Kwa serikali ya sasa ni Diaspora gani alitolewa nje kuja kusaidia nchi?

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,588
2,000
Nakumbuka enzi za Kikwete na Mkapa watanzania wengi wenye taaluma mbalimbali waliokua wanafanyakazi nje ya nchi waliletwa kuja kusaidia kuleta maendeleo kwa ujuzi na uzoefu wao walioupata huko nje.

Kwa mfano Mkapa alimleta Daudi Balali, Kikwete akamleta Ndulu, yule mama wa uwekezaji, mama Tibaijuka, tpdc na mashirika mengine.

Lakini pia Kikwete alikua anawachukua watu kutoka private sector nchini na kuwaingiza kwenye public sector kama Mchechu wa NHC, Bade wa TRA na wengine.

Je, kwa serikali hii ni diaspora gani walipewa nafasi au wameletwa kusaidia kuleta maendeleo? Naona ma dokta na maprofesa wengi waliokula shavu ni wa hapa hapa nchini kwenye vyuo vyetu labda ukimtoa wa tpdc ambae cv yake inaonyesha ni watanzania wachache wanaweza ku-match qualifications, exposure na experience yake.
 

kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,053
2,000
Kwa hali ya sasa hawawezi kuja kwasababu jiwe ni dikteta yeye anataka afanyekazi peke yake na anataka aonekane kila kitu ameunda yeye yaani Baraza la mawaziri ni kivuli tu. Pia atawalipa mshahara upi wakati watumishi wake wanalia njaa isiyokuwa na mfano,umeona Dr Ndugulile alivyotolewa mkuku kisa tu amemkosoa !kwenye utawala wa kidikteta wataalamu hawatakiwi wanafaa wale wanaomlamba mikono na miguu !!Angalia Mwigulu,Nape,nk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom