Kwa tra, wizara ya viwanda na biashara na wizara ya maliasili na utalii, na tic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa tra, wizara ya viwanda na biashara na wizara ya maliasili na utalii, na tic

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Oct 28, 2011.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Kwa wizara tajwa hapo juu.

  kuna haya makampuni ya utalii yanayo milikiwa na wazungu kutoka nje ambayo yanajihusisha na kupeleka wageni kwenye hifadhi zetu na vivutio vingine kama mlima kilimanjaro

  haya makampuni karibia yote akaunti za fedha zao ziko hukohuko kwao na wageni/watalii hulipia huko huko kabla ya kuja tz na huku huja na pesa my b za hotel na kununua vinyago.

  Sasa basi.

  1, je ni nani anafanya auditing ya haya makampuni kujua faida waliyo ipata wakati akaunti zao haziko tz?
  2. Tra wanawalipisha vipi hawa watu kodi? Je wanakadiria?
  3. Sheria za uwekezaji zinasemaje? Ni ruhusu kampuni kuwekeza tz wakati akaunti ya hiyo kampuni na payment zote zinafanyika my be marekani, au ulaya?

  wakuu kwa kweli inasikitisha sana, haya makampuni huku arusha na kwingineko kuna ofisi pekee lakini kila kitu kuanzia wakurugenzi na akaunti za makampuni yao na payment zote hufanyika ulaya, marekani na kwingineko.
   
 2. Ras

  Ras Senior Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabisa mkuu, kwa kweli inasikitisha. Na hii si kwamba haifahamiki, inafahamika lakini sababu wakuu wetu washapewa 10% Wanaziba masikia. Mimi nadhani mbali ya kuchagua viongozi ambao wana uchungu na nchi hii, pia ni vyema tukafuata wazo la Mbowe (Naomba nisieleweke kama ni shabiki wa siasa bali shabiki wa sera endelevu). Hii nchi ni kubwa sana na ina resources nyingi ila kutokana na ukubwa huu kuna wajanja wanautumia kama upenyo wa kutuhujumu. Tukiigawa katika majimbo na kila jimbo likawa na management ya resources zake itatusaidia kumanage vyema hizi resources. ndivyo wenzetu wengi walioendelea na wanaoendelea kwa kasi wanavyofanya (S. Korea, America, S. Africa n.k.). Wengine wanaingiza hili katika udini na kwamba livunja umoja wetu hii si kweli. Karibu kila kanda ina resources ambazo kwa namna moja au nyingine kanda ingine inategemea. Mfano kanda ya Kusini, wanazalisha chakula, Umeme (Mtela), Utalii (Ruaha, Selous), Gas (Songpsongo),Makaa ya mawe (Kiwira). Kanda ya kaskazini utalii (Kilimanjaro, Serengeti,Ngorongoro, Meru n.k.). Kanda ya Ziwa (Uvuvi-Ziwa victoria, Utalii, Kilimo mazao ya biashara-Pamba, Madini n.k.), Kanda ya magharibi (Kilimo mazao ya chakula, Uvuvi, utalii n.k.).
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i would love this thread to be "sticky"

  Tunaibiwa sana na wageni
   
Loading...