sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Tumeona tumeshuhudia yanayojiri kutokana na maazimio ya mkutano mkuu na nimegundua kuwa utekelezaji wake utakuwa ni kizungumkuti.Nasema hivi baada ya kuhudhuria moja ya mikutano ya hadhara ambayo ndiyo effectively impact ya maazimio yaliyo kusudiwa.Kinacho jiri baada ya mkutano mkuu ni tofauti na kazi waliyotumwa wajumbe wa NEC katika kukiimarisha chama. Mwenyekiti wa taifa CCM alisema chama kimepoteza taswira yake,kiasi kimekimbiwa na wanachama wake.
Ina hitaji nguvu ya ziada ya kimkakati kurudisha imani ya wananchi ili waweze kuiamini serikali yao waliyoichagua wakiamini serikali hiyo itatekeleza yale wananchi waliyoyakusudia.Alifika mbali kwa kuwataka wajumbe wa NEC na viongozi mbalimbali wa CCM kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwa CCM kutoka kwa wapinzani wao. Kinyume na jitihada za kukiokoa chama wajumbe waliochaguliwa na kupewa majukumu wameshindwa kuendeleza yale ambayo waliyoyaagizwa na M/kiti na mkutano mkuu.Chama kinatuhumiwa kuwakumbatia wahalifu wenye mikono michafu na kuwapa nafasi za uongozi ilihali hawana status quo katika jamii walizotoka,matokeo yake ni chama kuzidi kujichimbia kaburi lake.
Kushindwa huku mapema kabla hata mwezi haujapita tangu kumalizika mkutano mkuu ni dalili mbaya kwa CCM kuelekea 2015.Jana nili hudhuria mkutano wa hadhara ambao agenda kuu ya mkutano mkuu huo haikujulikana pamoja na kuwa walipokea wanachama ambao wanaosema walikuwa vyama vya upinzani wakitokea CCM lakini hatimaye wamerudi tena. Mbali na hayo protocol haikuzingatiwa na kila mtu alivamia jukwaa kutaka kuongea bila utaratibu kama vile chama hakijui taratibu za vikao.Ni hivi punde mmoja wa wajumbe wa NEC kutoka wilaya ya Shinyanga mjini alituhumiwa kuwa ana mikono michafu,lakini akiwa ndiye mgeni rasmi alishindwa kujibu tuhuma hizo zaidi ya kuitaka chombo cha dola kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliyojitangazia Ngokolo ni jamhuri.Ikiwa wajumbe wote wa NEC toka wilaya ya Shinyanga wana tuhuma za mikono michafu hivi kweli chama hiki kitabaki salama.
Wameagizwa kushughulikia matatizo ya wananchi na kuyapeleka serikalini kwa kutumia vikao vyao,lakini ajabu majukwaa haya ya mikutano ya hadhara nayo yameingia mkenge kumtuhumu mtu binafsi kama Dr. Slaa kuwa ni mwanachama wa CCM bila kutatua matatizo ya watu wa Shinyanga,ili yaweze kutatuliwa na serikali kama walivyoagizwa.Dr. Slaa kuwa na kadi au kutokuwa na kadi ya CCM kunatatua vipi tatizo la maji mkoani hapa ilhali kuna mradi wa maji mkubwa toka ziwa Victoria uliogharimu mabilioni ya pesa ambao hauna tija kwa watu wa mkoa huu. Pesa kiasi gani za miradi ya maendeleo ambazo zinahujumiwa na miradi mingi kukwama.
Kiko wapi chuo chenu cha viongozi ambacho mwalimu alikitumia kupika viongozi waadilifu na wazalendo. Hivi kama Mwalimu angejaza mafisadi ndani ya CCM kwa miaka ile nchi kweli ingefika hapa tulipo? CCM kwa kuwatumia wajumbe wenu wapya ambao mnaamini pesa zao chafu ndizo zitakazo weza kuwavusha 2015 basi mna kazi ya ziada,kwani hata kitendo cha kuwarubuni wananchi warudi ndani ya CCM kwa staili ya kupewa mapesa si suluhisho la matatizo ndani yenu.Watarudisha kadi lakini mapenzi na imani kwa vyama vingine vitabaki pale pale.