Kwa taarifa za kuaminika Ukraine anavamiwa sio muda na Urusi

Kiufupi ulichokiandika hata hakieleweki.

Yaani unajikanganya, Mara useme Russia havamii lakini Tena unasema Russia anaenda kuikalia Ukraine. Sasa Bila kuvamia ataikaliaje? Kwanza Ushawishi wa Russia kwa Raia wengi wa Ukraine Ni Mdogo Sana,wanamuona Kama Mkoloni,ndio maana wanataka kujiunga NATO ili kujihakikishia Usalama. Ndio maana hata Urus anaogopa Ukraine isijiunge na NATO make NATO itasomba mamia ya Nuclear Missiles pale KIEV ikawa shida kwa Urus.
Russia ni mkoloni wa hiyo nchi siku zote,huelewi nini sasa
 
Maadui wakubwa wa demokrasia ni china na urusi. Biden asogeze mitambo ya nuklia jirani kulinda demokrasia ukraine
 
Okay, kwahiyo kuwa cheap kwa silaha za mrusi maana yake sio bora? Au ubora wake hauwezi kuzidi mifumo ya ulinzi ya Marekani?

Kuhusu Uturuki naona unahamisha magoli tu, nimeitaja kwenye vikwazo kwa ulinganisho na India, na hata hii hoja uliyoiibua pia hauijui vizuri kwa sababu Uturuki aliwekewa vikwazo vya kununua silaha za Marekani baada ya kununua silaha toka Urusi. Uturuki ni Nato member kwahiyo kununua silaha toka Urusi ni kuvunja masharti ya umoja huo.
Jibu ni ndio silah za marekan ni bora mfano S300 na S400 zipo istalled syria na bado wana shamburiwa.
 
Kwa kweli Putin yuko sahihi kwenye hili. Move za NATO zinatishia uhai wa Russia na hakuna taifa linaloweza kubali. Nadhani kinachomkwamisha Russia kwa sasa ni Nord Stream 2 project.
How yaan nchi huru kuwa na ushirika nchi flan kosa?nimeona wachambuzi wanasema nchi zilizo jiunga na Ulaya zina kuwa kwa kasi kiuchumi ambapo ni tishio au wivu kwa putin kuona sio muda Warusi wata anza kuhiji sela zake za kiuchumi.
 
Nord Stream 2 sipati uhakika kama itafanya kazi au lah. Hao Marekani wanaolazimisha NATO iwe Ukraine wao wenyewe walipambana vikali USSR ilipokuwa Cuba na wakataka kumpindua Fidel Castro. Yanayofanyika leo na Russia ni yaleyale ya miaka ya 1960s
Yaan US ana force Ukrain kingia NATO?
 
How yaan nchi huru kuwa na ushirika nchi flan kosa?nimeona wachambuzi wanasema nchi zilizo jiunga na Ulaya zina kuwa kwa kasi kiuchumi ambapo ni tishio au wivu kwa putin kuona sio muda Warusi wata anza kuhiji sela zake za kiuchumi.
Historia huyafunza mataifa. Kama ambavyo Mmarekani hawezi kukubali Urusi awe jirani kwake, ndivyo ambavyo yeye Urusi hawezi kukubali Mmarekani awe jirani kwake. It's an existential threat, ambayo it's understandable kwa taifa linalopitia hatua hiyo kuchukua hatua kadhaa wa kadhaa za kujihami.
 
Ukraine inataka iingie ila Marekani anaitaka vilevile ili iwe buffer. Pale si anaweka silaha mdomoni kabisa mwa Urusi. Nchi za Ulaya ndio zinasitasita
Zinasita kwasababu wanajua ukitokea msala wao ndo wapo karibu ila Mmarekani atakua zake mbali huko anapiga domo tu
 
Jibu ni ndio silah za marekan ni bora mfano S300 na S400 zipo istalled syria na bado wana shamburiwa.
Mashambulizi yanayoendelea Syria hayana uhusiano kabisa na ubora wa s.300 na 400.
Mashambulizi yanatokea kwa sababu zifuatazo;

1) kuna baadhi ya maeneo bado yanakaliwa na Marekani na waasi. Russia hana nguvu kwenye hayo maeneo.

2) Mahusiano baina ya Israel na Russia. Urusi inafanya biashara kubwa na Israel kwahiyo huenda kukawana makubaliano ya gizani kuhusu Syria. Ukichunguza utagundua Mashambulizi yanayofanywa na Israel nchini Syria yanawalenga Hezbollah na makundi mengine rafiki kwa Iran ila sio majeshi ya Syria wala Russia. Na hapa kwa kiwango kikubwa inaonesha unafiki wa Urusi kwa kuwa wakiwa kwenye operation ya pamoja(Russia, Syria na Iran) huwezi kuona mashambulizi toka kwa Israel ila Hezbollah au kundi lolote rafiki kwa Iran likiwa lenyewe wanashambuliwa.

Umeizungumzia Israel pekee ila hata Uturuki na Marekani bado wanaendelea kushambulia Syria ila hakuna anaebeza uwezo wa hiyo mitambo.

Pia Mara nyingi Israel inatumia anga la Lebanon kushambulia Syria. Kwanini wanafanya hivi, sijui.
 
Jibu ni ndio silah za marekan ni bora mfano S300 na S400 zipo istalled syria na bado wana shamburiwa.
Screenshot_20220120-194628_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20220120-194655_Samsung Internet.jpg
 
Putin kwisha na ujamaa unaelekea kuzikwa kwann Ukraine anaingia umoja wa ulaya hivyo nipenyezo au langu la babylon kusambaratisha udikiteta wa mwamba Putin ...tusishangae 10 years later democrasia ,Law and reasonings zinatamalaki urusi ,naona urusi mpya
Nani kakuambia Urusi hamna demokrasia. Unataka kuilinganisha Urusi na Tanzania?
 
Urusi inaendelea kusogeza silaha za kivita mpakani na Ukraine. Taarifa ya tarehe 18 kutoka Washingston Post
View attachment 2090356

By Nature Putin ni mtu ambae akikkikusudia kitu huwa haogopi au kurudishwa nyuma

Canada wamepeleka special forces Ukraine kuyakoroga mambo na akilini mwangu kuna kitu nakihisi kibaya kinaisubiria kuikumba dunia
 
Inategemea hicho kitu anachokikusudia kina maslahi kiasi gani. After all, yeye ni binadamu (by nature), pia ni mwanasiasa kama wengine.

Kinachoendelea ni siasa za hapa na pale za kila upande ku-promote madai yake. Urusi inatafuta namna nzuri ama nafuu kwake ya kulinda usalama wake. Kutaka kuivamia Ukraine kwa sasa si njia nzuri kwake hata kidogo.

Hata hivyo, mpaka sasa NATO imekataa madai kadhaa ya Urusi likiwemo la kuitaka NATO kuondoa majeshi yake Bulgaria na Romania.

Meanwhile, shehena ya kwanza ya misaada ya kijeshi zikiwemo silaha za kivita, imepelekwa nchini Ukraine na serikali ya Marekani. Tutegemee silaha zaidi kuingizwa nchini Ukraine kutokea NATO member states.

Kutokana na kwamba Ukraine si mwanachama wa NATO, ni changamoto kwa policies muhimu za NATO kuwa applied kwake. Nafikiri, NATO itatumia zaidi njia hii ya kuisogezea silaha Ukraine mpaka hapo baadaye.
 
Putin huyu huyu aliwapelekea jeshi na kipigo juu Georgia miaka ile ile kwa msisitizo ni Rais alikuwa Putin huyu huyu na tunakumbuka Bush pamoja na mikwara na kupenda vita alipiga mikwara mingi na yakaongelewa mengi ila mwisho wa siku Georgia walipelekewa jeshi la Russia na kichapo walipigwa vizuri sana
 
Mazingira ya intervention ama uvamizi wa Georgia ni tofauti sana na ya sasa.

Ili uvamizi wa kijeshi dhidi ya nchi huru (sovereign state) uweze kuwa na mafanikio kwa mvamizi, yapo masuala kadhaa muhimu ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwanza kabla ya uvamizi. Masuala hayo yasipozingatiwa, huo uvamizi hauna tofauti na kamari (gambling).

Jambo la kwanza ni kisababishi ama kichochezi, kwa kiingereza tunaita "trigger". Ni lazima kuwepo na jambo ama kitu kitakachochochea kwa haraka ili uvamizi kufanyika. Mfano: kama ulifuatilia kisa cha uvamizi wa Georgia, mashambulizi ya Georgia katika maeneo ya Ossetia Kusini yanatajwa kama "trigger" katika vita hiyo.

Kitu ambacho kilipelekea uungwaji mkono mkubwa wa wakaazi wa maeneo hayo juu ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Georgia. Na hili ndilo jambo la pili ambalo linapaswa kuzingatiwa: uungwaji mkono wa wavamiwa (local support).

Kama local support ya wanaovamiwa ni ndogo sana kuhusu uvamizi, matatizo yatakayotokana na uvamizi huo yatakuwa makubwa sana hapo baadaye na yanaweza kusababisha machafuko ama vita vya muda mrefu sana kutegemeana na upinzani ama reaction ya waliovamiwa.

Ukiachana na hayo, kuna masuala mengine muhimu ya kitaalamu ama kiufundi. Kabla ya uvamizi, mahesabu ya muda mrefu yanahitajika ya kuweza kubaini access ama njia/mbinu za kufanikisha intervention ama uvamizi huo.

Ni lazima mvamizi awe na mpango mahususi wa utekelezaji wa uvamizi wake. Mfano mmoja: mvamizi anapaswa kupangilia maeneo ambayo majeshi yake yatapitia bila kuathiri masuala mengine kama 'local support'. Pia mvamizi lazima awe tayari amekwisha tarajia (anticipate) kiwango mahususi cha upinzani kitakachosababishwa na majeshi ya anayevamiwa.

Hapo katika suala la ku-anticipate kiwango cha upinzani kutoka katika majeshi ya anayevamiwa ni pagumu sana. Ni lazima mvamizi ajiandae kupokea kiwango fulani cha hasara kwa majeshi yake. Isitoshe, mvamizi anahitaji kugharamia uvamizi wake kifedha. Pamoja na hayo, jaribio la uvamizi linaweza kufeli kama mahesabu yasipofanyika vyema.

Sasa, katika masuala hayo kadhaa niliyoyasema, uwezekano wa Urusi kuivamia Ukraine kwa ujumla wake ni mdogo sana. Chukulia jambo moja rahisi kama 'local support'. Uungwaji mkono wa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine kwa sasa ni kiasi gani nchini Ukraine? Trigger je ni kitu kipi? Vipi kuhusu matarajio ya Urusi kuhusiana na uvamizi wake kama kweli ana mpango huo?

Urusi iliweza kufanikisha uvamizi wa Georgia sababu masuala haya yote muhimu yalizingatiwa na kutimizwa, kitu ambacho ni tofauti sana na suala hili la sasa la Ukraine. Kama nilivyosema hapo awali, kuivamia Ukraine kwa sasa haina tofauti na kamari (gambling).
 
Tayari Russia kashaivamia Ukraine kwa mujibu wa taarifa na kauli ya Putin aliyoitoa jana katika Video release

Kuna taarifa uvamizi unapitia pia nchi ya Byelorussia
 
Back
Top Bottom