Kwa Sheria hii ya Rais kutowajibika kwa makosa aliyofanya..... Tutalia sana.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Sheria hii ya Rais kutowajibika kwa makosa aliyofanya..... Tutalia sana..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Aug 29, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,216
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Nimejiuliza hawa watu wanapata wapi ujasiri wa kuua, kuiba, kupindisha sheria na hata mikataba feki wanayopingia roho haziwaumi kwa nini? Kumbe kinga yao wote ni hii sheria.
  Watoa amri wote kumbe ni wateule wa Rais kwa hiyo wanajua wapo salama chini ya vifungu vya sheria walivyotunga kwa masilahi yao wenyewe.
  Hii sheria ya rais kutowajibika kwa makosa aliyofanya akiwa madarakani ndiyo mbaya kupita zote na itatumaliza Watanzania.
  Hii imepelekea kila kiongozi sasa akishitakiwa anamtaja Rais mstaafu kuhusika ktk kesi yake akikiri basi kesi inakwisha kwani wako juu ya sheria.
  Sasa hawa wanaonyanyasa raia kwa sasa kama hii sheria isingekuwapo sidhani kama Kikwete angekaa kimya bila kukemea wasaidizi wake maana angejua mwisho wa siku angeulizwa yeye.
  Jamani tuhakikishe tunapata katiba safi itakayoliongoza taifa letu vema bila kuwa na miungu watu.
  Ni mawazo yangu tu weka yako tupate kitu safi.
   
Loading...