Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Lissu hakujiandaa,laiti angesoma barua ikiwa bado sealed.
BBC ni chombo kikubwa sio Clouds,ajipange upya.
Anahitaji kupewa shule na wataalamu jinsi ya kufanya mahojiano na press za Western World especialy Britain,USA,Germany.
 
Kweli we Shoga Bwabwa kwelikweli.... Kama unaona Tanzania hakuna Uhuru nenda kwenye nchi zenu za Ushoga mtuachie Tanzania yetu sisi wanaume wa kweli, hapa Tanzania ndio tuko fit Tunapiga kazi kwa kwenda mbele na pesa inapatikana lakini nyie mnao hitaji kubustiwa endeleeni kulalamika.
Kwa mawazo yako sasa hivi Libya ilivyo ndio unaona ni demokrasia hiyo kweli akili ni mali, Libya wanajuta kumpoteza Gadafi wewe unaona ndio ushujaa.... Hivi kumbe nyie shida yenu tuwe na vita Tanzania, kwa hilo mmeishafeli... Bwabwa kweli wewe.
Crap and non-sense!
 
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
una faili lake la hosp. hadi kusema ana afya njema

wajuaje kama amepewa muda wa maangalizo ili kumjenga kisaikolojia
 
Watu wengi wameingalia interview ya Lisu wakiwa tayari Na mitazamo yao moyoni . Hii imepelekea kuja na mitazamo mbali mbali.

Wapo waliongalia hard talk ile kama kampeni ya Lisu kwa ajili ya kugombea Urais 2020 . Na hapo ndipo walipofanya makosa . kati ya sasa na 2020 ni mbali mno , Lolote laweza kutokea kwenye Siasa. Ukiangalia kwa mtazamo huo unaweza kuona kama Lisu akulifanyia mema Jukwaa hilo... la hasha,nia ya Lisu kwenye hardtalk hiyo haikuwa kujijenga kwa ajili ya Urais 2020.

Wapo pia waliongalia kwa jicho la kichama , maana ya kama ni CCM basi aponde lolote litakalojadiliwa , kwa mtazamo huo pia utapelekea kupata picha tofauti na utaona Lisu amekosea ?. Kwa nini akueleza na mazuri yakiofanywa na JPM?

Wapo waliotazama kwa mtazamo wa chama kama Chadema, Hawa wamesifia na hata wengine bado waliona Lisu akutumia vyema jukwaa.. kwamba alitakiwa kutaja mambo mengi zaidi ya hapo.

Wapo waliongalia hard talk ile kwa mtazamo wa kufuatilia mambo ya siasa bila kujali chama wala suala la Uchaguzi. Hawa wameiona nia ya Lisu ya kuutangazia umma kile ambacho labda Lisu anaamini Dunia haijui.

Wapo pia watu ambao si watanzania bali ni wafuatiliaji wa karibu wa Siasa za Africa, hasa Misingi ya Demokrasia . Hawa wamepata kusikia toka kwa Mtanzania , tuhuma ambazo zinahitaji uchunguzi...

Yapo Mataifa na Mashirika mbalimbali ambayo nayo yametazama hardtalk kwa ajili ya kupata habari wanazozitafuta au kuthibitisha kile wanachokifahamu...
Je Ni Upi hasa Mtazamo wangu.
  1. Lisu pamoja na kuwa ni mtu anayetegemea kuja kugombea Urais kama akipendekezwa na chama chake alitaka kutumia fursa hii kuionyesha Dunia kuwa Tanzania ile ya amani na utulivu haipo tena. Sijui kama ni kweli au la yeye anajua?
  2. Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa kwa sasa Tanzania mtu anaweza kupigwa Risasi mchana kweupe na bado FAIL la kesi yake likafungwa ndani ya mwaka bila jitahada zozote.Sijui kama ni kweli au la, Ili hili lijulikane serikali ina wajibu wa kufanya uchunguzi na kukanusha.
  3. Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa mbunge aliyetakwa kuuwawa na watu wasiojulikana anaweza kunyimwa matibabu hata kama ni stahili yake. Sijui kama hili ni la kweli au la, Lisu anajua na serikali wanatakiwa kutoa majibu
  4. Lisu alitaka kueleza Dunia kuwa yapo mambo yanayohitaji uchunguzi wa kina kuhusu haki za binadamu yanayoendelea Tanzania. Sijui kama ni kweli au la , Lisu yeye anajua na serikali itawajibika kukanusha
  5. Lisu alitaka kueleza Dunia kuwa kuna kubanwa kwa Demokrasia kwenye Nchi ya Tanzania. Sijui hili kama ni la kweli?, Lisu anajua na Serikali itawajibika kukanusha
  6. Lisu alitaka kueleza dunia kuwa kuna mambo yanayofanywa kinyume na Katiba. Hili nalo serikali iatwajibika kukanusha
  7. Lisu alitaka kuonyesha Dunia kuwa kuna manunuzi yanafanywa nje ya kupitishwa na Bunge. Hili nalo serikali itawajibika kukanusha
  8. Lisu alitaka kuonyesha dunia kuwa kuna haki ambazo zipo kwenye Katiba kuhusu Uhuru wa mambo ya ndani ya mtu ambayo serikali inabidi kuyaheshimu. Hili nalo serikali inatakiwa kukanusha
Tatizo kubwa lililokuwepo kwenye kipindi kile ni Bw Stephen na Lisu kutaka kujadili mambo mengi wakati muda ulikuwa kidogo. Hii ilipelekea kwa Lisu kutokupewa muda wa kutosha wa kujieleza na Stephen kumkatiza na kuuliza maswali mengine ili kufikia lengo la maswali aliyotaka kumuuliza .

Sijui wewe uliangalia ukiwa na mtazamo Upi ? tujadili
 
Yapo mengi, Pole Pole yeye alichukulia Stiv ni mwana CCM mwenzao. Ndicho alichoelewa yeye kwenye ile interview. Bashite yeye hakuelewa chochote zile vocabulary hazipo kwenye dikshinari yake ya uvuvi wa samaki! Jiwe ndio kwanza yuko na dikshinari anajaribu kuirudia ile interview Kama atapata kuelewa chochote!
 
Lissu ametuharibia image ya serikali yetu tukufu! Hii haikubaliki.

Atatuletea hasara, misaada ikikatwa tutakaoumia ni sisi wananchi wala sio Magufuli na class yake.

Ajaribu kuipenda nchi yake japo kidogo mwambieni arudi nyumbani au atafte asylum huko huko EU atulie wajameni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichongundua tangu ahojiwe lissu ni kuwa lissu ni hazina ya taifa, jamaa ni kichwa ile mbaya anaogea point sana na hana chembe ya unafiki ila anataka haki kwa watu wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimegundua Lissu hana lolote bali ana inflammatory allegations kama alivyosema mtangazaji wa BBC Hardtalk Stephen na kwamba Stephen anayajua mengi mazuri yanayofanywa na Mh. Rais kuliko Lissu!!
 
Lissu ametuharibia image ya serikali yetu tukufu! Hii haikubaliki.

Atatuletea hasara, misaada ikikatwa tutakaoumia ni sisi wananchi wala sio Magufuli na class yake.

Ajaribu kuipenda nchi yake japo kidogo mwambieni arudi nyumbani au atafte asylum huko huko EU atulie wajameni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Japan wametoa tena msaada wa kujenga flyover pale makutano ya gerezani Dar kwa taarifa yako mkuu!
 
Nilichoona mimi Lisu ni akili kubwa sana, alijibu maswali kwa akili sana hasa swali la ushoga.

Alilijibu hilo swali kwa akili sana kuliko serikali walivyojibu na kumkana Makonda kupitia kwa Mahiga ya kuwa aliyoyasema makonda sio msimamo wa serikali.

Kuna watu wanapotosha sana kuhusu hilo.
 
Yapo mengi, Pole Pole yeye alichukulia Stiv ni mwana CCM mwenzao. Ndicho alichoelewa yeye kwenye ile interview. Bashite yeye hakuelewa chochote zile vocabulary hazipo kwenye dikshinari yake ya uvuvi wa samaki! Jiwe ndio kwanza yuko na dikshinari anajaribu kuirudia ile interview Kama atapata kuelewa chochote!
Nimecheka mpaka nimepaliwa makande

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yapo mengi, Pole Pole yeye alichukulia Stiv ni mwana CCM mwenzao. Ndicho alichoelewa yeye kwenye ile interview. Bashite yeye hakuelewa chochote zile vocabulary hazipo kwenye dikshinari yake ya uvuvi wa samaki! Jiwe ndio kwanza yuko na dikshinari anajaribu kuirudia ile interview Kama atapata kuelewa chochote!
Hapa ndipo watu wanaofikiri wana akili wanafeli. Mleta mada amefafanua kwa mapana akataka kila mtu aelezee ameelewaje mazungumzo hayo, wewe unakuja kuzungumzia wengine ambao nao wametizama kama wewe, kama ni mtihani mwalimu anakupa ZIRO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom