Kwa Tanzania Nani wa Kulaumiwa kati ya hawa, WILAYA Isipoendelea?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Wilaya?
DAS?
Mkurugenzi wa Halmashauri?
Wabunge wanaotoka wilaya hiyo?
Wananchi wa Wilaya hiyo?

Majibu angalau yaendane na majukumu yao...
 
Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Wilaya?
DAS?
Mkurugenzi wa Halmashauri?
Wabunge wanaotoka wilaya hiyo?
Wananchi wa Wilaya hiyo?

Majibu angalau yaendane na majukumu yao...
Kwa mtazamo wangu naona ni mbunge sababu wanahusika na mipango ya maendeleo na upangaji bajeti hao wengine hao hawajaribiwi
 
Hakuna wa kulaumiwa kuhusu maendeleo, hao wote wanatakiwa kufanya kazi kama timu moja kwa sababu kila mmoja ana majukumu na wajibu wake kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu.
 
Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Wilaya?
DAS?
Mkurugenzi wa Halmashauri?
Wabunge wanaotoka wilaya hiyo?
Wananchi wa Wilaya hiyo?

Majibu angalau yaendane na majukumu yao...
Katiba siyo nzuri , inawafanya wateule wa Rais na ofisi ya waziri mkuu kuwa na nguvu na sauti dhidi wananchi (wabunge na madiwani). Na daima wateule wanamtumikia aliyewateua na si wananchi (mifano ipo)

Tatizo katiba ya kikoloni na ipo kuimarisha utawala si wananchi.
 
mkuu nimekuelewa kwa kiwango cha kutosha. Tatizo linakuja pale pande mbili zinazopingana kutakiwa wafanye kitu kimoja kinachowaunganisha huku wao wakibaki na misimamo na tofauti zao. Hapo lazima maendeleo yadumae.
 
Wananchi ndiyo wa kwanza kulaumiwa kwa kuwachagua wabunge na kuanza kuwalea na kuwaachia bila kuwafuatilia utendaji wao.

Wabunge wanapaswa kuwana ofisi katika majimbo yao na hii ofisi au Surgery ni kwa ajili ya kuwasiliana na wananchi wa jimbo husika bila shuruti na bila kujali mbunge anatoka chama gani.

Hivyo wananchi ndiyo namba moja kwa kustahiki lawama kwani wasioona maendeleo yoyote wanamwondoa mbunge na anachaguliwa mwingine.

Anaefuatia kwa kulaumiwa ni mbunge mwenyewe ambae hawajibiki jimboni kwake, hatembelei wananchi wake na hana mipango yoyote ile ya maendeleo jimbon kwake tokea anachaguliwa hadi anamaliza muda wake wa ubunge.
 
Wakulaumiwa ni Rais. Wote hao hawana mamlaka ya kusema wilayani kwetu tumepata pesa kiasi fulani. Tunataka kiasi hiki tujenge mtambo. Huu, barabara hii au mradi huu wa umwagiliaji. Wote wanategemea pesa za maendeleo kwa fadhili za Rais na utashi wa mawaziri. Ndiyo maana sehemu ikipata waziri au Rais huendelea fasta. Tunahitaji decentralisation ya kufa mtu.
 
mkuu nimekuelewa kwa kiwango cha kutosha. Tatizo linakuja pale pande mbili zinazopingana kutakiwa wafanye kitu kimoja kinachowaunganisha huku wao wakibaki na misimamo na tofauti zao. Hapo lazima maendeleo yadumae.
Hilo ni tatizo kubwa najua na hasa ile mikoa au wilaya ambazo Kuna wabunge wa upinzani na Hata madiwani wanapokuwa wa upinzani ndipo unapoona huo msuguano wa kiuongozi
 
Mkuu wa Mkoa?
Mkuu wa Wilaya?
DAS?
Mkurugenzi wa Halmashauri?
Wabunge wanaotoka wilaya hiyo?
Wananchi wa Wilaya hiyo?

Majibu angalau yaendane na majukumu yao...
Hapana wa kulaumiwa hapo
Labda niulize hivi ni utaratibu gani hutumika kupeleka maendeleo kwenye baadhi ya maeneo na mengine ukakuta yanaachwa
Mfano kuna baadhi ya wilaya nchi hii yaani utadhani ni Kata
Hakuna lami wala umeme na wilaya zingine utadhani ni mkoa jinsi palivyochangamka
Naomba kueleweshwa
 
Mkuu wa shughuli za maendeleo ni Mkurugenzi wa wilaya. Huyu ndiye mwenye bajeti yote. Hao vilaza wengine ni wanasiasa tu.
Mbunge sio kazi yake kuhangaika na mambo hayo zaidi ni mshauri tu na muwakilishi wa wananchi katika kufikisha malalamiko yao kisiasa zaidi. Wakurugenzi wetu nao wameingia katika siasa hasa pale wanapokuwa wasimamizi wa chaguzi na kulazimishwa kutanga siasa nani awe mshindi, so wanatoka katika kazi ya kitaalamu na kuingilia kazi za siasa. Sehemu kubwa mkurugenzi ndio mwenye plan ya maendeleo ya Jimbo/wilaya/mkoa. DED akiwa kilaza mjue hakuna kitu.

Mfano kwetu Iramba nafikiri kuna haja ya kuwa na mkurugenzi mwingine mbunifu na anayejali maendeleo ya wananchi ili aibue miradi ya maendeleo na hivyo kusaidia kukuza pato la halmashauri kwa kuongeza vyanzo vya mapato. Miaka inapita sioni project zozote zinazosimamiwa na DED Iramba, yupo tu kupokea mshahara pale.
 
Unachokisema nakielewa, kwanza Kati ya wote huyu jamaa ndio huwa msomi. Kuna mmoja alistaafu wilaya flani aliwahi kunishushia mambo ya uchumi hadi nikabaki mdomo wazi. Huyo mzee alikuwa na Degree kama sio masters ya uchumi. Hawa jamaa ni wa muhimu sana kuliko wanasiasa ila huwa sio maarufu sana
 
Back
Top Bottom