Kwa tff na wapenda michezo tz!!

Amon

Member
Oct 17, 2010
49
3
Kulingana na hali halisi iliyotokea katika mashindano haya ya CECAFA yanayoendelea, ninawashauri TFF na wapenda michezo wote wa Tanzania, tujitoe CECAFA na kujiunga COSAFA, sababu mnazifahamu nanyi pia, ila kikubwa katika hali halisi mnayoiona hakika hakutatokea hata siku moja mpira ukandelea kukua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, perhaps miujiza itokee. Tutaendea kuwa chini katika ubora mpira wa miguu duniani. Hakika nawaambieni!!!!
 
Tukijiunga COSAFA ndio tutaweza kuinua vipi kiwango chetu cha soka?
 
CECAFA ni yetu, sisi ndio waanzilishi tangu enzi za Gossage. Kama kuna kasoro (au changamoto kama yanavyoitwa siku hizi), sisi ndio wa kuyarekebisha. Tujitoe ili tumwachie nani?
 
Nini tatizo uliloliona CECAFA kiasi cha kushauri tujitoe na nini kikubwa ulichokiona COSAFA mkuu,tujuze.
 
Mimi naona tuache kupoteza hela nyingi kulipa makocha wa nje, tena wanaotoka nchi ambazo kimpira haziko juu kihivyo. Mshahara unaotumika kumlipa kocha kwa mwezi, ukichukua mshahara wake wa nusu mwaka, unaweza kupeleka makocha kadhaa wa KiTanzania nchi za Ulaya wabrush-up skills zao.
Pia, hatuna misingi ya kutengeneza vijana chipukizi. Kuna tabia ya kurudisha wachezaji umri....haisaidii inadumaza vibaya sana na sio ujanja. Tuache shortcut. Kucheza CECAFA au COSAFA makes no difference kama misingi yetu ni mibovu.
 
]Mimi naona tuache kupoteza hela nyingi kulipa makocha wa nje, tena wanaotoka nchi ambazo kimpira haziko juu kihivyo. Mshahara unaotumika kumlipa kocha kwa mwezi, ukichukua mshahara wake wa nusu mwaka, unaweza kupeleka makocha kadhaa wa KiTanzania nchi za Ulaya wabrush-up skills zao.[/B]
Pia, hatuna misingi ya kutengeneza vijana chipukizi. Kuna tabia ya kurudisha wachezaji umri....haisaidii inadumaza vibaya sana na sio ujanja. Tuache shortcut. Kucheza CECAFA au COSAFA makes no difference kama misingi yetu ni mibovu.

Hili jambo muhimu sana kama uongozi mpya watalifanyia kazi,sijawahi kusikia kocha wa Tanzania ameenda kusoma nje.Charles Mkwasa,Sekilojo Chambua,Kenny Mwaisabula,Seleman Matola,Amri Said,Salvatory Edward,Mecky Mexime,Sylivester Mash,Keneth Mkapa,Ally Bushiri,Julio na wengine wengi hawa TFF ingewapeleka nje kwenda kuongeza ujuzi wangesaidia sana kukuza mpira wetu.Tunaongea kuanzisha academy na kuanzisha timu za watoto lakini hatuna makocha wa kufanya hiyo kazi
 
hivi ni jukumu la tff kupeleka makocha nje wakasomee,kwanini wasiendee kujiendeleza wenyewe kwa pesa yao na mipango,ama haiwezekani mpaka tff iwapeleke?
 
Ni expensive kwao ni ngumu sana mtu kama Matola au Julio ajilipie kwenda kusoma Ulaya
 
Sio kazi ya TFF. Lakini kama TFF wako tayari kulipa kocha wa kizungu pesa nyingi, wakati kocha wenyewe ni wa kawaida kabisa, kwani wasifikirie outside of the box? Makocha wazawa wanaweza wakiwezeshwa. Pointi yangu, ni kwanini umwage pesa nyingi kwa makocha wa kigeni wakati system ya ku-feed national team ni mbovu?
Pia chama cha mpira kutoa "msaada" kwa wananchi wake ni kwa manufaa ya nchi. Mfano, Uholanzi, wachezaji mpira waliopitia national team huwa wanapewa kozi ya ukocha kwa kufupishiwa muda ukifananisha na mtu ambaye hakucheza mpira katika level ya juu. Au chukulia mfano nchi za Ulaya zinapotoa scholarships kwa WaTanzania katika masomo mbalimbali bila masharti zaidi ya kurudi nyumbani kutumikia nchi. Wanafanya hivyo wakijua mtu akirudi nyumbani ataleta maendeleo fulani.
Nasema hivi kwasababu, kwanza makocha wazawa wakipewa kazi kufundisha timu ya taifa hawalipwi vizuri ukifananisha na wazungu....case in point Steven Keshi. Leo hii hata ukimleta Fergusson au Mourinho, hawatafanikiwa, misingi yetu ni mibovu!!
 
Nadhani Kwa sasa Stars irudi kwa mzawa, tena Silvester Marsh, naamini akipewa hii timu tutaona mabadiliko, huyu Poulsen afukuzwe tu amejaa ubishi mkubwa na hakuna jipya alilofanya zaid ya kuturudisha hatua Miami moja nyuma
 
wakuu dfk-agent na Belo hizo kozi za ukocha nje ya nchi ambazo ni expensive sana shs ngap mpaka makocha wazawa wasiweze?,kuna wananchi wa kawaida tu ambao wanajinyima na kuzichanga ili kufanikisha malengo yao na kwenda ng'ambo sasa kwa nini makocha wazawa washindwe?.Ni kweli pia makocha wa kigeni si wazungu tu hata waafrika wenzetu wakija bongo wanalipwa vizuri kuliko wazawa lakin najiuliza kwa nini hawa wazawa wetu hawatoki nje kufundisha na wao kulipwa vizuri huko?,mbona kina SIANG'A,PHIRI,TIMBE,MAYANJA..........etc etc kutoka nchi jirani tu wanakuja kwetu kila uchwao na kuonesha uwezo wao na tunaukubali na pesa wanapata sasa wazawa wetu kulikoni?.Kuna tatizo nahisi na kama wanasubiri tff iwawezeshe nafikiri kuna tatizo kubwa sana.Binafsi naona tuendelee kuwatumia makocha wageni labda tuangalie tunawapataje na tunawatoa wapi?.
 
Mimi naona tuache kupoteza hela nyingi kulipa makocha wa nje, tena wanaotoka nchi ambazo kimpira haziko juu kihivyo. Mshahara unaotumika kumlipa kocha kwa mwezi, ukichukua mshahara wake wa nusu mwaka, unaweza kupeleka makocha kadhaa wa KiTanzania nchi za Ulaya wabrush-up skills zao.
Pia, hatuna misingi ya kutengeneza vijana chipukizi. Kuna tabia ya kurudisha wachezaji umri....haisaidii inadumaza vibaya sana na sio ujanja. Tuache shortcut. Kucheza CECAFA au COSAFA makes no difference kama misingi yetu ni mibovu.
Wazo la kupeleka makocha wazawa nje ni zuri mno lakini linahitaji umakini mno. Labda tuanze na makocha vijana amboa bado hawajaathirika na mfumo wa soka letu. Makocha wazawa ambao wamekwisha fundisha mpira kwenye ligi kuu wengi wao unaweza kusema ni too late kuwabadilisha. Hili nimeliona mara kwa mara kila wakiitwa kwenye vyombo vya habari hasa radio na TV wachambue mechi. Wengi wao hata kujielezea ni shida tupu...Mwalimu asiyeweza kujielezea atawaelezeaje wachezaji! Angalia documentary ya Twiga Stars: Tanzania soccer sisters kuna sehemu Mkwasa anawaambia kabisa wachezaji wake wabutue mpira mbele ilhali wanaongoza! Sikiliza mahojiano ya JulioHawa ndio makocha wetu wazawa, wengi wamegoma kabisa kujiendeleza kabisa. Mfano mwingine ni Sunday Kayuni, amesoma, ana PRO Licence, lakini anaifanyia nini?
Hili la kuajiri makocha kutoka nje ambao viwango vyao si vya kutisha ni gumu kukwepeka kwa sababu ya maslahi. Kina Keshi, Henri Michel na Herve Renard wanataka mishahara ya kuanzia milioni 80 kwa mwezi. Sidhani kama TFF inaweza kumudu hizi gharama.Ukiangalia hata jirani zetu Zambia, mshahara wa Herve Renard wa milioni mia kwa mwezi ulikuwa unaelekea kuwashinda licha ya makampuni kadhaa ya madini kuchangia kumlipa.
Nakubali kabisa, tuache shortcut, turudi kwenye grassroot football huko ndio ubovu unapoanzia.
 
Tatizo la CECAFA ni Musonye,Tenga anaingizwa 'king' bila kujijua,maana mwenzie yuko kimaslahi zaidi....
 
Sawa, ila umeniquote vibaya kuhusu Keshi, si maanishi aje kwetu, yaani naongelea kwao huko huko. Yeye analipwa mshahara kidogo ukifananisha na mzungu akipewa hiyo kazi. Kazi yenyewe anaweza kuifanya vizuri kabisa if not better.
Pia, sio makocha wote walio Tanzania wanaweza kutema mayai, maana kupeleka nje hicho ni muhimu. Sijawahi kuongea na Kayuni, lakini nimeongea mara kadhaa na Kaijage na Marsh. Jinsi wanavyoongelea mchezo na ku-analyse wachezaji unaona kabisa hawa jamaa wanahitaji kutumiwa vizuri na kuwezeshwa. Kwahiyo sio makocha wote waliokwenda umri hawawezi kutumika.
Pia, kupeleka nje makocha inaweza kuwa internship tu katika club au football federation fulani kwa wiki/miezi kadhaa. You will surprised what assistance is out there.
 
Well said, na makocha wazawa inabidi wawe aggressive sio tu kusubiri nasi za kocha msaidizi kwenye vilabu vya Simba na Yanga au timu ya Taifa...Hata ukiangalia Keshi, Nigeria hawakumpa nafasi tu hivi, alitoka nje na kudhibitisha ubora wake ndipo wakampa hio nafasi. Hata kama wanaonekani hawafai Simba, Yanga na Taifa Stars kwa nini wasijaribu nchi za jirani? Watasubiri nafasi za upendeleo kama wazawa mpaka lini? Hizi ni zama za ushindani.Nenda Burundi, beba ubingwa...heshima lazima itapanda.
Kuna watu waliomba kazi kwenye mainstream media hapa Tanzania na kukataliwa lakini wakaja kwenye social media kama JF na kuzitumia vizuri na leo hii the same mainstream media zinawataka...It is all about being aggressive kuliko kusubiri affirmative action. Makocha wazawa wanatakiwa kupambana. Heshima yao haitakuja kwa sababu eti ni wazawa.
Tena bahati mbaya kwa vigezo vipya vya leseni vilivyotolewa na CAF hivi majuzi ni Kayuni pekee ndio anaweza kuwa kocha mzawa wa timu ya Taifa. The qualification bar has been raised, local coaches need to raise their standards. Kuna Watanzania kibao wanaopokea mishahara ya chini ya laki sita lakini bado wanajibana na kuweza kujiendeleza zaidi.
 
Kulingana na hali halisi iliyotokea katika mashindano haya ya CECAFA yanayoendelea, ninawashauri TFF na wapenda michezo wote wa Tanzania, tujitoe CECAFA na kujiunga COSAFA, sababu mnazifahamu nanyi pia, ila kikubwa katika hali halisi mnayoiona hakika hakutatokea hata siku moja mpira ukandelea kukua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, perhaps miujiza itokee. Tutaendea kuwa chini katika ubora mpira wa miguu duniani. Hakika nawaambieni!!!!

Kwa taarifa yako Malawi walikuwa wanachama wa CECAFA wakajitoa wakaenda huko COSAFA hali yao bado ni tete; haya, Zambia wanachama wa COSAFA punde tunacheza nao kutafuta mshindi wa 3. Kujitoa siyo suluhisho. TFF wabuni mbinu za kupata makocha wa kuaminika sio makocha aina ya Marsh na Poulsen wanaobahatisha hata kupanga timu. Mimi siyo kocha, laiti ningepewa hiyo timu walahi Kenya wasingetoka salama siku hiyo. Tatizo letu kubwa ni technical bench! Pamoja na hujuma za hapa na pale kama Kenya walivyojaribu kufanya hivyo ni vitu vya kawaida sana katika mpira haviwezi kutufanya tujitoae. Kama Mkuu wa Nchi alivyosema kuwa TZ itakuwa ya mwisho kujitoa EAC vivyo hivyo TZ iwe ya mwisho kujioa CECAFA. Hata hivyo ajira ya Musonye nayo imekuwa ya muda mrefu sana, naye ang'olewe kwa kupewa likizo ya malipo wakati mkataba wake ukisubiriwa ufikie tamati kama ilivyofanyika kwa 'Musonye' wa TFF.
 
Ni expensive kwao ni ngumu sana mtu kama Matola au Julio ajilipie kwenda kusoma Ulaya
Kwani lazima wawe hao tu? Tatizo ni kuwa wazazi hawajabaini umuhimu wa elimu ya ukocha wa soka. Mbona kwa masomo wanayoyahisi muhimu huwawanawapeleka watoto wao kwenye kozi ghali zaidi na kwenye vyuo ghali zaidi duniani? Tusiwalaumu TFF peke yao, hata sisi wenye uwezo wa kusomesha nje na tusifanye hivyo,tunapaswa kulaumiana.
 
Kuna tatizo tff hasa mkurugenzi wa ufundu huyo ndio anawajibika kwa mambo yote ikiwamo kuhakikisha maswala ya mafunzo kwa makocha wakati poulsen babu alipokuwepo alikuwa mara nyingi akitumiwa na fifa kwenda kuendesha kozi mbalimbali za ukocha duniani lakini cha ajabu TFF walishindwa kumtumia kabisa nashukuru nafasi ya Sunday kayuni imetangazwa upya ni matumaini yangu huyo atakayekuja atatutengenezea mfumo mzuri wa kupata makocha lakini na vilabu pia vinapaswa kulaumiwa kwani vimeshindwa kuwekeza kwa makocha badala yake wamekuwa wakitumia pesa nyingi kulipa makocha wa nje kwa kifupi hawana mipango endelevu lakini hata hao makocha wazawa mnaowapigia debe ni lini marea ya mwisho wamehudhuria kozi nakumbuka kuna kipindi zilipotoka nafasi tulishuhudia watu waliokwenda wengi waliachwa mpaka naibu waziri Kasim majaliwa naye pia alikwenda tatizo liko tff
 
Bandugu bangu, kusomesha akina Julio nje sio solution ya kuwa na timu nzuri ya Taifa. Cha msingi ni kuwa na mfumo mzuri katika klabu kuanzia daraja la 4 hadi premier, sana sana ktk academy level, U 10, 12, 14, 15, 17 na 18. Njia moja kuu ni kwa TFF kutafuta sponsors au kuwabana waliopo wawekeze huko chini kwa watoto. Serikali iludishe umishumta na umiseta na hapo ukiongeza na mfumo wa miaka ile ya 80s ambapo tulikuwa tunapata mechi za kirafiki za kimataifa kila miezi kadhaa ndo soka litakua. Walete klabu kubwa au timu zilizo juu ktk ranking ya FIFA tufungwe hata 10-0 lakini over time exposure hiyo inasaidia.

Binafsi naamini sana Simba ndiyo kama imetufumbua macho na kutuamsha usingizini pale Babu alipoamua kutumia Yosso tuu. Haya mambo ya kusajili magarasa ya nje eti Burundi, Rwanda, Kenya au Congo yanatugharimu. Ona babu wa France alivyowakolesha vijana wa Matola, akawajenga kisaikolojia na wakapewa motisha uwanjani ni balaa. Tunahitaji u 10, na kuendelea na huko tutapika vipaji vingi na kuachana na hawa mabishoo wa vibwenzi kama Ngasa ect..

Soka kama michezo mingine inapikwa kuanzia chini, sio unakuta timu ya taifa players hawawezi hata kupiga danadana 10, sasa huyo kweli utamfundisha formation mbalimbali ?? Au tunategemea players mpaka wavute bangi kwanza ndo watapiga mashuti..

Tuna uwezo mkubwa sana na hazina ya players (Ona Mecco, Mbeya City n.k) lakini mipango mibovu na kuleta makocha kisiasa...

Tena kukomesha TFF wanaweza weka limit ya age, kama ilivyo ya foreign players kuwa kila timu ya premier iwe na say only/maximum 5 players over 26 yrs.

Mashindano ya U 17 na U 19 yakipata sponsors na wakawa na ligi kama ya premier tutacheza world cup !!

Hili jambo muhimu sana kama uongozi mpya watalifanyia kazi,sijawahi kusikia kocha wa Tanzania ameenda kusoma nje.Charles Mkwasa,Sekilojo Chambua,Kenny Mwaisabula,Seleman Matola,Amri Said,Salvatory Edward,Mecky Mexime,Sylivester Mash,Keneth Mkapa,Ally Bushiri,Julio na wengine wengi hawa TFF ingewapeleka nje kwenda kuongeza ujuzi wangesaidia sana kukuza mpira wetu.Tunaongea kuanzisha academy na kuanzisha timu za watoto lakini hatuna makocha wa kufanya hiyo kazi
 
Bandugu bangu, kusomesha akina Julio nje sio solution ya kuwa na timu nzuri ya Taifa. Cha msingi ni kuwa na mfumo mzuri katika klabu kuanzia daraja la 4 hadi premier, sana sana ktk academy level, U 10, 12, 14, 15, 17 na 18. Njia moja kuu ni kwa TFF kutafuta sponsors au kuwabana waliopo wawekeze huko chini kwa watoto. Serikali iludishe umishumta na umiseta na hapo ukiongeza na mfumo wa miaka ile ya 80s ambapo tulikuwa tunapata mechi za kirafiki za kimataifa kila miezi kadhaa ndo soka litakua. Walete klabu kubwa au timu zilizo juu ktk ranking ya FIFA tufungwe hata 10-0 lakini over time exposure hiyo inasaidia.

Binafsi naamini sana Simba ndiyo kama imetufumbua macho na kutuamsha usingizini pale Babu alipoamua kutumia Yosso tuu. Haya mambo ya kusajili magarasa ya nje eti Burundi, Rwanda, Kenya au Congo yanatugharimu. Ona babu wa France alivyowakolesha vijana wa Matola, akawajenga kisaikolojia na wakapewa motisha uwanjani ni balaa. Tunahitaji u 10, na kuendelea na huko tutapika vipaji vingi na kuachana na hawa mabishoo wa vibwenzi kama Ngasa ect..

Soka kama michezo mingine inapikwa kuanzia chini, sio unakuta timu ya taifa players hawawezi hata kupiga danadana 10, sasa huyo kweli utamfundisha formation mbalimbali ?? Au tunategemea players mpaka wavute bangi kwanza ndo watapiga mashuti..

Tuna uwezo mkubwa sana na hazina ya players (Ona Mecco, Mbeya City n.k) lakini mipango mibovu na kuleta makocha kisiasa...

Tena kukomesha TFF wanaweza weka limit ya age, kama ilivyo ya foreign players kuwa kila timu ya premier iwe na say only/maximum 5 players over 26 yrs.

Mashindano ya U 17 na U 19 yakipata sponsors na wakawa na ligi kama ya premier tutacheza world cup !!

Hizo Academy zitafundishwa na kina nani?
Huwezi kuwa na timu za vijana wakati huna makocha,wachezaji wetu wanaanza kufundishwa na makocha profesional wakifika ligi kuu.
Nchi kama France,Spain,Holland,Germany wana makocha wengi sana na ndio wanapika vijana kwenye level ya chini.
Makocha wetu wanahitaji kupata knowledge mpya ya soka la sasa.
 
Back
Top Bottom