Kwa stahili hii ya tume tutapata katiba shirikishi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa stahili hii ya tume tutapata katiba shirikishi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masulupwete, Jul 15, 2012.

 1. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Wakati wa mjadala wa bunge kujadili makadirio ya wizara ya sheria na katiba kuna mbunge kutoka kanda ya ziwa (sikumbuki jina lake) aliilalamikia kamati ya uratibu wa katiba ya warioba kuwa imekuwa ikichagua maeneo ya kwenda.

  Mbunge huyo akatolea mfano wa eneo moja huko kanda ya ziwa kuwa kamati imetembelea chini ya nusu ya maeneo husika (mfano kati kata 20 kamati inaenda kata 8 tu).

  Pia akadai kamati imekuwa ikikwepa kwenda kwenyw maeneo ambayo mbunge alidai yana watu wenye ufahamu mkubwa wa mambo na badala yake tume hutumia muda mwingi kutembelea maeneo yenye watu wenye ufahamu mdogo (naamini kigezo itakuwa ni idadi ya watu walioenda shule).

  Leo tar 15.07.12, mmoja wa wanakamati ya katiba ameskika kupitia tbc1 akidai kundi lililoenda visiwani unguja limeshangaa kukuta watu wa huko wamejipanga kutoa maoni kwa kuzingatia itikadi ya vyama vyao kinyume na utaratibu wa kamati wa mwananchi mmojammoja.

  Maswali yangu ni je, wananchi tumeandaliwa swsw kwa zoezi hili?
  Ripoti hii itakuwa na mawazo mengi, mengi kati yao yenye kukinzana, Je mwisho wa siku hiyo ripoti inachukua mawazo gani?
  Je kwa stahili hii ya kuchagua maeneo tutapata katiba shirikishi kweli? au ndo utakuwa mwanzo wa kuunda tume nyingine?
   
 2. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani hujui kuwa ni changa la macho kwa hii tume ya Jk na wanataka watengeneze katiba yao then waje waseme ni maoni ya wananchi na Jk ameamuwa kuwapa fungu la pesa lakutosha ili wafate matakwa yake yeye.
   
Loading...