Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Kwanza nianze kwa kutoa pongezi zangu za dhati kwa mh Rais John Pombe Magufuli na Mh waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, kwa kukutana kwao hapo jana
Ni ukweli usiopingika, moja ya chaguzi za vyama vingi, zilizowahi kuwa na ushindani wa karibu, ni ule wa mwaka 1995 kati ya mh Mkapa na Mh Mrema na huu wa 2015 kati ya mh Rais Magufuli na mh Lowassa
Kitendo cha waheshimiwa hawa kukutana jana ni cha kupongezwa sana, kwani kimetupa funzo kubwa,
kuwa siasa si uadui, siasa si chuki bali siasa ni kutofautiana mawazo tu, juu ya namna gani bora, ya kuwaletea maendeleo wananchi
Kwa waluomsikiliza jana mh Rais, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, baada ya kumaliza mazungumzo ya faragha na mh Lowassa, alinuita mh Lowassa "Mzee Lowassa" Binafsi kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikimfuatilia mh Rais kwenye mikutano mbalimbali, amekuwa akitumia neno "mzee" kwa wanasiasa waliostaafu ama wanaotarajiwa kustaafu kwa siku za karibuni
Binafsi, naamini moja ya mambo mh Lowassa aliyomwambia mh Rais kwenye mkutano wao wa faragha, ni kwa yeye kustaafu siasa ndani ya muda mfupi ujao