Wakati wa kampeni alikuwa ni bingwa wa kutaja matatizo ya vijana kwa hisia huku akitaka kutokwa na machozi.
Siku mia moja baadae anataka vijana tufanye kazi kwa nguvu, hata biashara zetu za pooltable, betting zinazolipa kodi halali ya serikali sasa nazo zimekuwa haramu zaidi ya madawa ya kulevya.
Sasa sisi vijana ambao hatuna ajira, mjini tunaishi kwa ndugu mnataka tukafanye wapi kazi? Au unatufundisha tukakabe? Maana umewaagiza wakuu wa mikoa kwamba watukamate watupeleke kwenye makambi, yani umelipaka rangi jina magereza na kuwa makambi. Sawa kama huko ndio degree yangu ya IT itakakokwenda kutumika. Hakuna shida mkuu kama Ile mitaji uliyotuahidi tutaikuta huko magereza.
Hivi inamaana huku kwamba kule kijijini vijana hatuna hata robo ekari, sasa Mheshimiwa unataka tukalime wapi? Sawa mkuu labda huko kwenye makambi ndio kuna ardhi ya kwa ajili yetu vijana. Lakini huku mtaani tunamiliki vyeti tu na hata familia zetu hazina chochote.
Lakini hivi kilimo kingekuwa na tija hii nchi yetu si ingekuwa inalingana na Marekani? Maana asilimia zaidi ya sabini ni wakulima ambao mnawaahidi pembejeo na mpaka sasa hamjapeleka, mnashindwa kuwatafutia masoko matokeo yake mazao wanapikia pombe.
Vijana tulitarajia utatuonyesha muelekeo wa kutuwezesha kama ulivyoahidi, lakini kama ni kukamatana maana yake vijana wa taifa hili wote tumekuwa kama machinga. kweli hii ni mbele kwa Mbele.