Kwa Tanzania sensa ni upotevu wa fedha.........labda kama kuna mengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Tanzania sensa ni upotevu wa fedha.........labda kama kuna mengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Nov 26, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  The National Bureau of Statistics (NBS) on Thursday received £4.5 million funding from the British government through its Department for International Development (DFID) as additional support for the 2012 population and housing census.

  British High Commissioner to Tanzania Diane Corner said in Dar es Salaam that providing the additional support would ensure that the next 2012 census provided accurate and reliable population data, which were vital in delivering an effective programme to reduce poverty.

  "The information collected in the census is necessary for informed policymaking, efficient planning, delivery of public services and to inform potential investors," said Corner.


  Information collected from households in the country, according to her, will ensure that the government, development partners and the private sector resources are effectively targeted, which will give strong evidence base for examining inequalities between different regions and districts in
  Tanzaniaas to why some are poorer than others.

  This will be the fifth census after independence of Tanganyika in 1961, the last four were conducted in 1967, 1978, 1988 and 2002 aimed at contributing to the improvement of quality life of citizens through the provision of up to date and reliable data for policy formulation, development planning and service delivery.

  KWANINI SENSA SI MUHIMU

  1
  )Tulielezwa kuwa Tanzania ipo kwenye mchakato wa vitambulisho vya uraia, ni mategemeo yangu kuwa katika hivyo vitambulisho kutakuwa na Namba ya utambulisho ya Raia,yaani Citizen Identification Number tena kwa mtiririko maalum pamoja na taarifa muhimu. Kama ni hivyo basi Idadi ya kila mtu itafahamika na shughuli yake itafahamika, makazi yake yatafahamika. Hii ni njia reliable kuliko Sensa. Kama hiyo namba ya Raia itatumika katika kila huduma zitolewazo na serikali kuanzia hospitali, mashuleni, Bank etc, ni matumaini yangu kuwa kila raia itamlazimu kuwa na hiyo namba ili aweze kupata huduma yoyote nchi. Utaratibu huu ndio wenzetu walioendelea wanautumia. Sensa tuache wafanyiwe wanyamapori.

  2)
  Tanzania ina Idara ya uzazi na vifo (RITA) ambayo kazi yake kubwa ni kutunza takwimu za wanaozaliwa na wanaozaliwa, Idara hii ni bora ikaongezewa uwezo na hayo mabilioni yaliyotengwa kwa ajili ya Sensa ili wafanye kazi kisayansi zaidi. Uhamiaji pia waongezewe uwezo ili wachukue takwimu zote za wageni, na kuziingiza kwenye Database na kuwapa wageni Namba ya utambulisho wawapo nchini.

  3) Serikali haiwezi kutufanya tuamini kuwa itakusanya Takwimu makini kwa watu zaidi ya milioni 40 kupitia (NBS)Sensa wakati hadi leo Serikali kupitia Tume ya uchaguzi imeshindwa kutoa takwimu za uchaguzi kwa watu wachache tu waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Hii maana yake information itakayopatikana kwa namna yoyote ile itakuwa Unreliable.

  4)Sababu zinazotolewa na Serikali kuwa zitasaidia kufanya maamuzi sahihi si kweli, kwani Sensa nne zishafanywa na hakuna maamuzi yalofanywa kwa kuzingatia hizo Takwimu za Sensa. Kama madawati hayatoshi, Mikopo kwa wanafunzi haitoshi, Madawa Hakuna, Mahospitali hayatoshi, Miundombinu karibia yote haijareflect idadi yetu. Nadhan serikali ingejikita zaidi kutafuta vyanzo vya mapato badala ya kuchezea mapato kwa miradi isiyo na tija.

  5) Serikali ijiulize
  , Priority kwa watanzania kwa sasa ni kujulikana idadi tena kwa njia ya Sensa??Na Idadi ikishajulikana itasaidia nini???Je ni bora hiyo Fedha 20 Billions of money ikatumika kutuhesabu au kununulia wananchi wanaoteseka kwa maradhi madawa, kuboresha miundombinu, mahospitali n.k???

  Hitimisho, Serikali itumie Vitambulisho vya Uraia tunavyotarajia kuvipata na tena vinavyogharimu pesa nyingi, Rita pamoja na Uhamiaji katika kupata idadi ya wananchi wake, wageni pamoja na basic information za raia/wageni wake. Utaratibu huu ndio unaotumika nchi zilizoendelea. Wenzetu utaratibu wa Sensa walishaondokana nao maana kila siku watu wanakufa, wanazaliwa, wanaingia nchini kutoka nje ya nchi na kuondoka nchin kwenda nje ya nchi, hivyo tukiwa na Database ambayo ipo updated kila siku ndipo tutaweza sema tuna accurate na precise information. Otherwise ni uchezeaji wa hela maana takwimu zitakazokusanya hazitachelewa kupoteza sifa. Kwa sababu tajwa hapo juu, na imani lengo la serikali sio kujua Sensa, yaani kujua idadi, bali ni kuchezea Fedha na kuzifanyia ufisadi as usual.


   
Loading...