Kwa tuliopitia machozi, jasho na damu katika ukuaji wetu

Huyo msamehe ila asilete mazoea kwenye hela...
Kuna mzee mmoja alimuomba mwanae msamaha alafu baada ya siku 2 akaanza kupiga mizinga , kuna wazazi wanajirudi kwasababu tu una unafuu wa maisha, ungekuwa bado umechoka hata usingemuona.

Mimi mtu ambaye hakuwa na mm wakati wa dhiki siwezi kuwa naye karibu abadani,maana najua yupo kimaslahi tu..
Ni kweli mkuu,
Kilio changu kikubwa kwa sasa ni kujua hatima na Baba yangu kipenzi.

Maana sielewi kama yupo hai ama la!
 
Habari JF Members.

Majuzi nimepokea meseji kutoka kwa mwanamke wa makamo akinikumbusha kuwa yeye ni MAMA yangu After 25 years ya kupotezana.

Ilikuwa hivi:
Miaka 25 iliyopita stendi ya mabasi ya kwenda mikoani pale UBUNGO mama yetu mzazi alitupeleka ofisi moja ya kukatia ticket sehemu ambayo baba yetu mdogo alikuwa anafanyia kazi, alitufikisha hapo mimi na mdogo wangu anayenifuata wa kiume na kutuacha pale huku akimuachia maagizo Ba mdogo kuwa amtafute kaka yake (baba yetu) amwambie aje achukue watoto wake yeye hana tena muda wa kuishi na mwanaume masikini,fukara na asiye na uelekeo kwenye maisha.

Habari za kipindi hiko zinadai mama alimpata mwanaume mwingine mwenye uwezo kifedha na inasemekana alimuomba kumuoa ila tu kwa sharti hataki watoto ajumuike nao kwenye maisha yao...hivyo ma alichukua maamuzi ya kutubwaga ili tu awezs kukidhi vigezo ya jamaa na waoane.

Baada ya masaa 5 baba anakuja pale Ubungo kutupitia tunaenda kibanda cha chips na kupata chakula then tunarudi home,ila njiani nilipata kujua baba yangu alikuwa kwenye lindi la mawazo kiasi gani,maana tulipanda karibia gari 3 zisizo sahihi mpaka tunafika nyumbani.

Miezi 8 tuliishi bega kwa bega na baba yetu kitu ambacho kilichofanya afukuzwe kazi kule kwa wahindi alipokuwa anafanya kisa Mahudhurio mabovu...

Alirudi nyumbani na kuanza kufanya vibarua vya hapa na pale ili tuweze kuishi..baada ya muda wa kodi yetu kuisha ilitupasa tutafute sehemu ya kuishi maana baba hakuwa tena na uwezo wa kulipa kodi kwa uhakika,tukapelekwa kwa shangazi yetu ambaye mumewe aligoma kabisa sie kuishi pale..alitufanyia visa sana..kuna muda mkiwa mnakula anakuja anawaputa chakula kinamwagika,au mkilala usiku anakuja anavuta sigara bwege/bangi chumbani kwenu basi mtakooa hapo mpaka usingizi unakata.

Shangazi ikabidi amueleze baba kuwa hawezi kuishi na sie maana mumewe hayupo tayari kwa jambo hilo.

Bahati nzuri baba alipata kibarua cha kujenga nyumba kama saidia fundi basi ikawa ndio sehemu yetu ya kushinda,na akimaliza jioni tunalala pale pale kwenye lile pagala mpaka asubuhi anaamkia kazi.

Kuna siku tulikuwa tunatoka town sasa muda wa kugombania daladala pale kariakoo shule ya uhuru baba alifanikiwa kunipitisha dirishani ili nikalie kiti kwanza,kile kitendo cha kugeuka nyuma amchukue na mdogo wangu anakuta mdogo wangu hayupo..anamuita na kukagua daladala nzima bila mafanikio...

Anamuachia maagizo konda anishushe kituo flani kuna fundi viatu ambaye ni rafiki yake kisha atakuja kunipitia..yeye wacha afanye utaratibu wa kumtafuta mdogo wangu.

Saa 5 usiku namuona baba anakuja pale nyumbani kwa fundi akiwa mikono mitupu ikiashiria hajampata mdogo wangu..nasikia wakiongea kuwa kaishatoa taarifa kila sehemu hivyo tusubirie taarifa kutoka huko.

Baada ya wiki baba anaenda kituo cha polisi biguruni na kusikia habari kuna mtoto kaletwa pale na msamaria mwema,sema itabidi aje kesho maana kuna afande wa zamu kaondoka nae kumuhifadhi kwake..

Kesho baba anaenda tena na kufanikiwa kumkuta mdogo wangu na kurudi nae,nilifurahi sana siku ile...japo kuna jambo huwa mpaka leo mdogo wangu hapendi kunihadithia au kuniambia nini kilitokea..maana alivyorudi alikuwa na vidonda kwenye magoti,kapasuka mdomoni,afu kachanika pakubwa sana mgongoni kama mtu aliyekuwa anateswa....kumbuka mdogo wangu kipindi hiko alikuwa na miaka 3.

Hata yule afande alisema nilishangaa sana yule mtoto kipindi ameletwa pale kituoni jinsi alivyokuwa na vidonda vile.

Kwa ufupi baba badae alipokea ujumbe kutoka kijijini kwa bibi kuwa atupeleke maana anasikia maisha tunayoishi huku town ni hatari sana...

Nakumbuka siku tuliyosafiri kwenda kwa bibi almost tulitumia masaa 9 kwenye Bus bila kula ,tulitepeta kiasi cha kushindwa hata kuongea kwa jinsi njaa ilivyokuwa imetupiga...nilikuwa kama mpira uliotolewa upepo sijiwezi ila namshukuru Mungu tulifika salama kwa bibi na kupewa uji.

Kesho yake baba aliondoka kurudi Town.

Tuliishi na bibi kipindi chote hiko.

Mpaka tulipopata taarifa za kutatanisha kuhusu baba yetu kuna waliosema kafungwa maisha,kuna waliosema kagongwa na gari Tazara na kufariki hapo hapo...

Bibi aliuza kila kitu ili tuweze kusoma na tulisoma mpaka bibi yetu yalipomkuta mauti...SITOMSAHAU BIBI YANGU..

Leo mimi ni Accountant private sector na mdogo wangu ni Engineer Public sector.

Majuzi nimepokea meseji ya mwanamke akiniomba niende whatsap anitumie picha za kumbukumbu ili niweze kumtambua kama ndio MAMA YETU.

katika ile picha huyu MAMA kakaa mie nimemlalia miguuni na mdogo wangu kamuegemea begani tukiwa kwenye tabasamu zito.

Inasemekana ndio siku za mwisho mwisho kuwa karibu na MAMA yetu...

Nimemtafuta baba yangu magereza yote sijampata labda kweli aligongwa gari akafariki.

Sijajibu mpaka sasa meseji za huyu mama..anapiga sana simu kila siku.
Samehe tu, afande sele na mibangi yake yote na mdomo ule, alimsamehe mama yake, alilelewa na bibi yake, alifyatua tofar, aliuza karanga, story yako na yake zinafanana tu.
 
aisee pole sana ndugu na hongera kwa kufanikiwa na mdogo wako kupata pa kujikimu.
Sometimes wazazi sijui huingiwa na nini , mie kwangu ni mshua kabsa huduma anatoa kwa kulazimishwa na mwajiri wake. Hadi sasa nina uoni hafifu, sisikii vizuri, sauti inakwaruza au haitoki na miguu kuuma na kukoea nguvu matibabu nayo hadi kulazimisha. Utaiehia kuambiwa tafuta kazi na ukiomba pesa japo ufatilie vyeti utaambiwa si unaumwa. Isitoshe mdogo wangu naye kaanza kusumbuliwa na macho hadi wa leo hakuna action zaidi ya kusema siaache shule tu imemshinda na wakati yupo vizuri kabisa. Inauma sana unakuta mzazi uwezo anao ila ndio hivyo au mwingine hathamini watoto kabsa.
Baba yangu japo sielewani naye Sana ila iwahi kunishauri kwamba ,nizae na mwanamke mmoja tu yani nisichanganye wanawake,aliishia hapo
nikitafakari kauli yake naona alikuwa sahihi,Kuna ndugu yetu yeye alipenda kuoa na kutelekeza wanawake na watoto then anaenda kuoa kwingine,hivi Sasa ni mzee amestaafu lakini watoto aliotelekeza na kuwakataa Wana Elimu nzuri wapo wanapambania Maisha ila wameshamsamehe japo wanaumia mpaka leo
 
Ningemsamehe lakini nisingekuwa na mapenzi nae wala nisingwletaka ukaribu nae.

Inaonekana anajali sana pesa kuliko utu

Siku yoyote anaweza waletea vitimbi utadhani alikuwepo muda wote kwenye maisha yenu.

Mimi ningempotezea tu

Kama i make it without her why now!?
Yaani huyo mama yao kaona watoto wametoboa
Miaka 25 mama umetulia?

Hapana isee

Angetoroka hata kutoroka akaone wanae

Na wakimkaribisha kwenye maisha yao anaweza akawavuruga mpaka wajiulize nini kimetokea.

Zaidi hapo anataka pesa... wawe makini sana

Kama mgonjwa wamlipie tiba ya hospitali wakae pembeni
 
Hii story yako inanikumbusha watoto flani wa ki sure, mama yao aliwaacha na kuolewa na mwanajeshi. Baba yao aliwalea single handed mpaka alipokuja kuoa.

Bahati mbaya baba alifariki na walilelewa na mama wa kambo mpaka wanakua wakubwa.
 
Aisee pole sana kwa hii mitihani umepitia. Mungu akupe nguvu na maarifa ya kufanya maamuzi ambayo yatakupa amani ya nafsi yako..
 
WANAOKUAMBIA UMSAMEHE NI WAPUUZI KIWANGO CHA LAMI NI MAFALA WANGEKUWA WAMEPITIA HIZI SITUATION WANGEELEWA

NA MIMI NIMEPITIA HAYA NA NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA ILI UONE MSIKILIZE ANATAKA NINI PIA MUULIZE KUHUSU FATHER MPOTEZEEE
Mkuu ukupata wasaha kdg naomba usome hvi vitabu CHANGE YOUR THINKING, CHANGE YOUR, NA MINDSET SECRET. You will never remain the same.
 
Dingi mdogo yupo hai au kafa
Mtafute kwanza yye kama yupo active
Ana mengi yanayoweza kukusaidia kuhusu huyo anayedai mama yako
 
Mtoa mada hapo hatujakuelewa tudadavulie na hapa inakuaje na wakati unasema hujalelewa na mamaako

Screenshot_20220503-113151.jpg
 
Pole mkuu dah nimelia sana! Msamaha ni jambo jepesi kutamka ila utekelezaji wake ni mgumu. Mungu akupe moyo thabiti kwenye hili
 
Baba yangu japo sielewani naye Sana ila iwahi kunishauri kwamba ,nizae na mwanamke mmoja tu yani nisichanganye wanawake,aliishia hapo
nikitafakari kauli yake naona alikuwa sahihi,Kuna ndugu yetu yeye alipenda kuoa na kutelekeza wanawake na watoto then anaenda kuoa kwingine,hivi Sasa ni mzee amestaafu lakini watoto aliotelekeza na kuwakataa Wana Elimu nzuri wapo wanapambania Maisha ila wameshamsamehe japo wanaumia mpaka leo
nilishawahi kuchukia kila mtu dunia hi kidogo nijinyonge, maana niliona nawasumbua tu kunijali. Ila mtihani niliuvuka salama nikasamehe kila mtu. Hadi sasa sinaga rafiki kabsa ni Mimi mama na wadogo zangu na baba kwa mbali. Hiyo ya mzee kuona na kuacha nahisi anayo sema anaogopa kufukuzwa kazi isingekuwa hivyo, kwa sasa tungekuwa na mama tu.
 
Back
Top Bottom