Kwa tathimini niliyoifanya katika majiji ya Dar es Salaam,Mwanza na Arusha mwitikio wa wananchi kuacha kutumia rambo ni mkubwa

tusipotoshane

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
730
693
Kwa tathimini niliyoifanya katika majiji ya Dar es Salaam,Mwanza na Arusha mwitikio wa wananchi kuacha kutumia rambo ni mkubwa sana.Kwa hii kampeni,Serikali imefanikiwa na itafanikiwa zaidi.

Kinachotakiwa elimu ya mazingira iwafikie wananchi maeneo yote ya nchi sio walioko mijini tu,hata wa vijijini.

Wana Jf,hebu tupeni tathimini yetu katika maeneo mliyopo.

Hongera Serikali,mifuko ya Rambo lilikuwa janga la uharibifu wa mazingira.

Baada ya kampeni hii kufanikiwa,naomba Serikali yetu kufanya yafuatayo;

1. KUPIGA MARUFUKU MAWIGI KWANI NA YENYEWE NI JANGA LA MAZINGIRA.

2. HAYAOZI KABISA NA KUATHIRI VIUMBE HAI WA ARDHINI.

3. YANATOA HARUFU MBAYA YANAPOVALIWA NA KUATHIRI WENGINE.

4. WAVAAJI MUDA MWINGI WANAJIKUNA KUNA KWANI YANATUNZA UCHAFU.

5. YANASABABISHA UMBA VICHWANI.

6. GHARAMA KUBWA HUTUMIKA NA KUATHIRI UCHUMI WA FAMILIA NA MIZOZO KUTOKEA.

7. RASILIMALI MUDA HUTUMIKA VIBAYA WAKATI WA KUWEKA NA KUYAFUMUA.

8. YANABADILI SURA ZA DADA/MAMA ZETU KUTOKUWA ASILIA NA WANAPOYAVUA HUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI KWA WAPENZI KUTALIKIANA,HASA "ME"WENGI HUDAI WALIKOSEA KUCHAGUA.

9. YANAADHIRI UFANYAJI KAZI KWA UFANISI KWA MVAAJI KWANI MENGINE YANAPOVALIWA YANAKUWA NA UZITO ZAIDI YA KILO 2.

10. YANASABABISHA KINYAA KWA WANAUTOA HUDUMA ZA CHAKULA KWA SABABU MUDA MWINGI MVAAJI HUJIKUNA NA KUSABABISHA WATEJA KUTOTAKA HUDUMA NA KUMWATHIRI ALIYEWEKEZA.

11. HUSABABISHA KANSA YA UBONGO/NGOZI KWA MATUMIZI YA MADAWA YANAYOTUMIWA NA WAVAA MAWIGI.

12. YANALETA USUMBUFU KWA WATU WENGINE HASA USAFIRI WA UMMA KWA SABABU MAWIGI MENGINE YAMACHUKUA NAFASI KUBWA MITHILI YA MBUNI.

13. MAWIGI YANAONDOA UTU WA DADA/MAMA ZETU KUTUMIA NYWELE ZA WATU WA NJE AIDHA WAFU AU HAI KWANI SISI WENGINE TUNAWAPENDA ZAIDI WABAPOKUWA HAWAJAVAA HIYO MIAVULI BANDIA.

Nawasilisha Wakuu,karibuni mtoe mawazo kuisaidia Serikali yetu katika kupambana ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

SERIKALI/NEMC HONGERENI SANA.
 
Hili ni katazo la mifuko ya plastiki au mifuko meusi?
Mifuko ya plastiki ya rangi zote unazozijua wewe humu duniani,iwe ni blue,nyeusi,nyeupe au njano na zingine.

Pia katazo la MAWIGI ya rangi zote unazozijua tuhamasishe lifanyiwe kazi.

Mfano unaweza ukawa umelala na patina kalivaa,itakufanya uharakishe kuondoka/kumwauga kwa SABABU ya harufu isiyovumilika na ya ajabu ajabu,Madhara yatakayojitokeza ni kupoteza rasilimali muda na fedha wakati una piga song/tongozo.
 
Zoezi limefanikiwa, maana leo nimeenda sokoni naona watu ni full displine
Mifuko mipya ina gharama kwa kweli anyways nadhani tutazoea
IMG_20190601_155843.jpeg
 
Kuna hizo wig na rasta za buku wazosukia penseli nazo pia ni adui wa mazingira.Laiti kuku au njiwa wangepewa uwezo wa kuongea wangetoa ushahidi jinsi rasta za kusukia pensili zinavyotesa wakikutana njiani huwa zinawafungafunga miguu.
 
14. Yanatufanya wanaume tuibiwe, unadhani mwanamke ni mzuri kama kim kardashian akilivua ana kichwa kikubwa kama cha vincent Company wa man city
Mkuu kweli watu wameibiwa sana.Mvizie usiku akiwa amelala ufunue/utoe hilo wigi kama hajalishonea na nyuzi za katani stimu inaweza kukata.Utaona maajabu ya nywele utadhani mavuzi ya ngiri.

Halafu wakiwa wanatembea muda wote mikono kichwani wanazirudisha rudisha nyuma kama wafanyavyo watasha wa ukweli,kumbe anayefanya hivyo ametokea mitaa ya Kwa Mtogole/Manzese .

KIKUBWA MAWIGI HAYO NI ADUI WA MAZINGIRA KAMA MIFUKO YA RAMBO/ PLASTIKI ILIYOKATAZWA.
 
Kuna hizo wig na rasta za buku wazosukia penseli nazo pia ni adui wa mazingira.Laiti kuku au njiwa wangepewa uwezo wa kuongea wangetoa ushahidi jinsi rasta za kusukia pensili zinavyotesa wakikutana njiani huwa zinawafungafunga miguu.
Zipi tena hizo? Za penseli?Zikoje hizo?Wadada watuonee huruma sio kwa u- artifial huo.
 
Mkuu kweli watu wameibiwa sana.Mvizie usiku akiwa amelala ufunue/utoe hilo wigi kama hajalishonea na nyuzi za katani stimu inaweza kukata.Utaona maajabu ya nywele utadhani mavuzi ya ngiri.

Halafu wakiwa wanatembea muda wote mikono kichwani wanazirudisha rudisha nyuma kama wafanyavyo watasha wa ukweli,kumbe anayefanya hivyo ametokea mitaa ya Kwa Mtogole/Manzese .

KIKUBWA MAWIGI HAYO NI ADUI WA MAZINGIRA KAMA MIFUKO YA RAMBO/ PLASTIKI ILIYOKATAZWA.
mav** ya ngiri yanakaa sehemu gani mkuu!
 
Zoezi limefanikiwa, maana leo nimeenda sokoni naona watu ni full displine
Mifuko mipya ina gharama kwa kweli anyways nadhani tutazoeaView attachment 1114342
Wamejipangaje na izi Aluminum Foil nadhani zile na zenyewe ndio balaaa linalokuja baada ya mifuko. Labda Waweke makampuni ya kukusanya izi chupa na aluminum foil. Lasivyo balaa
 
Wamefanikiwa ila wenye mabasi waweke visado vyakutapikia kwenye mabasi maana Leo Kuna madogo wametapika kwenye basi hadi wakachafua begi langu nililoweka chini ya siti
 
Back
Top Bottom