Kwa staili hii ya Sabodo naweza kabisa nikaamini CCM na CHADEMA lao ni moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa staili hii ya Sabodo naweza kabisa nikaamini CCM na CHADEMA lao ni moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calipso, Oct 21, 2011.

 1. C

  Calipso JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kuwa mimi ni mpinzani na tokea nimepata fahamu zangu nimekuwa upinzani na sikuwahi hata siku moja kukishabikia CCM ktk maisha yangu kwa mengi walotufanyia na nimekua ktk harakati za upinzani kuhakikisha tunaliondoa dudu CCM muda wangu wote,lkn kwa staili hii ya Sabodo kwa kweli inanipa wasi wasi sana, na nakumbuka na niliwahi kuleta thread hapa miaka ya nyuma kuwa CCM inaitumilia CHADEMA kuimaliza CUF na niliwahi kutoa baadhi ya ushahidi,na nilisema ipo siku kwa mfumo huu Chadema itachukua nafasi ya pili na kuipiku Cuf,na nilisema hilo ndio lengo la CCM ktk harakati zake za kuimaliza Cuf kabisa kisiasa


  Na kwa kweli CCM kwa hili wamefanikiwa,wanachoshindwa CCM ni kuwa znz hawawezi kabisa kuimaliza CUF na ndio maana safari hii wakawa hawana njia ya kufanya ila kukubali matakwa ya wananchi ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa,na ikiwa na hatua kubwa kwa Cuf ya kuchukua kabisa madaraka ktk uchaguzi mkuu ujao. Nathubutu kusema CHADEMA kwa hili la Sabodo kuna walakini,lkn mumezowea kukipakaza chama cha Cuf kuwa ni CCM-B kwa ajenda yenu ya pamoja na CCM kuimaliza CUF, lkn hili lenu la Sabodo mnalifanya kama hamlioni.


  Nakumbuka mlikipakazia uongo Cuf inafadhiliwa na Rostam ili kuwaaminisha wananchi kua Cuf si chama cha upinzani,na mlifanikiwa kwa hili na mengine,lkn hakuna ushahidi mlotoa mpaka leo kwa kua ni uongo mtupu na hakuna kitu kama hicho.


  Je! ingekuwa Cuf ndio wanafadhiliwa na Sabodo kama mnavofadhiliwa Chadema ingekuwaje? Naamini mungesema sana sana,lkn kwa kua kafadhiliwa CHADEMA mnapindisha mambo na kuleta tafsiri nyengine ili muaminike. lkn kwa hili la Sabodo kwa kweli CHADEMA hawana pakukimbilia,hilo mnalolifanya CHADEMA NA CCM kupitia Sabodo ni dudu kubwa sana na ufasadi wa hali ya juu ktk kuiangamiza democracy nchini kwa lengo lenu maalum lkna ipo siku litafichuka tu hili.

  Sijawahi kuona siasa ya namna hii ila CCM na CHADEMA wana lao. Ajabu kwa Sabodo mara wameenda viongozi wa Chadema mara viongozi wa CCM. labda niseme pale ni transit.

  Yetu macho ipo siku ukweli utafichuka. Kuna mengi yanafichwa na viongozi wa chadema na ccm.
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ok! lakini huo ni mtazamo tu!
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  unataka uifufue CCM B ionekane chama cha upinzani!
  haiwezekani na ccm b (CUF) iwe chama cha upinzani wewe!
  CUF IMEKUFA KABISAAA!
   
 4. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hapo uliposema ingekuwa Cuf pana ukweli kabisa.
   
 5. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mtoa thread unajichanganya, inawezekana unafanya makusudi au ni ujinga wako unakusumbua, kwa taarifa yako CUF ilifia Zanzibar baada ya kuolewa na CCM na hii ilitokana na uroho wa madaraka wa viongozi wa CUF. Baada ya hapo tumewasikia viongozi hao wakiukana upinzani kwa visingizio kibao.

  Fikiria mbunge wa CUF aliposimama bungeni na kuikataa kambi ya upinzani ati kwa sababu mnadhimu wa kambi hiyo mh. Tundu Lisu alitolewa nje ya bunge na naibu spika bwana Job Ndugai.

  Utasemaje CUF haiwezi kufa Zanzibar wakati kaburi lake tayari limesha titia? Unathubutu kujiita ati na wewe ni mpinzani kwa mawazo duni kama haya?
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Umejawa na umimi, unasukumwa na msongo wa akili, una lazimisha mambo .Kaa tulia angalia mwendo wa Chadema na linganisha na KAFU kabla hujaanza kulia lia na KAFU yako na CCM yenu .
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  Kilichoimaliza CUF ni ubinafsi wa Maalim Seif kukubali madaraka hewa na kwenda kugonga mvinyo Ikulu na kuacha CUF ikionekana kuwa nyumba ndogo ya CCM. Halafu unachekesha wewe unasema CCM imeshindwa kuimaliza CUF huko Zanzibar, waimalize mara ngapi? Kwani huko Zanzaibar kuna CUF au kuna CCM-B? Hivi hukumbuki siku ile Maalim Seif alipowatangazia waliokuwa wanachama wa CUF kuwa amemtambua Karume kuwa ni Rais wa Zanzibar jinsi wakina mama walivyoangua vilio? Basi siku ile ndiyo ilikuwa mauti ya iliyokuwa CUF, na muuaji alikuwa Maalim Seif mwenyewe, usiibebeshe lawama Chadema kwa ubinafsi wa Maalim Seif.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  kaka mtu akisha tumia masaburi kuwaza basi anakuwa kesha isha kama KAFU wewe pita tu .
   
 9. M

  MUGOLOZI Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nakupongeza mwanaJF kwa kumpa ukweli huyo mwana CUF kwamba chama chao kilifia Znzbar kwa uroho wa madaraka. Pili naomba mwenzetu ajue kuwa maji na mafuta havichangamani, yaani hata siku moja chatu na mbwa hawalali chumba kimoja.

  CCM janga lake kuu ni CDM yaani CCM wanaenda kwa wanganga kujua dawa ya kuwaondoa waasimu wao CDM itakuwaje tena wawe na lao moja? Fikiria sana jinsi CCM wanavyopata shida wawapo kwenye kampeni hadi kupata majibu, wanatumia hela nyingi, ahadi tele, mauaji na matambiko ili kuua Pple's power.

  Jamani lete wazo jingine hili umekosa, Sabodo kakunwa hadi kichogo ndo maana anafanya hivyo. Nawasihi mbadilishe jina la chama kwani hili lina ukakasi vinginevyo mtaendelea kushiriki chaguzi.
   
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mpaka hapo sijaona sehemu Chadema iliyoshiriki kama Mshenga kwenye ndoa yenu mliyoolewa na CCM. Na katika ile ndoa ya Mkeka mliyoolewa anayefaidika nayo ni CCM na wala sio nyie. Wewe mume umemkubali mwenyewe tena mlikuwa mnakutana kwa siri bila kumshirikisha mtu yeyote leo hii unakuja kutulilia eti ulikuwa mjinga kukubali kuolewa na CCM! Nendeni mkaulaumu ujinga wenu msimlaumu mtu yeyote hapa.
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  KAFU wakajipange tena then waanze upya...................mana sisi SISIEM tunawapiga chini sio mda
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kwa watuw anaoitakia mema CCM ni alzima wafanye kama anavyofanya Sabodo. Huyu bwana ameudhika sana na madudu aynayofanywa na chama hiki kikongwe ambacho kilistahili kuwa mfano wa kuingwa, lakini kimejigeuza kuwa mfano wa kuogopwa. sabodo anaipenda sana CCM na amegundua kuwa juhudi za kuwaambia wajirekebishe moja kwa moja haziwezi kufanikiwa. Ameramua kuisaidia Chadwema ili kuiamsha CCM, sasa kama CCM haiwezi kutambua hilo na ikaamka, hilo litakuwa ni kosa lao
   
 13. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani ungetuonyesha hapa jinsi Sabodo anavyofanana na Rostam kwa wizi wa rasilimali zetu na ufisadi labda ungeeleweka, lkn kitu unachojaribu kusema hapa hakieleweki, labda ujaribu kuja na hoja inayoeleweka.
   
 14. Mporipori

  Mporipori Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mtoa thread,

  Ulichosema ni kweli kabisa., CHADEMA kama hizi tuhuma sio za kweli basi tafadhali chukueni hatua.. Kuna hatari kubwa mtu mmoja kukifadhili chama kwa kiasi kikubwa hivyo. Itamfanya kuwa na ushawishi mkubwa sana katika chama na chochote atakachosema kitasikilizwa.. Atataka jambo fulani lifanyike, mtu fulani awekwe/aondolewe na mtajikuta mnafanya (NA KURUDIA YALE YALE YA CCM) Mtakataa kufanya wakati yeye ndio anawaweka mjini? ANGALIENI KUNA UWEZEKANO WA KUWA MNAWEKWA MFUKONI.. Na siku ya siku mkatakiwa mzitumikie hela mlizokuwa mnapewa.
  NAWASILISHA!
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hahahahaha mkuu umenichekesha sana....
   
 16. C

  Calipso JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  UP TO DATE: KADA WA CCM AIFADHILI CHADEMA.

  Plz! jibu hoja sio kumzungumzia mtu mwengine,hili ni lenu wana chadema na viongozi wenu. sijawahi kuona mwanachama na kada wa chama tawala akifadhili chama cha upinzani. karibu litafumuka hilo.

  Ukweli unauma
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... Julius Mtatiro in the BUILDING akitoa ya moyoni hapo.
   
 18. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mporipori umewasilisha vizuri sana, na umeweka kama angalizo, kitu ambacho ni kizuri.
  Sasa mleta maneno ni ameyumba sana kwenye uwasilishaji wake hadi imekuwa tena ni anailaumu CDM kwa kuanguka kwa CUF.
  Katika namna ya kuheshimu mawazo ya mtu ni sawa ila lazima mtu uwe focused katika kile unachosema.
   
 19. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tofauti ya Rostam na Sabodo,
  ni kuwa Rost - Tamu alikuwa anafadhili CUF kwa kificho ili akimalize na kafanikiwa
  Sir - Bodo, yeye hana siri wala ajenda ya siri, wala hafanyi kwa kificho, zaidi ya kuwaudhi CCM, na kuwarekebisha
  Ni mpenda demokrasia, kwa maoni yangu.
  Hawezi kulazimisha CDM wafuate matakwa yake
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Una anza hisia siyo ? Nani kasema Sabodo anautaka uanachama Chadema ? Unadhani Sabodo anaweza kuwa anataka ndani ya Chadema kwa afya yake ile ?
   
Loading...