Kwa tabia hizi LAZIMA UOLEWE

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,801
6,231
Kana miaka 20, baba yake mzazi ni mpare na mama mu-iraq. Ni kazuri kupindukia coz sinaga historia ya ku-date mabinti wabaya. Bado kako chuoni.

Oneni tabia zake... hakajawahi HATA SIKU MOJA kuniomba pesa, nikajishtukia ikabidi nimuulize kama ana shida yoyote, akanijibu kwamba kwa sasa wenye wajibu wa kumtunza na kumsomesha ni wazazi wake.

Nina gari, ila hajawahi kuliulizia siku asiponiona nalo, ameshaniaminisha kwamba ananipenda kama nilivyo, tofauti na madem wengine wapenda maujiko kwamba mabwana zao wana magari!

Siku nikipata dharura nikawa sina airtime kwenye simu ananitumia!

Msimamo ndio usiseme, kuna jamaa alimtaka mtoto akakataa, jamaa akamtishia, mtoto akaenda kumshtaki polisi.

Binafsi nimewahi kumnunulia vitu vidogovidogo tu tena kwa kumbembeleza ikibidi kumlazimisha!

Asipobadilika wallahi vile NAOA!
 
Nipe namba yake nimuunganishe kwenye Namba ya maajabu!!
Marriage is a destiny usipokaza msuli utaambulia manyoya pamoja na dalili zoote za uke wema!!
 
mi huwa nahakiki namba za simu, muulize hata DEMBA ....kwa hyo kitu ukilala tu......
 
Last edited by a moderator:
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom