Kwa sasa Tanzania baada ya John Magufuli, basi ni Profesa Palamagamba Kabudi

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI, ANAKAA KWENYE MZANI MMOJA NA DAKTARI NAMDI AZIKIWE, KWAME NKRUMAH, JULIUS NYERERE, W.E.B.DUBOIS, GEORGE PADMORE, MARCUS GARVEY, PATRICE LUMUMBA NA JOHN MAGUFULI.

Leo 14:35hrs 22/11/2020

Awa ni Viongozi Mashuhuri waliobeba wazo turufu la Pan Africanism mioyoni mwao,Pan Africanism ni chimbuko la harakati za ukombozi wa mtu mweusi lililowasha moto wa ukombozi kwa Nchi za kiafrika,Pan Africanism ilileta Viongozi kama Dk. Namdi Azikiwe wa Nigeria na Julius Nyerere wa Tanzania ambao ushawishi wao haukuwa kwa Nigeria au Tanzania tu, bali Afrika nzima,Dk. Kwame Nkrumah wa Ghana ambaye aliiletea Afrika dhana ya “vyama vya umma” Mass Parties kwa pamoja waliwasha moto wa “Pan Africanism” kwa Afrika nzima na harakati za kudai uhuru kutoka kwa Wakoloni.

Filosofia ya “Pan-Africanism” kama ilivyobuniwa na Daktari W.E.B. Du Bois, ilikuwa juu ya “nguvu ya kisiasa na heshima ya mtu mweusi ulimwenguni kote”. Kwa Daktari W.E.B. Du Bois na wenzake, heshima ya mtu mweusi ilimaanisha “heshima ya watu wote wenye asili ya Kiafrika”. Na kwa masaibu aliyoonja chini ya mfumo wa utumwa nchini Marekani, yenye kudhalilisha mtumwa na mmiliki wa mtumwa kwa pamoja, ambapo mtumwa alikuwa mtu mweusi na mwenye kumiliki mtumwa, mweupe; alifikia uamuzi kwamba dharau hii ingekoma kama Afrika ingekuwa huru.

-Je tunaukumbuka Wimbo huu tulioimba enzi za Mwalimu Nyerere!?

"Afrika nakutamani sana, nikikumbuka sifa zako;

Utumwa ni kitu kibaya sana, tuliuzwa kama samaki;

Samaki wa kwetu wanono, nakukumbuka Afrika”.

Wengi hatukujua kwamba maneno ya wimbo huo yaliwakilisha kilio na maombolezo ya mtu mweusi aliyeuzwa utumwani huko Marekani, Visiwa vya Ki-Karibian Caribbean Islands,na vya Uhindi Magharibi West Indies na Uingereza kabla ya karne ya 19, pale biashara ya utumwa,biashara ya kudhalilisha na kutweza utu wetu ilipopigwa marufuku ulimwenguni kote,Leo Wazungu wamekuja na aina nyingine ya utumwa,utumwa mkopo, kudharirisha utu wetu, shukrani kwa maneno haya,Kati ya Pesa na heshima ya Nchi yetu,tutasimamia heshima ya Nchi yetu,kati ya misaada na utu,wetu tutasimamia utu wetu,hatutakubali kudharauliwa utu wetu na kutoheshimiwa kutokana na misaada", maneno haya yamenikumbusha Pan Africanism.

Kwa Tundu Lissu,Zitto Kabwe pengine na kwa Fatma Karuma wenye kutamani wazungu watutawale tena mimi naona hawana taarifa kamili kuhusu kutawaliwa na wazungu,hawana taarifa kamili ya kwamba wazungu walikuja Afrika kuanzisha makazi Ila walishindwa, shukrani kwa Babu zetu,natamani Tundu Lissu,Zitto Kabwe,Fatma Karuma wapewe taarifa za kweli kuhusu Afrika kwa mara nyingine Afrika tupewe elimu yetu iliyofungiwa kwenye nchi zao tupewe historia yetu tuambiwe namna gani Afrika ilitawala dunia namna gani wazungu walifundishwa ustaarabu na waafrika namna gani Chuo Kikuu cha kwamza duniani kilikuwa Afrika,kilifundisha watu wote duniani na namna gani afrika ilikuwa Mfalme wa matibabu na madawa,

Waafrika tuwaenzi wakubwa zetu kina Marcus Garvey, George Padmore,Kwame Nkrumah,Nnamdi Azikiwe,Julius Nyerere kwa kulinda utu wetu,tufungue akili,hakuna atakae kuja kutuokoa hapa leo,hivi leo Trump amekataa Ushindi wa Joe Biden,kwa nini Marekani isiingie mahakama ya kimataifa kama Raisi wao ana force hivyo ila ingekuwa Afrika ni shidaa wengine wange pelekana huko ni tatizo hilo,Africa tuwe na mfumo mzuri wa siasa zetu ikiwezekana uchumi na hata kitaaluma haiwezekani mpaka leo unasoma kuhusu dutch impact kwa south Africa for what and for who na ina saidia nini tukianza kuwapa ukweli watoto wa 2020 yaani watoto wote chini ya miaka 5 waambiwe ukweli kuwa ifikapo 2025 SGR itakuwa imeisha,Ndege zote zitakuwa zimenunuli,Bwawa la Stigglers Gorge litakuwa limeisha,tutakusanya zaidi ya trillioni 4 kwa mwezi,na hatutakuwa na Miradi mikubwa ya kutumia hela zetu nyingi kama sasa tunapoangaika na Ujenzi wa miradi hiyo mikubwa, ikifika mwaka 2040 hadi 2060 tuna kizazi ambacho kinajua ukweli juu ya Africa,leo msomi ndio bullet proof ya mfumo wa mzungu inasikitisha sanaa,

Kwa sasa hapa Tanzania,baada ya John Magufuli,basi ni Profesa Palamagamba Kabudi pekee anayeendelea kutambua umuhimu wa maono ya Pan-Africanism na Tanzania tulitumia nguvu zetu zote na rasilimali zetu kusaidia Ukombozi wa Afrika na baadaye katika kuanzisha OAU mwaka 1963, kama hatua ya kwanza kuelekea Serikali moja ya Shirikisho la Afrika,mawazo ya Profesa Kabudi yanaendana na mawazo ya Nnandi Azikiwe,Kwame Nkrumah,Julius Nyerere katika kuupiga vita uonevu na utumwa wa kutweza utu wetu,mawazo ya uzoefu, ujasiri, ari na mtizamo wa kimapambano wa mtu mweusi,maono mapana juu ya nafasi ya Afrika katika dunia ya sasa, mawazo ya ujasiri kwa fikra na kwa vitendo,Profesa Kabudi analenga mambo makuu kwa matarajio makubwa akifikiri kwa msingi wa bara zima la Afrika,kwa mtizamo wa Pan Africanism,Mashujaa wote wa kiafrika waliongozwa na fikra na siasa za mrengo wa Ki-Karl Marx, fikra za kimapinduzi.

Nimalizie kwa kusema,wao wamelalamika kwenye media kuhusu 'msaada' wao,nasi tumewajibu kupitia media kwamba tukosoane kwa heshima kila upande una mapungufu yake,kamwe tusingewaacha watoa 'misaada' waseme na kufanya wanachotaka bila kuguswa,enzi za ukoloni za kumwacha 'bwana mkubwa' akuendeshe anavyotaka umepita,huu ni ulimwengu wa partnership na mutual respect,ba hii tabia ya kuogopa kwamba 'misaada' ikisitishwa tutakufa ndiyo inaifanya Afrika iendelee kubaki masikini. Bila kuchukua hatua madhubuti, tena kwa maumivu makubwa, kujiendeleza sisi wenyewe tutabaki kutawaliwa milele.

Afrika tuna kila kitu lakini kwa nini bado tunaendekeza misaada?
Hao Mabeberu wanaitegemea Afrika kuendesha viwanda vyao na vyakula toka barani Afrika, mbona hatujiamini?
Ata wasipotoa misaada lazima waje tu hata kwa mfumo mwingine wa kibiashara na bado dola zao tutazipata tu,Rais John Magufuli kaonesha kabisa kujiamini na inabidi hata wengine tujiamini na tulicho nacho,kwa sasa Rais John Magufuli anajenga miradi mingi kwa fedha za kodi ya Watanzania na si pesa za Mabeberu,kwa hili tu tunapaswa kutembea kifua mbele,ifikapo 2025 baada ya miradi yote kukamilika basi tutakusanya trillioni 4 kwa mwezi,na utegemezi kwa Mabeberu utakuwa umeisha,tutembee kifua mbele,
Sisi tuna rasilimali kibao na wakisusia Western tutafanya biashara na Mchina ambae yupo tayari muda wowote,saa yoyote.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
JIWE ASINGEKUWA AMEZUIA UTEUZI NINGEKUPIGIA DEBE AKUTEUE.
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master of Leadership and Management.

WAZUNGU KUULIZIA HELA YAO MMEFANYIA NINI MNASHINDWA KUJIBU MATUMIZI YA FEDHA BADALA YAKE MNAJIKITA KUANDIKA UPUMBAVU KABISA.

SHAME ON U
 
Ni bora kurudi utumwani kuliko kuendelea na haya tuliyo yaona kwenye uchaguzi yakifanywe na mtu mweusi tena ndugu wa damu,uongozi haupo maalumu kwa kudi fulani katiba yetu inaruhusu mwenye sifa kuomba ridhaa na akichaguliwa na awe,falisafa ya pan africanism haikuwa waafrika tuumizane na kudhalilisha sisi wenyewe kwa wenyewe,haiwezekani mtu kwenye uchaguzi anashinda kihalali unampora ushindi wake kwa kuingiza kura bandia, tulipo Kama taifa ni bora mzungu arudi kututawala.
 
Naona mnatekenyana
emoji1.png
emoji1.png
sawa sawa kweli beberu kawakuna vizuri nikulia lia tu hapa
 
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo mnakwepa kuzijibu badala yake mnajikitabkwenye UZALENDO WA KIPUMBAVU.

1.Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo?
2. Je, vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi?
3. Je, watu hawakukamatwa?
4. Je, hakuna walioripotiwa kuuawa?
5. Je, hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

ACHENI UZWAZWA HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SI UZALENDO WA KISHAMBA.
 
Umeandika sana lakini hoja ya msingi ni je, tulichukua pesa za Corona au wametusingizia? Kama tulichukua, zimefanya kazi gani wakati kwetu Corona haipo?
 
Hivi ulikuwa wapi wewe hukumsikia papa wemba alisema Atahakikisha watu kama Kabudi na yule mwingine nani oh na wengine wa umri kama wake, kamwe hawaingii katika ufalme wa mbiguni?. hujasikia eti ok sasa futa bandiko haraka au badilisha wa kumpigia debe fasta au futa uzi umesha expire
 
Haya matamko ya kibabe ndiyo yanadhihurisha uminywaji wa demokrasia Tanzania maana hawataki kuingiliwa mambo yao ya ndani eti.
 
Kikundi kidogo kimegeuza wananchi walio wengi kuwa daraja la chini, yaani watumwa, ambao hawatakiwi kuchukuwa madaraka hata wakishinda uchaguzi kwa sanduku la kura. Afu unakuja hapa na ngonjera za Pan Africanism!!!
Pathetic.

Hao magwiji wa zamani uliotaja hawakuwa na ulimbukeni huo
 
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo mnakwepa kuzijibu badala yake mnajikitabkwenye UZALENDO WA KIPUMBAVU.

1.Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo?
2. Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi?
3. Je, watu hawakukamatwa?
4. Je hakuna walioripotiwa kuuawa?
5. Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

ACHENI UZWAZWA HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SI UZALENDO WA KISHAMBA.

Ebu kaulize Je Rais Putin wa superpower imekuje kakubalika kuongeza nchi hiyo mpaka 2034??? Pili kavamia kijeshi sehemu ya nchi jirani Crimea kipande cha Ukraine kwa sababu ni mzungu hamsemi mnazungumza ya Tanzania nchi ya amani! Polisi kule hawafanyi kazi au hakuna
vyama vya upinzani?
 
Mimi nimeelewa swala Moja tu kwa mleta mada.
Amejaribu kutamka falsafa yake.
Pili akaweka na CV yake. Na dhani Kwa ufupi.

Ila sijaona Jambo jengine.
Isipokua Nina wasiwasi tu kama je Hiyo falsafa anaiamini kweli au Ni Tapeli tu.
 
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo mnakwepa kuzijibu badala yake mnajikitabkwenye UZALENDO WA KIPUMBAVU.

1.Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo?
2. Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi?
3. Je, watu hawakukamatwa?
4. Je hakuna walioripotiwa kuuawa?
5. Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.

ACHENI UZWAZWA HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SI UZALENDO WA KISHAMBA.
tayar simu yako imejaa mkuu😂😂😂😂😂 naona umeacha mavi yako tayari😂😂😂🛫
 
Ebu kaulize Je Rais Putin wa superpower imekuje kakubalika kuongeza nchi hiyo mpaka 2034??? Pili kavamia kijeshi sehemu ya nchi jirani Crimea kipande cha Ukraine kwa sababu ni mzungu hamsemi mnazungumza ya Tanzania nchi ya amani! Polisi kule hawafanyi kazi au hakuna
vyama vya upinzani?
Jikite kwny mada.. Hapa tunaongelea Tanzania. Hiyo hoja yako inafaa kule "International Forum"
 
Nimeupenda sana uchambuzi wako kiongozi. Nilikuwa ninashawishika kuungana na uchambuzi wako, LAKINI Baada ya kurejea hotuba ya Mh Rais alipokuwa akimuapisha Waziri Mkuu na Mawaziri wa Mambo ya nje na Waziri wa fedha alisema watu Kama akina Lukuvi wasiote kugombea kwa kuwa 2025 ni awamu ya vijana. Je Palamagamba anaingia kwenye vijana?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom