Sep 17, 2021
39
84
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Kwanza pongezi sana kwa kila anayetamani Katiba Mpya kwa sababu nia ya Rais Samia Suluhu kutekeleza nia yake inaonekana wazi. Kwenye Bunge lijalo la Bajeti, Wizara ya Katiba na Sheria inaenda kuomba pesa kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya. Ni wazi 'Mama' anakwenda kufufua mchakato huo kabla ya 2025.

Hata hivyo kwa sasa, tunamhitaji zaidi MAMA kuliko Katiba Mpya yenyewe. Naomba nieleweke.

Tunachohitaji kwa sasa ni utashi wa kisiasa na utayari kiongozi. Katiba Mpya haijitengenezi, ndio maana kabla ya Rais Samia hata kutaja Katiba mpya ilikuwa inatisha, ila yeye karuhusu. Tunamuhitaji yeye kwa sasa kuliko hata hiyo katiba Mpya, bila yeye hakuna Katiba Mpya.

Pia tunamhitaji Rais Samia kwa sababu yeye anatoa suluhu kwa matatizo ya msingi ya nchi. Anaboresha elimu, maji, afya na mengi ya msingi. Katika miaka yake miwili tumeona mambo yote haya yakifanikiwa.

Unaweza kuwa na Katiba mpya ila kama Rais sio mtu wa kuendana na upya huo itakuwa kazi bure. Kenya wana katiba mpya ila hawaachi kulia kila siku.

Tumuunge mkono Mama, tumuunge mkono kama wanavyofanya CHADEMA, ACT na wengine.

#MamaAnafanikisha
 
Mimi nikishasikia mtu anamwita huyu raisi wenu MAMA tu yatari najua hana akili sawa sawa.

Maana kwanza hatuna cheo cha mama kwenye katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na hata kwenye sheria za uongozi wa inchi sidhani kama kuna hicho cheo serikalini.

Sasa sijui shida ni kutokunyonyeshwa vizuri wakati wa utotoni ndio kuna sababisha watu kuwa na utindio wa ubongo kama wewe mleta uzi au labda ndio watu ambao wakiwa watoto wanapitia ile hali wanaita kubembendwa ndio wanakuwa na shida kama hii tunayoiona hapa.

Anyways, uwe serious na maisha achana na ushabiki wa kisiasa hautakusaidia lolote.
 
Kuna watu mnakera mpaka basi. Tanzania ya sasa inahitaji taasisi imara, na siyo wanasiasa miungu watu wa kujisifia kumiliki chawa.
 
Wananchi hawataki jina wala chama cha kuwaongoza wanachohitaji ni uongozi mzuri sio kupelekwa pelekwe kama vitunguu sokoni sio wananchi wote hawana akili ya uelewa kwamba sasa hiv wanaongozwa vibaya
 
Back
Top Bottom