Kwa Sekta Nyeti ya Nishati na Madini kwa nini Kikwete Hamteui Magufuli Kuisimamia?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Sekta Nyeti ya Nishati na Madini kwa nini Kikwete Hamteui Magufuli Kuisimamia?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Nov 20, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,
  Sekta ya Nishati na Madini ni mojawapo ya mihimili mikubwa ya uchumi wa nchi yetu. Kinachonishangaza ni kwamba pamoja na sekta hii kuwa muhimu imekuwa ikikabidhiwa kwa watu ambao hawana rekodi yoyote ya maana kiutendaji na hata kitabia. Na ndiyo maana Sekta hii imejaa kashfa nyingi za kuliibia taifa mabilioni ya fedha. Nina imani mchangao huu unawapata watz wengi. Sasa swali ninalojiuliza ni kwa nini mawaziri ambao wameonesha kwa vitendo umahiri wao wa kusimamia Sekta wanazoteuliwa wasipewe Sekta hii muhimu?!? Watu kama akina Magufuli wanaishia kuundiwa Wizara ya Mifugo na Samaki wakati vijana wasioeleweka hata wametokea wapi akina Ngereja na Malima wanapewa Sekta nyeti namna hiyo!!!!! Kwa nini!!!? Wadau hapa lazima kuna siri imefichika.

  Wengi wetu tulidhani kikwete ameamua kuwapatia vijana madaraka lakini sasa tumeanza kupata wasiwasi kwamba ujana ulikuwa ni coincidence tu. Kilichozingatiwa hapo ni hicho kilichofichika.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wizara hiyo ndiyo yenye dili chafu nyingi!! Siku tukiweza kumuondoa mchawi kwenye hiyo wizara basi tutakimbiza uchumi mara moja kunakotakiwa. Lakini wajanja walishawahi site, ni kuendelea kuwabana waboreshe huduma na kuangalia namna ya kurekebisha taratibu zingine kuhusu hiyo wizara.
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe. Inawezekana deal kubwa zote za 'wakubwa' zimelala hapo.
   
Loading...