Pengo alitoa tamko baada ya mlipuko wa kwanza wa bomu Arusha ambapo watu wengi walimbeza lakini baadaye imeonekana kweli. Pia Mbunge wa Arusha Lema alitoa tamko lililobezwa pia, sasa hayohayo yaliyotokea wakati huo yamejirudia tena. Sasa tutawaaminije viongozi wetu wanaokataa kuwajibika wakati wameshindwa kulinda usalama wa Watanzania. Jamani Watanzania tukatae kuchezewa na watu wauaji ambao ni kama mchawi anayekulia mtoto wako halafu anakuwa wa kwanza kuja kukupa pole. Hivi RC kama mlongo ambae juzi tuu tukio limetokea mkoani kwake atatuambia nini tumuelewe, hali kadhalika Nchimbi na Mwema. Rais wetu anayemndisha cheo Mtu kama Kamhanda Watanzania mnaona nini hapo, tusichezewe jamani kama wajinga. Hivi Bunge letu haliyaoni haya? kwanini wasipige kura ya kutokuwa na imani na Rais anayetoa pole kila mauaji yakitokea bila hatua stahiki kuchukuliwa. Kama kweli wabunge hawa ni ndugu zetu, jamaa zetu, Baba/Mama zetu au watoto wetu sasa ni wakati wa kuwashinikiza wachukue hatua. Tuone sasa ni muda muafaka wa kuweka kwenye mchakato wa katiba mpya kipengele kinachoruhusu mtu yeyote kushitaki Rais aliye madarakani kama atatenda uhalifu wowote akiwa madarakani au kushindwa kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa katiba. Karibuni kwa michango yenu kwa moyo wa dhati bila ushabiki ila kutokana na hali halisi.