Waterloo
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 25,356
- 38,908
Habari za jioni wadau,
Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza,
Wakati wa uchumba na mwanamke ambaye alikuja kuwa mke wangu nilikuwa na mawasiliano ya karibu na upande wa mke wangu anyway naweza kusema ilikuwa haipiti wiki moja au mbili nitawapigia kuwajulia hali nakadhalika.
Lakini tangu nimemuoa nimekua mzito sana kiasi kwamba naweza kukaa mwezi mzima bila kupiga simu kuwajulia hali. Na hii ni kwa wakwe zangu na mashemeji zangu pia.
Sasa nilikuwa naomba kuuliza kwa wenzangu nyie ambao nanyi mna nyumba zenu, je huwa mnawasiliana mara ngapi kwa wakwe zenu kwa wiki au mwezi? Na je kuna ubaya wowote kama mimi ninapata habari zao kupitia kwa mke wangu bila kuwapigia simu?