Rais Magufuli kataka mwekezaji Mtwara arudishiwe hela alizonunulia Transfoma. Nami TANESCO wanirudishie gharama zangu

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,815
20,660
Katika hali ya kufurahisha na Rais wetu kuendelea kuwatendea wananchi wake haki, Mh. Dr. John Joseph Magufuli amelitaka shirika la Umeme nchini (TANESCO) kumlipa Tsh. 27 Million mwekezaji wa kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Mtwara vijijini Hata baada ya kutompa ushirikiano wa kumfikishia umeme kwenye kiwanda hicho.

TANESCO ilimtaka mteja huyo kujinunulia Transformer kitendo ambacho Mh. Rais Magufuli alikipinga kwa kusema "haiwezekani anunue transformer alafu muje kumlipisha bili tena" .

Mazingira ya kujinunulia Transformer yamenikumba hata mimi. Baada ya TANESCO kufanya survey ya eneo langu na kunishauri ninunue Transformer.Nilifanya hivyo, lakini katika hali ya kushangaza nimeendelea kulipà bili za umeme kama kawaida,pamoja na kwamba nimejinunulia Transformer mwenyewe.

Kwa tamko hili la Rais kwamba TANESCO wanapaswa kumrudishia mwekezaji wa kiwanda cha kubangulia Korosha cha Mtwara hela alizonunulia Transformer, nadhani ni wakati muafaka sasa na haki yangu TANESCO kunirudishia pesa niliyonunulia Transformer. Risiti zote ninazo.

Kama TANESCO watataka kuwasiliana na mimi namba zangu ni 0735442559/0787442559 au 0715090976.

Wanaweza pia kuwasiliana na mimi kwa e-mail:mwanawamungu116@gmail.com
 
Hizo case ni nyingi sana kwa Tz, viwanda/watu wamenunua sana tranforma, sidhani kama ataweza kusema wote hao warudishie pesa!!

Mzee wa kick Alishapata ile kick ya mtwara basi!! Kwanini asingetangaza kuwa watu wote walionunua transfoma warejesheshwe pesa zao moja kwa moja au kwa utaratibu maalum utakaowekwa na Tanesco?
 
Hizo case ni nyingi sana kwa Tz, viwanda/watu wamenunua sana tranforma, sidhani kama ataweza kusema wote hao warudishie pesa!! Mzee wa kick Alishapata ile kick ya mtwara basi!! Kwanini asingetangaza kuwa watu wote walionunua transfoma warejesheshwe pesa zao moja kwa moja au kwa utaratibu maalum utakaowekwa na tanesco?
Labda hana taarifa kwamba watu huwa wanajinunuliaga transformer.

Ngoja tusubiri, nimechomekea tu.Ila sheria walizojitungia TANESCO ni kandamizi mno.Mtu anunue transformer, watu waunganishiwe umeme kwenye transformer yake,halafu alipe bili za umeme bila hata punguzo,hapana jamani even common sense says no.
 
Back
Top Bottom