mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Mwaka 1959, wanasosholojia wa Marekani, John French na Bertram Raven, waliandika chapisho lenye jina, The Bases of Power, yaani misingi ya nguvu, katika chapisho hilo waliandika vyanzo vitano vya kumfanya mtu awe na nguvu ya kimamlaka kwenye taasisi yake.
Vyanzo hivyo ni uhalali wa mamlaka, utaalamu au elimu, nguvu ya kulazimisha, nguvu za zawadi na nguvu ya uhusiano. Kama kunakuwa na kiongozi mwenye nguvu kwenye taasisi yake basi atakuwa anasababishiwa chanzo kimojawapo au zaidi kati ya hivyo.
Ufafanuzi wake ni huu; Nguvu ya Uhalali (Legitimate Power), kwamba kiongozi anaweza kuwa na nguvu kubwa kwenye taasisi yake kwa sababu ya uhalali wa uongozi wake. Sauti yake inasikilizwa kwa sababu mamlaka yake yanakubalika kwa kila mtu.
Nguvu ya utaalamu (Expert power), maana yake ni kwamba kwenye taasisi kiongozi anaweza kuwa na nguvu kubwa kwa sababu watu wake wanamheshimu na kumtii kutokana na utaalamu alionao au elimu kubwa kiasi kwamba mengi hayawezi kufanyika bila mkono wake.
Nguvu ya Uhusiano (Referent Power), hii ni kumaanisha kuwa kiongozi anaweza kuwa na nguvu kwenye taasisi yake kutokana na uhusiano wake na watu anaowaongoza.
Jinsi mtu anavyoshirikiana na watu wake, kwa hiyo wanampenda, wanamheshimu, wanahamasika naye na wanamtii.
Nguvu ya kulazimisha (Coercive Power), kwamba kwenye taasisi watu wanalazimishwa kumwogopa kiongozi, kwa hiyo watu wanamtii kwa kumwogopa, maana wanahofia wasipofanya hivyo maisha yao yatakuwa magumu.
Nguvu ya Zawadi (Reward Power), kiongozi anaweza kukubalika kwa sababu anawashawishi watu wa taasisi kwa maslahi bora, kama mishahara, posho na bakshishi. Kwa hiyo watu wanamtii kutokana na kile ambacho wanapata.
Nguvu ndani ya CUF
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, mwanzoni alipewa utukufu kwa sababu ya nguvu ya utaalamu. Aliimbwa na kutukuzwa kwa sifa kwamba ni mchumi bora duniani. Utaalamu wake ukawafanya watu wampende kisha apate nguvu ya uhalali.
Baada ya Lipumba kujiuzulu uenyekiti Julai 2015 kisha kurudi mwaka jana na kusema anatengua barua yake ya kujiuzulu, mwisho Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akamthibitisha, kilichofuata ni kuwa Lipumba alibebwa na nguvu ya kulazimisha.
Tangu Lipumba atambuliwe na msajili, maana yake CUF walilazimishwa na mamlaka ya juu kumkubali kuwa mwenyekiti wao. Lipumba akafanya kazi za chama kutoka Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam, kutokana na nguvu ya mamlaka za nchi.
Katibu Mkuu wa Cuf, Seif Sharif Hamad, alibeba kundi kubwa la viongozi wa juu wa chama hicho kwa sababu ya nguvu ya uhusiano. Ukweli ambao haupingiki ni kuwa Seif ni kiongozi pendwa na anakubalika kwa viongozi wengi wa chama hicho.
Seif amekuwa nembo ya CUF na viongozi wengi wanaamini kuwa huwezi kuwa CUF kama hukubaliki na Seif. Nguvu ya uhusiano aliyonayo Seif ndiyo iliyosababisha Lipumba awe na kundi ndogo linalomuunga mkono hata baada ya kutambuliwa na msajili.
Nguvu ya zawadi ikawa sababu nyingine ya Seif kubeba kundi kubwa, kwamba ilikuwa rahisi watu kutetea maslahi yao kwa kuungana kwenye kundi la Seif na wale wa Lipumba walionekana wazi kuwa wanapoteza.
Suala la Lipumba kutambuliwa na msajili, watu wa Seif waliona kuwa ni la mbio za sakafuni tu, kwamba muda ungewadia angeondoka, hivyo wangebaki wanapanga safu yao mpya ya uongozi.
Hali ya sasa CUF
Uamuzi wa msajili kusitisha ruzuku ya CUF ilikuwa ni pigo kubwa kila upande, ila baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba upande wa Lipumba wamepewa ruzuku ni maumivu makali kwa akina Seif.
Fedha ni sababu ya vyanzo vitatu vya nguvu. Hivyo, kwa sasa upande wa Lipumba ndiyo ambao wanashika nyenzo muhimu ya kuwafanya wawe na nguvu kwenye chama.
Bila fedha huwezi kufanya vikao, wajumbe wakitaka posho na nauli utawapa nini? Mwenye fedha ndiye anaweza kushiriki uchaguzi kikamilifu, maana anaweza kugharamia kampeni.
Aliye na fedha ndiye anaweza kuifanya ofisi ipate utulivu kwa sababu watendaji watalipwa mishahara na shughuli nyingine za uendeshaji wa chama zinaweza kufanyika vizuri.
Mwenye fedha ndiye anaweza kuhudumia ofisi za chama mikoani na wilayani, maana viongozi wa maeneno wanapohitaji fedha wataomba na kupewa. Ukiwa huna chochote unawapa nini?
Kwa msingi huo, aliye na fedha ndiye ambaye anaweza kufanya chama kiwe hai katika ngazi zote. Ni watu wachache wenye kusimamia kile wanachokiamini na wale wasio na uhakika wa maisha yao ya kisiasa kupitia upande wenye nguvu ndiyo wanaweza kung’ang’ana na wasio uhakika wa kuendesha chama.
Isisahaulike kuwa chama kinahitaji wanasheria kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kitaifa hata ngazi za chini. Aliye na fedha ndiye angalau anaweza kuwa na uhakika kugharamia wanasheria.
Siasa za upinzani Tanzania na Afrika kwa jumla, zina changamoto nyingi. Kama viongozi hawana fedha za ruzuku, maana yake wanaweza kuwaacha wanachama au viongozi wao wajigharamie mawakili katika kesi zao. Aliye na fedha anaweza kunyoosha mkono kumsaidia mwenye uhitaji.
Anayesaidiwa naye atasema: “Huyu ndiye safi maana ukiwa na tatizo yupo na wewe.” Hatazingatia kuwa ambaye hakumpa fedha alifanya hivyo kwa sababu hakuwa nazo. Usisahaulike msemo wa “mkono mtupu haulambwi.”
Mkorogo wa CUF na msajili
Kwanza kabisa lugha ambayo ilitumiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro kuwa fedha za chama zimeibwa siyo sahihi. Alipaswa kutamka kuwa fedha za ruzuku za chama zimetolewa kwa upande mmoja.
Sababu ni kwamba msajili wa vyama anamtambua Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama. Anamtambua pia Seif kama katibu mkuu, kisha hamtambui Mtatiro na kamati yake.
Kwa maana hiyo, Mtatiro anapohoji fedha za ruzuku ya chama kutolewa upande mmoja, msajili akiulizwa ilikuwaje akaidhinisha, anaweza kurudisha swali badala ya kujibu: “Mtatiro anahoji kama nani?”
Mantiki hiyo ni kuwa Seif ndiye hasa alitakiwa kuhoji utolewaji wa fedha za ruzuku kwa upande mmoja wa akina Lipumba, wakati inafahamika kuna pande mbili ambazo zina mgogoro. Na yeye msajili kwa kutambua mgogoro huo ndiyo sababu alizuia ruzuku kwa chama mwaka jana.
Maswali; nini kimetokea mpaka msajili aruhusu fedha za chama ziende upande mmoja wa akina Lipumba wakati mwanzoni alizuia ruzuku kwa maelezo hana imani na usimamizi wa fedha za chama?
Kama msajili alijiridhisha kuwa ana imani na usimamizi wa fedha kwa upande wa akina Lipumba ni kwa nini hakumjulisha Seif kama katibu mkuu kuhusu mabadiliko aliyoyafanya ya njia za utoaji ruzuku za chama?
Fedha hazikutoka Benki Kuu moja kwa moja zikaenda kwa mtu binafsi, bali ziliingizwa kwenye akaunti ya CUF, Wilaya ya Temeke. Kwa maana hiyo fedha zililipwa katika njia ambazo hazikuwa zenye kukubalika kwa pande zote mbili. Kwa nini wilayani na siyo taifa ambako malipo yote ya ruzuku hupitia?
Msajili wa vyama ndiye msimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa kutoka mfuko mkuu wa Serikali (Hazina). Hazina haikai na fedha, kwao zinasoma tarakimu tu, fedha zinahifadhiwa Benki Kuu. Msajili anaporuhusu fedha za vyama zilipwe, maana yake ndiye mwenye mamlaka kisheria, kwa hiyo Hazina na Benki Kuu ni watekelezaji tu.
Haipaswi kusemwa kuwa fedha zimeibwa, wakati walioidhinishiwa ndiyo wenye kufanya kazi kutoka makao makuu ya chama. Wanamiliki nyaraka zote na wanatambuliwa na msajili.
Malalamiko yanayotakiwa kusimamiwa na CUF, yanapaswa kutolewa na Seif kwamba msajili anatoa upendeleo kwa akina Lipumba wakati mgogoro wa uongozi kwenye chama haujaisha.
Mgogoro unakwenda kwisha
Hizi ni nyakati ambazo upande wa Seif unakumbwa na majaribu mazito. Watiifu wao wa kweli watajulikana. Upande wa Lipumba unabebwa na fedha pamoja na nguvu ya kutambulika na msajili ambaye ndiye mlezi wa vyama vya siasa.
Upande wa Seif mpaka sasa unabebwa na nguvu ya uhalali, kwa maana kundi kubwa linaendelea kuamini kuwa Lipumba alishapoteza sifa ya kuwa mwenyekiti.
Hata hivyo, sasa hivi Lipumba anayo fursa ya kujitengenezea uhalali kwa kuungwa mkono na kundi kubwa kwa sababu ya uwezo wa kifedha pamoja na kubebwa na mamlaka ya msajili.
Kwa mantiki hiyo, kwa vile anakubalika na msajili, na kwa asili ya siasa za Tanzania, ni rahisi sasa Lipumba kuchukua kundi kubwa kisha kujipa uhalali hata kufika wakati ikaonekana akina Seif hawana pakushika.
Uamuzi wa kutoa fedha kwa akina Lipumba tafsiri yake ni kuwa msajili wa vyama ameamua kumaliza mgogoro wa CUF kwa kutumia sayansi ya jamii. Kwamba sasa Lipumba ndiye anakwenda kuwa na nguvu nyingi, akina Seif wasiwe na chao.
Chanzo: Maandishi Genius