Kwa tuliopitia machozi, jasho na damu katika ukuaji wetu

Pole Sana Kwa mapito na hongera Kwa mafanikio. Acha maisha yaendelee, mtu anayejileta Tena anakwambia "kumbuka Mimi ni Mama yako" mpitishe kwenye chujio fasta.
 
Ningemsamehe lakini nisingekuwa na mapenzi nae wala nisingwletaka ukaribu nae.

Inaonekana anajali sana pesa kuliko utu

Siku yoyote anaweza waletea vitimbi utadhani alikuwepo muda wote kwenye maisha yenu.

Mimi ningempotezea tu

Kama i make it without her why now!?
 
Wachawi wamenipitisha sehemu ngumu
Pasipo Yesu kuingilia kati hali yangu ingekuwa mbaya ambayo nilitamani hata kujiua

Ushari wangu cha kwanza muamini Yesu Kristo kwanza akupe moyo wa msamaha
Hata ukikaa na hiyo chuki baadae utakufa ,kwanini ukikae na kitu moyoni wakati unaweza kusamehe
Mkuu weka mkasa wako kama inawezekana, maana namimi naona kama kuna zengwe flani hivi
 
Am all alone huwa sipendi kuzungumzia Maisha yangu ya hapo awali bse yanaumiza Sana .

Toka mshua aukate dah .. all in all Maisha yanaendelea.

Tuliambiwa mama yenu alishakufa kwa hiyo msikae mkimlilia , Okay Varangati linaanza tulizoea Maisha ya kila kitu KWA wakati lakini Ili bidi tuanze upya , kila mara nikifanya kosa kidogo nitapigwa kama mbwa mwizi , as if walezi wangu walikuwa hawapendi mimi niwepo pale...

I was bright very bright .. nilipokea praises nyingi , zawadi kemkem KWA namna niliyokuwa nikibukua .. lakini niliishi katika familia ambayo haikujua nini umuhimu wa elimu japokuwa baadhi yao walienda shule ila hawakuzitumia taaluma zao, KWA vipigo vikali nikageuka Tarzan , niliishi maporini kula ndizi mbivu ,miwa , kushindia maji au kwenda kudoea KWA watu , I was very young ..
Nilikuwa na ndugu wenye uwezo ila niliishi kama yatima , my sister too was very bright ila kutokana na mateso Aliishia 4m4 baada ya kupata ujauzito too sad na Ilibidi achukue jukumu la kunilea mimi ambalo alishindwa litimiza.

Niliishi kipori pori , nakumbuka kuna kipindi nilikuwa natembea kutoka machame nkuu Hadi bomang'ombe nikijua naweza kufika singida nilipozaliwa , Mara nyingi nilikula mabaki ya vyakula vilivyotupwa na abiria njiani , kuna siku nilikamatwa ña kiu , niliona chupa mbele inae kimiminika nikijua ni maji nilifungua nakupiga funda moja Kubwa damn it ulikuwa ni mkojo , Dah nashindwa kuendelea nafsi inaniuma , machozi yananitoka ... Ninamaumivu makali

KWA ufupi Sana ...
Nimelala Sana nje kwenye Mvua kwenye jua Jambo anmbalo liliharibu performance yangu darasani .. I was expected to do wonders lakini haikuwa hivyo nilikuwa nikiyabeba maumibu makubwa mno ndani yangu , sikuwahi kupata wa kumwambia anisaidie , Nilivyomaliza f4 nilishindwa kuendelea juu ya kukosa ada ,
Nimepigwa Sana .. mateso , and so on and so on .

Nina maumivu mno uzi huu umeongeza maumivu mara dufu .
Pole sana mkuu, japo najua pole pekee haifuti machungu/magumu uliyopitia
 
Huyo msamehe ila asilete mazoea kwenye hela...
Kuna mzee mmoja alimuomba mwanae msamaha alafu baada ya siku 2 akaanza kupiga mizinga 😄😄, kuna wazazi wanajirudi kwasababu tu una unafuu wa maisha, ungekuwa bado umechoka hata usingemuona.

Mimi mtu ambaye hakuwa na mm wakati wa dhiki siwezi kuwa naye karibu abadani,maana najua yupo kimaslahi tu..
 
Habari JF Members.

Majuzi nimepokea meseji kutoka kwa mwanamke wa makamo akinikumbusha kuwa yeye ni MAMA yangu After 25 years ya kupotezana.

Ilikuwa hivi:
Miaka 25 iliyopita stendi ya mabasi ya kwenda mikoani pale UBUNGO mama yetu mzazi alitupeleka ofisi moja ya kukatia ticket sehemu ambayo baba yetu mdogo alikuwa anafanyia kazi, alitufikisha hapo mimi na mdogo wangu anayenifuata wa kiume na kutuacha pale huku akimuachia maagizo Ba mdogo kuwa amtafute kaka yake (baba yetu) amwambie aje achukue watoto wake yeye hana tena muda wa kuishi na mwanaume masikini,fukara na asiye na uelekeo kwenye maisha.

Habari za kipindi hiko zinadai mama alimpata mwanaume mwingine mwenye uwezo kifedha na inasemekana alimuomba kumuoa ila tu kwa sharti hataki watoto ajumuike nao kwenye maisha yao...hivyo ma alichukua maamuzi ya kutubwaga ili tu awezs kukidhi vigezo ya jamaa na waoane.

Baada ya masaa 5 baba anakuja pale Ubungo kutupitia tunaenda kibanda cha chips na kupata chakula then tunarudi home,ila njiani nilipata kujua baba yangu alikuwa kwenye lindi la mawazo kiasi gani,maana tulipanda karibia gari 3 zisizo sahihi mpaka tunafika nyumbani.

Miezi 8 tuliishi bega kwa bega na baba yetu kitu ambacho kilichofanya afukuzwe kazi kule kwa wahindi alipokuwa anafanya kisa Mahudhurio mabovu...

Alirudi nyumbani na kuanza kufanya vibarua vya hapa na pale ili tuweze kuishi..baada ya muda wa kodi yetu kuisha ilitupasa tutafute sehemu ya kuishi maana baba hakuwa tena na uwezo wa kulipa kodi kwa uhakika,tukapelekwa kwa shangazi yetu ambaye mumewe aligoma kabisa sie kuishi pale..alitufanyia visa sana..kuna muda mkiwa mnakula anakuja anawaputa chakula kinamwagika,au mkilala usiku anakuja anavuta sigara bwege/bangi chumbani kwenu basi mtakooa hapo mpaka usingizi unakata.

Shangazi ikabidi amueleze baba kuwa hawezi kuishi na sie maana mumewe hayupo tayari kwa jambo hilo.

Bahati nzuri baba alipata kibarua cha kujenga nyumba kama saidia fundi basi ikawa ndio sehemu yetu ya kushinda,na akimaliza jioni tunalala pale pale kwenye lile pagala mpaka asubuhi anaamkia kazi.

Kuna siku tulikuwa tunatoka town sasa muda wa kugombania daladala pale kariakoo shule ya uhuru baba alifanikiwa kunipitisha dirishani ili nikalie kiti kwanza,kile kitendo cha kugeuka nyuma amchukue na mdogo wangu anakuta mdogo wangu hayupo..anamuita na kukagua daladala nzima bila mafanikio...

Anamuachia maagizo konda anishushe kituo flani kuna fundi viatu ambaye ni rafiki yake kisha atakuja kunipitia..yeye wacha afanye utaratibu wa kumtafuta mdogo wangu.

Saa 5 usiku namuona baba anakuja pale nyumbani kwa fundi akiwa mikono mitupu ikiashiria hajampata mdogo wangu..nasikia wakiongea kuwa kaishatoa taarifa kila sehemu hivyo tusubirie taarifa kutoka huko.

Baada ya wiki baba anaenda kituo cha polisi biguruni na kusikia habari kuna mtoto kaletwa pale na msamaria mwema,sema itabidi aje kesho maana kuna afande wa zamu kaondoka nae kumuhifadhi kwake..

Kesho baba anaenda tena na kufanikiwa kumkuta mdogo wangu na kurudi nae,nilifurahi sana siku ile...japo kuna jambo huwa mpaka leo mdogo wangu hapendi kunihadithia au kuniambia nini kilitokea..maana alivyorudi alikuwa na vidonda kwenye magoti,kapasuka mdomoni,afu kachanika pakubwa sana mgongoni kama mtu aliyekuwa anateswa....kumbuka mdogo wangu kipindi hiko alikuwa na miaka 3.

Hata yule afande alisema nilishangaa sana yule mtoto kipindi ameletwa pale kituoni jinsi alivyokuwa na vidonda vile.

Kwa ufupi baba badae alipokea ujumbe kutoka kijijini kwa bibi kuwa atupeleke maana anasikia maisha tunayoishi huku town ni hatari sana...

Nakumbuka siku tuliyosafiri kwenda kwa bibi almost tulitumia masaa 9 kwenye Bus bila kula ,tulitepeta kiasi cha kushindwa hata kuongea kwa jinsi njaa ilivyokuwa imetupiga...nilikuwa kama mpira uliotolewa upepo sijiwezi ila namshukuru Mungu tulifika salama kwa bibi na kupewa uji.

Kesho yake baba aliondoka kurudi Town.

Tuliishi na bibi kipindi chote hiko.

Mpaka tulipopata taarifa za kutatanisha kuhusu baba yetu kuna waliosema kafungwa maisha,kuna waliosema kagongwa na gari Tazara na kufariki hapo hapo...

Bibi aliuza kila kitu ili tuweze kusoma na tulisoma mpaka bibi yetu yalipomkuta mauti...SITOMSAHAU BIBI YANGU..

Leo mimi ni Accountant private sector na mdogo wangu ni Engineer Public sector.

Majuzi nimepokea meseji ya mwanamke akiniomba niende whatsap anitumie picha za kumbukumbu ili niweze kumtambua kama ndio MAMA YETU.

katika ile picha huyu MAMA kakaa mie nimemlalia miguuni na mdogo wangu kamuegemea begani tukiwa kwenye tabasamu zito.

Inasemekana ndio siku za mwisho mwisho kuwa karibu na MAMA yetu...

Nimemtafuta baba yangu magereza yote sijampata labda kweli aligongwa gari akafariki.

Sijajibu mpaka sasa meseji za huyu mama..anapiga sana simu kila siku.
Kibinadamu ni ngumu kusamehe
Lakini kama ni Mkristo msamaha ni lazima.

Kipimo sahihi cha hukumu anacho Mungu..
Wewe unaweza kuonya tu Kwa ukali .
Usishinde ubaya kwa ubaya bali ushinde ubaya kwa wema.

Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhi..
Inawezekana vipi?
Kwa Roho Mtakatifu..
Yeye ni tunda la upendo mahala palipo na chuki.

Kumbuka hekima ya Mungu Kwa wanadamu ni upumbavu.
 
Mkuu wanaokushauri ukae nae chini akwambie sababu pengine wanaweza kuwa hawana maana yoyote..

Unajua ata ukikaa nae chini atakachokwambia hakitakua balance kwa sababu unakuwa unasikiliza upande mmoja tu wa mzani kwingine hujui ivyo ni rahisi upande mwingine kupewa lawama.

Japo unapaswa umsamehe Lakin jua wababa uwa wanabeba siri nzito sana za wakina mama sema ni vile tu hawanaga time ya kukaa chini kuwajaza maneno watoto. Je unafikiri muda wote huo alishindwa kwel kuja kwa mume wake na kwanini awaache kwa baba mdogo wenu? Kwa nini hakuwapeleka Moja kwa Moja kwa baba mzazi?.

Uamuzi ni wako kaa chini na mdogo wako japo msamaha ni bora Zaid Lakin nakumbuka Kwny familia yet wenyewe ilitokea ish kama yako ila mama yy tulienda nae Moja kwa Moja kwa faza na tukaishi nae pamoja kutoka kijijin mpaka dar ambapo mzee alikuwa anafight na mpaka kesho wanaishi pamoja na wanazeeka pamoja katika kila Hali ya maisha.
 
Mkuu wanaokushauri ukae nae chini akwambie sababu pengine wanaweza kuwa hawana maana yoyote..

Unajua ata ukikaa nae chini atakachokwambia hakitakua balance kwa sababu unakuwa unasikiliza upande mmoja tu wa mzani kwingine hujui ivyo ni rahisi upande mwingine kupewa lawama.

Japo unapaswa umsamehe Lakin jua wababa uwa wanabeba siri nzito sana za wakina mama sema ni vile tu hawanaga time ya kukaa chini kuwajaza maneno watoto. Je unafikiri muda wote huo alishindwa kwel kuja kwa mume wake na kwanini awaache kwa baba mdogo wenu? Kwa nini hakuwapeleka Moja kwa Moja kwa baba mzazi?.

Uamuzi ni wako kaa chini na mdogo wako japo msamaha ni bora Zaid Lakin nakumbuka Kwny familia yet wenyewe ilitokea ish kama yako ila mama yy tulienda nae Moja kwa Moja kwa faza na tukaishi nae pamoja kutoka kijijin mpaka dar ambapo mzee alikuwa anafight na mpaka kesho wanaishi pamoja na wanazeeka pamoja katika kila Hali ya maisha.
Asante mkuu,
Kwa ushauri mzito na mzuri.
 
Kibinadamu ni Mungu kusamehe
Lakini kama ni Mkristo msamaha ni lazima.

Kipimo sahihi cha hukumu anacho Mungu..
Wewe unaweza kuonya tu Kwa ukali .
Usishinde ubaya kwa ubaya bali ushinde ubaya kwa wema.

Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhi..
Inawezekana vipi?
Kwa Roho Mtakatifu..
Yeye ni tunda la upendo mahala palipo na chuki.

Kumbuka hekima ya Mungu Kwa wanadamu ni upumbavu.
Ahsante Madam,
Nimekupata vyema.
 
WANAOKUAMBIA UMSAMEHE NI WAPUUZI KIWANGO CHA LAMI NI MAFALA WANGEKUWA WAMEPITIA HIZI SITUATION WANGEELEWA

NA MIMI NIMEPITIA HAYA NA NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA ILI UONE MSIKILIZE ANATAKA NINI PIA MUULIZE KUHUSU FATHER MPOTEZEEE
Shukrani mkuu,
Japo sidhani kama nitampa muda wa kumsikiliza maana nimepambana mno kuyasahau ya nyuma.
 
Back
Top Bottom