Kwa tuliopitia machozi, jasho na damu katika ukuaji wetu

Mtoa mada hapo hatujakuelewa tudadavulie na hapa inakuaje na wakati unasema hujalelewa na mamaako

View attachment 2209575
Watu mnajua kufukunyua Mambo
 
Hii story yako inanikumbusha watoto flani wa ki sure, mama yao aliwaacha na kulewa na mwanajeshi. Baba yao aliwalea single handed mpaka alipokuja kuoa.

Bahati mbaya baba alifariki na walilelewa na mama wa kambo mpaka wanakua wakubwa.
Very interesting,madam.
 
Hakuna kitu natafuta kwa nguvu kama hela humu dunian na hakuna kitu nakichukia kama hela. Sababu hela zimeshindwa kutufanya kujua watu halisi. Watu wanaweza kuwa karibu yako ukadhan wako na wewe kumbe wako karibu na hela zako. Zikikata na wenyewe wanakata. Unaweza kuona huyu mama alivyojisahau
 
Hata sijui nikushauri nini, maana hata mimi ninayakwangu, na sioni kama ushauri wa mtu utabadilisha chochote, basi nimebaki mimi tu na Imani yangu.

Ila ninaelewa sana situation unayopitia kwa ambaye hajawahi kusimama nafasi ambayo umesimama wakati huu, anaweza akaona ni rahisi tu, kutoa ushauri lakini waliopitia hizo hali wanaelewa.

Yaani unajua kabisa what is the right thing to do, lakini......... Mwenyezimungu atuongoze.

Nikupe pole kwa unayoyapitia.
Kabisa anaemuelewa ni mtu aliyepitia
Kutelekezwa na mam kisa tu penzi jipya ni ngumu kwa moyo was kibinadamu kusamehe
 
Dah jamani so sad baba Yako angekuwepo angekuwa anafaidi matunda ilishindikanaje kujua alipo? Kipindi anapotea hamkuuliza taarifa zake? Mkuu pôle Sana sipati picha maumivu unayopotia emotional, mungu awape Imani
 
Pole sana mkuu sina cha kusema.. maana nawapenda wazazi wangu hatari naona ushahuri wangu kama ntawakandamiza wazazi wangu.. M/Mungu atukubali hivyo hivyo tu InshAAllah
 
Kama vile naitazama ile filam ya JB, "NAENDA KWA MWANANGU". Nakuelewa jinsi unavyoumia zaidi kwa machungu ya
hiyo past yako mkuu, yaani bora asingetokea muda huu, uwepo wake kama vile hauna thamani tena kwenu.
Kila jambo hutokea kwa sababu, hata usipomsamehe bado ukweli huwezi kuupinga kamwe, she will still be your mother
 
Mtoa mada hapo hatujakuelewa tudadavulie na hapa inakuaje na wakati unasema hujalelewa na mamaako

View attachment 2209575
😂😂😂
 
Habari JF Members.

Majuzi nimepokea meseji kutoka kwa mwanamke wa makamo akinikumbusha kuwa yeye ni MAMA yangu After 25 years ya kupotezana.

Ilikuwa hivi:
Miaka 25 iliyopita stendi ya mabasi ya kwenda mikoani pale UBUNGO mama yetu mzazi alitupeleka ofisi moja ya kukatia ticket sehemu ambayo baba yetu mdogo alikuwa anafanyia kazi, alitufikisha hapo mimi na mdogo wangu anayenifuata wa kiume na kutuacha pale huku akimuachia maagizo Ba mdogo kuwa amtafute kaka yake (baba yetu) amwambie aje achukue watoto wake yeye hana tena muda wa kuishi na mwanaume masikini,fukara na asiye na uelekeo kwenye maisha.

Habari za kipindi hiko zinadai mama alimpata mwanaume mwingine mwenye uwezo kifedha na inasemekana alimuomba kumuoa ila tu kwa sharti hataki watoto ajumuike nao kwenye maisha yao...hivyo ma alichukua maamuzi ya kutubwaga ili tu awezs kukidhi vigezo ya jamaa na waoane.

Baada ya masaa 5 baba anakuja pale Ubungo kutupitia tunaenda kibanda cha chips na kupata chakula then tunarudi home,ila njiani nilipata kujua baba yangu alikuwa kwenye lindi la mawazo kiasi gani,maana tulipanda karibia gari 3 zisizo sahihi mpaka tunafika nyumbani.

Miezi 8 tuliishi bega kwa bega na baba yetu kitu ambacho kilichofanya afukuzwe kazi kule kwa wahindi alipokuwa anafanya kisa Mahudhurio mabovu...

Alirudi nyumbani na kuanza kufanya vibarua vya hapa na pale ili tuweze kuishi..baada ya muda wa kodi yetu kuisha ilitupasa tutafute sehemu ya kuishi maana baba hakuwa tena na uwezo wa kulipa kodi kwa uhakika,tukapelekwa kwa shangazi yetu ambaye mumewe aligoma kabisa sie kuishi pale..alitufanyia visa sana..kuna muda mkiwa mnakula anakuja anawaputa chakula kinamwagika,au mkilala usiku anakuja anavuta sigara bwege/bangi chumbani kwenu basi mtakooa hapo mpaka usingizi unakata.

Shangazi ikabidi amueleze baba kuwa hawezi kuishi na sie maana mumewe hayupo tayari kwa jambo hilo.

Bahati nzuri baba alipata kibarua cha kujenga nyumba kama saidia fundi basi ikawa ndio sehemu yetu ya kushinda,na akimaliza jioni tunalala pale pale kwenye lile pagala mpaka asubuhi anaamkia kazi.

Kuna siku tulikuwa tunatoka town sasa muda wa kugombania daladala pale kariakoo shule ya uhuru baba alifanikiwa kunipitisha dirishani ili nikalie kiti kwanza,kile kitendo cha kugeuka nyuma amchukue na mdogo wangu anakuta mdogo wangu hayupo..anamuita na kukagua daladala nzima bila mafanikio...

Anamuachia maagizo konda anishushe kituo flani kuna fundi viatu ambaye ni rafiki yake kisha atakuja kunipitia..yeye wacha afanye utaratibu wa kumtafuta mdogo wangu.

Saa 5 usiku namuona baba anakuja pale nyumbani kwa fundi akiwa mikono mitupu ikiashiria hajampata mdogo wangu..nasikia wakiongea kuwa kaishatoa taarifa kila sehemu hivyo tusubirie taarifa kutoka huko.

Baada ya wiki baba anaenda kituo cha polisi biguruni na kusikia habari kuna mtoto kaletwa pale na msamaria mwema,sema itabidi aje kesho maana kuna afande wa zamu kaondoka nae kumuhifadhi kwake..

Kesho baba anaenda tena na kufanikiwa kumkuta mdogo wangu na kurudi nae,nilifurahi sana siku ile...japo kuna jambo huwa mpaka leo mdogo wangu hapendi kunihadithia au kuniambia nini kilitokea..maana alivyorudi alikuwa na vidonda kwenye magoti,kapasuka mdomoni,afu kachanika pakubwa sana mgongoni kama mtu aliyekuwa anateswa....kumbuka mdogo wangu kipindi hiko alikuwa na miaka 3.

Hata yule afande alisema nilishangaa sana yule mtoto kipindi ameletwa pale kituoni jinsi alivyokuwa na vidonda vile.

Kwa ufupi baba badae alipokea ujumbe kutoka kijijini kwa bibi kuwa atupeleke maana anasikia maisha tunayoishi huku town ni hatari sana...

Nakumbuka siku tuliyosafiri kwenda kwa bibi almost tulitumia masaa 9 kwenye Bus bila kula ,tulitepeta kiasi cha kushindwa hata kuongea kwa jinsi njaa ilivyokuwa imetupiga...nilikuwa kama mpira uliotolewa upepo sijiwezi ila namshukuru Mungu tulifika salama kwa bibi na kupewa uji.

Kesho yake baba aliondoka kurudi Town.

Tuliishi na bibi kipindi chote hiko.

Mpaka tulipopata taarifa za kutatanisha kuhusu baba yetu kuna waliosema kafungwa maisha,kuna waliosema kagongwa na gari Tazara na kufariki hapo hapo...

Bibi aliuza kila kitu ili tuweze kusoma na tulisoma mpaka bibi yetu yalipomkuta mauti...SITOMSAHAU BIBI YANGU..

Leo mimi ni Accountant private sector na mdogo wangu ni Engineer Public sector.

Majuzi nimepokea meseji ya mwanamke akiniomba niende whatsap anitumie picha za kumbukumbu ili niweze kumtambua kama ndio MAMA YETU.

katika ile picha huyu MAMA kakaa mie nimemlalia miguuni na mdogo wangu kamuegemea begani tukiwa kwenye tabasamu zito.

Inasemekana ndio siku za mwisho mwisho kuwa karibu na MAMA yetu...

Nimemtafuta baba yangu magereza yote sijampata labda kweli aligongwa gari akafariki.

Sijajibu mpaka sasa meseji za huyu mama..anapiga sana simu kila siku.
Poleni sana. Kila la heri waungwana. Jaribu kumtafuta umsikize tu, maana haya mambo huwa yana tabia ya kujirudia kwa vizazi vijavyo
 
Mtoa mada hapo hatujakuelewa tudadavulie na hapa inakuaje na wakati unasema hujalelewa na mamaako

View attachment 2209575
Huyu mleta uzi ajitafakari
 
Back
Top Bottom