Kwa teuzi hii tutegemee mabadiliko katika baraza la Mawaziri, Je wakina nani watakuwa ingizo jipya na wakina nani watatolewa?

nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
745
1,000
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10/09/2021 amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika nafasi kumi za kuteuliwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Stergomena Lawrence Tax, alikuwa Katibu mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa jangwa la afrika (SADC), ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti mwaka huu.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Tuwe wavumilivu, mabadilko yanakuja hivi karibuni katika baraza la mawaziri.

62A2AA67-2BDD-499B-85FA-DC199BEC198A.jpeg
 
Juma1967

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
17,154
2,000
Dorothy apumzike tu..

Madelu akija Ulinzi na JKT atulie asilete nye nye nye..
Kuna kila Dalili Dorothy anaenda. Coz uteuzi wa Msomi wa Kimataifa means Lameki anaenda kucheza na jamaa zetu (PhD first class) ikiwa kwenye bahasha ya khaki.
NB: Vijana punguzeni kupoteza muda kwenye stori za Simba na Yanga mtaishia kulaumu watu tu mpaka kiama
 
mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
761

Kwa hiyo unashauri vijana wafanyaje?
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,382
2,000
Hongera kwa Dr. Tax kwa kupewa Heshima na Rais.
Mama stegomena Tax ni Jembe sasa ni wakati muafaka likatumika hapa nyumbani.
Atafaa sana kwenye wizara ya Katiba na Sheria.
ana faaa popote pale maana ni mama aliye iva kila idara.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,824
2,000
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10/09/2021 amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika nafasi kumi za kuteuliwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Stergomena Lawrence Tax, alikuwa Katibu mtendaji wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa jangwa la afrika (SADC), ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti mwaka huu.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Tuwe wavumilivu, mabadilko yanakuja hivi karibuni katika baraza la mawaziri.

View attachment 1931809
Huyu apewe Ulinzi,mama Gwajima atumbuliwe,Afya atafutwe Profesa mzuri kama alivyokuwa Prof Mwaikusa,Kuna yule Director wa Jakaya Kikwete Cancer institute,Prof Janabi,apewe Afya.
Mchemba,apumzishwe,Gwaji girl apumzishwe,
 
Juma1967

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
17,154
2,000
Huyu apewe Ulinzi,mama Gwajima atumbuliwe,Afya atafutwe Profesa mzuri kama alivyokuwa Prof Mwaikusa,Kuna yule Director wa Jakaya Kikwete Cancer institute,Prof Janabi,apewe Afya.
Mchemba,apumzishwe,Gwaji girl apumzishwe,
Prof Janabi Si Mbunge na nafasi za uteuzi Kama zishajaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom