The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,495
- 2,041
Nimekaa tu na kujiuliza kama raia wa kawaida kwamba serikali yetu inakopa na inaendelea kukopa, na inaonekana kila inapotokea uhitaji au upungufu wa aina yoyote, ufumbuzi unaowajia viongozi wetu vichwani ni kutafuta mahali pa kwenda kukopa.
Huenda wako sahihi kwa sababu wao Wana wataalam na wana washauri wa mambo ya kiuchumi ila wasiwasi wangu kama raia wa kawaida ni kwamba dunia imekuwa ikikumbwa na dharula mbalimbali zinazopelekea kubadilika kwa matarajio ya mapato.
Kwa mfano rahisi ni hili janga la corona ukame mafuriko vita na majanga mengine ya asili. Je ikitokea majanga ya namna hii halafu tumejaa madeni Hali itakuwaje? Je serikali yetu ina mpango wowote wa kujinusuru!?