uzi utakuwa na wachangiaji wengi sana baada ya mechi. Wengine watakuja kumponda mleta uzi na wengine watakuja kumpongeza mleta uzi kwamba kapita mle mle. Binafsi hili swala sipingani nalo, nilitegemea Simba watafanya kila mbinu ili ipindue meza, kwenye mpira uchawi upo. Nikikumbuka mechi ya juzi juzi hapa kati ya Simba na timu za nje ya nchi ndani ya uwanja wa Mkapa unaona kabisa wapinzani wanavyozidiwa maana mpira wanautafuta kwa tochi na magoli pia hawayaoni. Al Ahly ilipata shida sana utadhani anacheza na Bayer Munich jinsi walivyozidiwa.
Al ahly hawapo vizuri wanashindia bahat. Kama uliangalia game lake na mamelod utakubaliana nami.
 
Mkuu kwa ' Uchawi ' uliofanyika, unaofanyika na utakaofanyika Kesho ( hasa pale Uwanjani ) kwa Mkapa hawa Wazulu wawe makini, wajiangalie kwani wanaweza hata Kufungwa Goli 6 hadi 7.

Huyo Mtaalam ( Mganga ) wa TP Mazembe anachokifanya sasa eneo Moja la Mikocheni alilowekwa Kesho Wajukuu wa Hayati Mandela na Waafrika Kusini wanaweza wasiamini na kile wanachoenda Kukutana nacho.
Walianza wao SSC wanamaliza...
 
Mkuu huyu Mtaalam ( Mganga ) wa Congo DR wa TP Mazembe ' Vitu ' anavyovifanya eneo la Siri Mikocheni lililo Jirani pia na Bahari ya Hindi kuna Watu Kesho watafungwa Goli 6 au 7 kwani ni ' Kufuru ' tupu tu
Kwa msisitizo wako Mkuu Sina shaka kesho itakuwa patashika nguo kuchanika....
 
SIMBA KESHO AKISHINDA NA KUFUZU NITAWEKA HAPA REAL NAME, VYETI VYANGU, KITAMBULISHO CHA KAZI, MAHALI NINAPOISHI, NITATOA MSHAHARA WANGU WA MWEZI HUU NA KUWANUNULIA TIMU YA SIMBA KWA WIKI NZIMA.

MATOKEO RASMI YA GAME YA KESHO
SIMBA 2 - 3 KAIZER CHIEFS
Kwa nilivyoiangalia hii mechi kwa jicho la kiufundi (maana uchawi haupo ktk soka)
SIMBA ITAANZA KWA MPIRA WA KASI SANA DK 10 ZA MWANZO NA NDANI YA DK HZO kutokana na presha yao KAIZER CHIEFS WATAPATA BAO LA KUONGOZA hali itakayopelekea Simba kuchanganyikiwa na kupigwa la pili dk chache mbele. Lkn matokeo ya mwisho simba atafungwa 3 - 2
 
Hawa makomandoo ni wanajeshi wa south afrika au
'makomandoo' kama 'makomandoo'. Serikali ipo na Simba, funguo za mageti ya Kwa Mkapa zilisakabidhiwa muda mrefu kwa Simba, wao washindwe wenyewe! Ukisikia AC za vyumba vya kubadilishia nguo zinafanyiwa ukarabati, wala usidhani kwamba zilizopo zimechakaa
 
Back
Top Bottom