Kwa sasa viongozi wa dini ni hatari kuliko hata waganga wa kienyeji

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,328
2,282
Inasikitisha sana viongozi wengi kuacha kufanya walichoagizwa na kuanza kuogopesha watu.

Badala ya kufundisha kilicho kwenye maandiko na kuacha mtu afanye uamuzi, wengi wanapamba zaidi kuwatisha.

Kiongozi anaedai anahubiri anahubiri hivi
Kama umesoma huna kazi una jini mikosi,kama ndoa yako haina amani kuna jini mahaba, kama hupati mchumba una sijui jini gan...unahisi watoto wako hawafanyi vizuri shule basi chukua hatua haraka sana...njoo kanisani kwetu tukuombee n.k.

Hapo amehubiri nini? Amefundisha nini? Umeamua kuwatisha watu kwa njia hiyo watamjuaje Mungu? Ni wapi Yesu aliwatisha watu badala ya kuwahubiria?

Hakuna jambo la maana kama kujifunza kweli ili ikuweke huru,bila kujua kweli utaogopa matukio ambayo ni ya kawaida kabisa ukidhani kweli unamajini tofauti sababu kila kiongozi utakayemsikiliza lazma ataaja kitu ambacho wewe kinakugusa. Kuweni makini sana acheni kufuata upepo.
 
Wamekua na maono kama waganga, tatizo hakuombei ukapona kabisa ukaenda....nilaza uwe muumini wake uhudhurie ibada, hapo ndio wana kula sadaka sasa.
 
nenda youtube andika MAHUBURI TV, achana na hao wahun wauza mafuta
 
Kama ilivyo misimu ya hali ya hewa Duniani yaani mvua, baridi, kipupwe na kiangazi hali kadhalika na sisi Binadam tuna pitia nyakati tofautitofauti katika maisha yetu kuna nyakati za kufurahia maisha na kuna nyakati za huzuni, shida, dhiki, na matatizo.
Na mapito yote haya ndio hutufunza na kutuimarisha kiakili na kiimani, pia ndio huleta ile ladha na maana halisi ya maisha.

Hivyo ni wapumbavu tu ndio wanaodhani wao wameumbiwa upande mzuri pekee wa maisha ila shida, dhiki, matatizo na changamoto za maisha wao haziwahusu.
 
Asante
 
Back
Top Bottom