Kwa sasa kuwekeza Tanzania ni sawa na kucheza kamari?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,124
Hali ya sintofahamu imezidi kutanda katika sekta binafsi hapa nchini Tanzania baada ya Baadhi ya Makampuni makubwa(Kama Dangote Cement) na madogo kufunga biashara, kupunguza mtaji, kutangaza kupata hasara au Kupungua kwa faida, huku sababu hasa zikisemwa kuwa ni...

1/Mabadiliko ya kisera yasiyoweza kutabilika.

2/Mifumo ya ukusanyaji kodi.

3/Misukumo ya Kisiasa katika utendaji.

4/Mzunguko mdogo wa Kipesa.
 
You're only guaranteed if and only iff a president you signed with still holds power, that's to say only ten years
 
Kama kuna mtu anaamini kujenga uchumi wa nchi ni kama kujenga nyumba yako binafsi kwamba inabidi uivunje yote kisha ujenge mpya atakuwa looser. Kuna watu wataona aibu kurudi kwa wananchi 2020.
 
Du wee kada ndo hasira? Kwanini matusi? Mchezo huu haitaki hasira
 
Kuwekeza Tanzania ni sawa na kusaidia watoto wa mitaani kwa kuwapa mavazi na kuwanunulia Chakula ukitegemea wakikua watakulipa hela yako
 
Wabongo bana!
Wawekezaji walipokuwa wanapewa Incentive Kama vile

1. Tax holiday
2. Sera Rafiki kwao za uwekezaji Kama vile kupewa rasilimali kwa Bei rahisi
Tulikuwa tunaponda na kukejeli kuwa inakuaje Mgeni atapewa kipaumbele

Sasa Magu kakaza wanaanza kukimbia tunalaumu

Jakaya alikuwa radhi kufanya Ziara hata Kama kaalikwa na Taasisi zisizo za Kiserikal tukawa tunatupia Picha kumkashif kuwa anashusha heshma cheo sasa Magu kakaza hataki kusafiri na hata kwny Gogoro la Dangote hajakutana private na Dangote kumsikiliza wakati Jk Muda Kama huu angeshamwita Ikulu
 
Bora hata kucheza kamari angalau mara moja nawe unaweza ukawala, kuwekeza Tanzania sasa hivi katika mazingira ya hii Serikali ni kupoteza pesa zako tu.

Hali ya sintofahamu imezidi kutanda katika sekta binafsi hapa nchini Tanzania baada ya Baadhi ya Makampuni makubwa(Kama Dangote Cement) na madogo kufunga biashara, kupunguza mtaji, kutangaza kupata hasara au Kupungua kwa faida, huku sababu hasa zikisemwa kuwa ni...

1/Mabadiliko ya kisera yasiyoweza kutabilika.

2/Mifumo ya ukusanyaji kodi.

3/Misukumo ya Kisiasa katika utendaji.

4/Mzunguko mdogo wa Kipesa.
 
Back
Top Bottom