johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,914
- 141,866
Awali pale mkoani palikuwa na mtu anaitwa RDD akisimamia shughuli zote za maendeleo. Cheo hiki kilifutwa baadaye lakini kule wilayani akina DED wakaachwa.
Nimefuatilia agizo la Waziri mkuu Majaliwa kwamba wakuu wa mikoa wakasimamie shughuli za biashara ya madini kule mikoani. Kisha nikamsikia Waziri Jaffo akisema RCs wote wanaitwa na Rais Magufuli jijini Dsm ili kupewa maelekezo ya utoaji wa vitambulisho vya ujasiriamali kwani wengi wao wamevurunda.
Ndiposa nimejiuliza hawa walioshindwa kugawa vitambulisho watawezaje kusimamia biashara nyeti na yenye changamoto ya madini. Ghafla nikaikumbuka nafasi ile ya RDD enzi za Mwalimu Nyerere.
Si vibaya Rais Magufuli akawarejesha Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mikoa na huko awajaze wataalamu siye makada tutabaki kwenye uRC na uDC.
Mungu wa mbinguni ambariki Rais Magufuli
Maendeleo hayana vyama!