Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!

Mag 3,
Ahsante sana nimekusoma na mimi nitaeleza yale ambayo nayajua kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mswada wa kitabu changu ulipitia mikono ya watu wengi na kwa hakika nilifaidika sana na ushauri wao.

Leo ninapokusoma najiona mimi wakati ule nimemaliza kuandika na wataalamu wanapitia kazi yangu.

Ushauri mkubwa ambao kwa kweli ulinisaidia sana ni kule kuniambia kuwa eleza historia kama uijuavyo kutokana na wazee wako na katika utafiti na futa katika akili yako kuwa kuna watu unawajibu.

Mwenzangu umetumbukia kwenye shimo nililotoka mimi miaka mingi nyuma.
Mimi nitaeleza yale niyajuayo.

Wazee wangu hawakuwa wajinga walikuwa wanajua kuwa Tanganyika ni Mandate Territory.
Tusomeni hapo chini:
''Having established the political committee, Abdulwahid settled down to write to all TAA branches in the territory in order to revitalise them.​
Major issue facing Abdulwahid and the political committee was the status of Tanganyika as a mandate territory.​
Abdulwahid engaged Earle Seaton, a lawyer from Bermuda based in Moshi, and attached him to the committee to advise them on constitutional law and decolonisation of mandate territories under foreign rule.​
The United Nations Trusteeship Council had already sent its first visiting mission to Tanganyika in 1948; but not much was gained from this mission.​
The TAA headquarters in Dar es Salaam under Dr Kyaruzi and Abdulwahid with the backing of the political committee was now rising from its deep slumber.​
What was now required were serious issues to stimulate the minds of the young intellectuals.​
The TAA leadership did not have to look far.​
These issues came in the form of the Constitutional Development Committee set up by Governor Edward Twining and the Meru land evictions.''​

Mag 3,
Kuhusu misukosuko:

''Abdulwahid was elected General Secretary of the Dar es Salaam Dockworkers’ Union.[1]

Mwaka mmoja baada ya Abdul kuchaguliwa kuongoza chama hiki cha makuli mgomo mkubwa ulitokea ambao ulitikisa nchi nzima.​
Hii ilikuwa mwaka wa 1949 na babu yangu aliupokea mgomo huu wa makuli wa Dar es Salaam akiwa kiongozi wa wafanyakazi wa reli Tabora na wakafanya mgomo kuwaunga mkono wazalendo wenzao wa bandarini Dar es Salaam.​
Ingia hapo chini:​
[1] Iliffe, ‘A History of Dockworkers...’ p.119. Tanganyika Labour Report, 1947.

Mag 3,
Si kweli kuwa alikuwa Nyerere ndiye aliyezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu Tanganyika na uraia wa Malkia wa Uingereza.

Tusomeni hapo chini:

''last agenda item was for discussion was the status of the Queen vis-a-vis the Africans of Tanganyika and the Meru evictions. It be remembered that in 1951, Ally Sykes as TAGSA secretary had made remarks against the status of British jurisdiction over Tanganyika.''​
Mag 3,
Mzee Rupia alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU lakini hakupatapo kutoa nyumba yake kuwa ofisi ya TANU.

Wengi walitoa nyumbza zao kuwa ofisi ya TANU katika hao alikuwa Ali Msham ambae tawi lake lilikuwa Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa na akamfungulia Mama Maria duka la kuuza mafuta ya TAA.

Tusomeni hapo chini:


Mag 3,
Namjua vizuri sana Chief David Kidaha Makwaia na nimepata kumuona kwa kuwa mwanae alikuwa rafiki yangu na tukisoma darasa moja St. Joseph's Convent.

Lakini zaidi nimeelezwa mengi ya Chief Kidaha na Mama Daisy mke wa Abdul Sykes kama hutaki kuamini ni sawa tu kwangu.

Hayo mengine kuwa Cecil Matola ndiye muasisi wa African Association si jambo la mimi kubisahana na wewe wala kuhusu ofisi ya chama hicho.

Mimi ndiye niliyeweka hadharani piacha ya mwaka wa 1933 ufunguzi wa ofisi hiyo na nimeitoa katika Nyaraza za Sykes:

Angalia picha hiyo hapo chini:

1575146549664.png
 
Mohamed Said, kuna maswali machache ningependa uyatolee ufafanuzi...
  • Je unakubali kuwa Gavana Cameron ndiye alitoa jengo litumiwe na civil servants waandamizi wa serikali weusi ?
  • Je jengo hilo lilitolewa kwa masharti gani?
  • Je lilikuwa linamilikiwa na nani kabla ya kuwa la ofisi ya AA na kwa sasa kiwanja kilipokuwa hili jengo kinamilikiwa na nani?
  • Je kabla ya hili jengo kutolewa na Gavana Cameron, civil servants weusi walikuwa wakikutana wapi baada ya kazi?
  • Je wakati linatolewa nani kiongozi mkuu yupi alikabidhiwa usimamizi wa hili jengo kwa niaba ya AA?
  • Je baada ya kufariki Rais muasisi wa AA Cecil Matola, uchaguzi ulifanyika wa mtu kuchukua nafasi yake?
 
Mohamed Said, kuna maswali machache ningependa uyatolee ufafanuzi...
  • Je unakubali kuwa Gavana Cameron ndiye alitoa jengo litumiwe na civil servants waandamizi wa serikali weusi ?
  • Je jengo hilo lilitolewa kwa masharti gani?
  • Je lilikuwa linamilikiwa na nani kabla ya kuwa la ofisi ya AA na kwa sasa kiwanja kilipokuwa hili jengo kinamilikiwa na nani?
  • Je kabla ya hili jengo kutolewa na Gavana Cameron, civil servants weusi walikuwa wakikutana wapi baada ya kazi?
  • Je wakati linatolewa nani kiongozi mkuu yupi alikabidhiwa usimamizi wa hili jengo kwa niaba ya AA?
  • Je baada ya kufariki Rais muasisi wa AA Cecil Matola, uchaguzi ulifanyika wa mtu kuchukua nafasi yake?
Mag3,
Maswali hayo uliyoniuliza atayajibu Kleist Sykes (1894 - 1949) kwani majibu yake yamo katika kitabu chake ambacho nimekitaja hapa mara kadhaa (Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114).

Swali la Kwanza:
Kleist anaeleza kuwa jengo la ofisi ya African Association walijenga kwa kujitolea wakienda pale kufanya kazi ya ujenzi kila Jumapili.

Abdul Sykes anasema yeye akiwa mtoto mdogo alikuwa akifuatana na baba yake pale.

Swali la Pili:
Sina jibu.

Swali la Tatu:
Hapakuwa na jengo pale kilikuwa kiwanja kitupu.

Swali la Nne:
Sina jibu

Swali la Tano:
Jengo halikutolewa kwa kuwa lilijengwa kati ya 1929 - 1933

Swali la Sita:
Uchaguzi ulifanyika na Mzee bin Sudi akachukua nafasi yake.
 
Kwanza sijifanyi mimi ndio msahihishaji wa urongo, urongo, urongo, bali mimi ni mtu mkweli na muwazi, nilipouona urongo ule wa matamshi ya urongo ya Mkuu Mohammed Said akilihutubia taifa katika mahojiano yale, jukumu langu lilikuwa moja tuu, kuibuka na kusema ule ni urongo.

Nilikueleza wewe katika lili lile bandiko lako la maorongo kuwa ulicholeta humu ni urongo, na nikamkabili Mkuu Maalim na kumweleza wazi hicho alichotamka ni urongo.

Maalim akanipa list ya.vitabu vya mimi kwenda kuvisoma ambako nayeye ndiko alikopatia urongo ule, nikasema nitavitafuta, nitavisoma na nikithibitisha ni kweli, nitamuomba radhi Mkuu Maalim Mohammed Said na kusahihisha huo urongo ili ukweli ujulikane ikiwemo kumswafi Mkuu Mohammed Said, kazi hii ya kutafuta vitabu adimu sio kazi ndogo, inahitaji time, money and resources nyingine, hivyo bado najipanga.

Hili la Mama Daisy sijasema popote namfahamu kuliko Mkuu Maalim Mohamned Said anavyomfahamu, ila kwa vile nimeongea nae mimi mwenyewe, kuna uwezekano kuna vitu aliongea na mimi, na hakuwahi kuongea na Maalim Mohammed Said, kama ilivyo simulizi ya Sheikh Takadiri na Mwalumu Nyerere inayosimuliwa humu na Malim Mohammed Said, kuna mengine ya Sheikh Takadiri na Nyerere, Mohammed Said hakuwahi kuyahadithia, mfano la kusema Mtume Mohamadi (SAW), ni Mwarabu, ni Mtume wa Waarabu na sio Mtume wetu sisi Waswahili, sisi mtume wetu ni Nyerere!.

Kwa bahati mbaya mimi sijajaliwa kipaji cha kuandika kama Mkuu Mohamned Said lakini mimi nimezungumza na Nyerere face to face, japo sio kuhusu historia bali kuhusu mambo mengine muhimu zaidi kwa taifa letu kuliko bygones, ila sikuandika, nimerekodi.

Hivyo hakuna wa kushindana na Mohammed Said katika anga zake, ila lengo la bandiko hili ni Mohammed Said asibezwe, licha ya maurongo yale, pia kuna mengine ni ukweli mchungu, ila pia nikatoa angalizo asipuuzwe, na mtu wa kwanza kufaidika na bandiko hili ni wewe, kwa kukimbia mbio mbio ukayatoa yale maurongo yake uliyoleta kwenye ile video, hivyo bandiko hili limekusaidia hata wewe, kwa sababu naamini wakati ukiileta video ile hukujua kuwa ina maurongo, lakini nilipokueleza ule ni urongo,naamini uliisikiliza tena, ukaiondoa, hivyo urongo ule hauendelei kusambaa, mimi nakua ni raia mwema kuisaudia jamii isilishwe maurongo,sasa kazi iliyobakia ni moja tuu, kuuthibitisha urongo ule kupitia homework niyopewa.
P.
Bado tunasubiri. Miezi 6 au zaidi imeshakata.
 
Bado tunasubiri.
As long as hakuna time frame tulioweka, endelea kusubiria.
NB. Ukimtuhumu mtu kitu cha urongo, huku ukijua ni urongo, ila unamtuhumu ili ahukumiwe kwa urongo, then sehemu ya karma ya tuhuma zile za urongo itakuwa juu yako, na kila anayemlaani mtuhumiwa kwa urongo ule, karma ya laana ile itamrudia na mlaaniwa badala ya kulaanika, atabarikiwa!.
P.
 
As long as hakuna time frame tulioweka, endelea kusubiria.
NB. Ukimtuhumu mtu kitu cha urongo, huku ukijua ni urongo, ila unamtuhumu ili ahukumiwe kwa urongo, then sehemu ya karma ya tuhuma zile za urongo itakuwa juu yako, na kila anayemlaani mtuhumiwa kwa urongo ule, karma ya laana ile itamrudia na mlaaniwa badala ya kulaanika, atabarikiwa!.
P.
Nilikuahidi kukukumbusha na nitaendelea kukukumbusha kila baada ya muda kwani nilikuambia wapo walioahidi kama wewe miaka sasa hawajarudi.

Na wewe nnauhakika hautarudi na jibu kwani ukweli unaujuwa. Dunia ya leo si ya kutafuta kitabu miezi sita ukikose. Unaendelea kuumbuka.

Hayo ya "karma" hujayaona? Umekumbushwa huku, kama sikosei post namba 28...

 
Swali la Kwanza:
Kleist anaeleza kuwa jengo la ofisi ya African Association walijenga kwa kujitolea wakienda pale kufanya kazi ya ujenzi kila Jumapili. Abdul Sykes anasema yeye akiwa mtoto mdogo alikuwa akifuatana na baba yake pale.

Swali la Tatu:
Hapakuwa na jengo pale kilikuwa kiwanja kitupu.
Kwa maswali mengine umepatia kwa kukiri kwamba hujui lakini kwa haya mawili hapo juu unasema uongo. Kama unakataa kwamba Gavana Cameroun hakutoa hilo jengo hapo ndipo utata unapoanzia...je jengo alilolitoa Gavana Cameroun kwa waliokuwa wafanya kazi wa serikali weusi, lilipotelea wapi baada ya kifo cha Rais muasisi wa AA, Mwalimu Cecil Matola, kuaga dunia (RIP!)?

Kwa taarifa tu kwa Pascal Mayalla...huko nyuma niliwahii kuchangia hivi;

  1. Mohamed Said kwa asili ni 3rd Generation ya wahamiaji wa Kimanyema kutoka Magharibi ya Tanzania katika eneo lililojulikana kama Congo. Hawa walikuwa ni Waislaam.
  2. Ukoo wa Sykes kwa asili pia ni 3rd Generation ya askari wa Kizulu kutoka Afrika Kusini walioletwa na Wajerumani kuja Tanganyika wakati wa mapambano dhidi ya Uingereza. Hawa walikuwa ni Wakristo.
Mohamed Said anapohadithia kuhusu wapiganaji wa uhuru wa Tanganyika, anayapa uzito sana haya makundi mawili (Manyema na Wazulu) kwamba ndio waliopigania uhuru wa Tanganyika. Bila shaka swali ambalo sisi Watangannyika tunatakiwa tujiulize ni kwamba, je babu zetu walikuwa wapi? Je bila ya hawa walowezi Watanganyika wasingepata uhuru?

Chama cha wafanyakazi AA kilipoanzishwa Tanganyika mwaka 1927 Rais wake muasisi na Kiongozi wake Mkuu, Cecil Matola, Mtanganyika na Myao, hapewi uzito wowote na Moamed Said kama anaopewa Katibu wake, Mzulu.

Baada ya mauti kumkuta Cecil Matola, nafasi yake ilichukuliwa na Ramadhani Ali, Mtanganyika na Mzaramo lakini huyu naye hatajwi kabisa na Mohamed Said katika ngano zake.

TAA ilipozaliwa upya mwishoni mwa miaka ya 1940s, Rais wake muasisi na Kiongozi wake Mkuu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Mtanganyika na Mhaya, hapewi uzito na Mohamed Said kama anaopewa Katibu wake, Mmanyema

Hivyo hivyo TANU ilipozaliwa mwaka 1954, Rais wake muasisi na Kiongozi wake Mkuu Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Mtanganyika na Mzanaki...

Katika historia ya Tanganyika haya makabila mawili, Manyema na Zulu, je kuna popote yanatajwa kama Watanganyika? Je ni kitu gani kinawaunganisha hawa Manyema (Waislaam) na Wazulu (Wakristo)? Je ni kwa sababu ya kuoleana? Kuishi pamoja kota za Gerezani? Kutaka na wao historia ya Watanganyika kuwatambua? Hii ya mwisho Mohamed Said kaivalia njuga na anajitahidi kweli kweli ifanikiwe na wao watambulike.

Tanganyika tulikuwa na makabila mengi tu lakini haya mawili si miongoni mwao. Wakati Watanganyika wananyanyaswa na Wajerumani, walowezi hawa walikuwa upande wa Wajerumani. Baada ya Wajerumani kutolewa mkuku na Waingereza wengi wa hawa walirudi walikotoka lakini wachache waliamua kubaki na ndio hawa Wazee wa Mohamed Said anaodai walipigania uhuru wa Tanganyika.
 
Wanabodi, mimi ni mshabiki na mfuasi wa simulizi za mwana Jf maarufu, mwenye powers fulani za ushawishi, Mkuu Maalim Mohamad said, nyingi ya simulizi zake zina some religious controversies zinazoibua very heated debates humu jukwaani, kwa baadhi ya watu kumsupport asemacho ni kweli, na wengine kubeza, kuwa ni urongo. Most times, supportes wengi ni watu wa dini fulani, na wabezaji ni watu wa dini fulani!.

Huu uzi ni wa kumtetea Mkuu Maalim Mohamed Said, kuwa japo ni kweli kwenye baadhi ya simulizi zake kuna urongo fulani wa makusudi wenye malengo fulani mahsus, lakini sio simulizi zote ni urongo, nyingine zina ukweli fulani, ambao ni ukweli mchungu, hivyo asibezwe.

P.
Kuna hoja nyingine ya Mkuu Maalim Mohamed Said hapa Je, kuna tofauti ya IQ za Watanzania kutokana na dini zao? Kuna dini wanapasi sana, wanafeli sana, huwa wanabaguliwa na kudhulumiwa?
P
 
Back
Top Bottom