Kwa sasa Kilimanjaro ndio sehemu bora ya kuishi kabisa hapa Tanzania

Kwa sasa Moshi ndo sehemu bora kabisa ya kuishi hapa Tz pana viwango vyote vinavyopaswa


Hapa nazungumzia Moshi kuanzia Rombo hadi Siha kule Sanya juu


Maeneo yenye huduma zote za kijamii za uhakika

Maji ya kutosha


Shule za kutosha


Hospital za kutosha


Barabara nzuri kama upo ulaya


Hali ya hewa nzuri kama upo Ulaya flan hivi amaizing


Vyakula vya uhakika food security ipo ya kutosha hakunaga njaa huku


Mazingira mazuri kwa kilimo cha kisasa cha greenhouse na ufugaji wa kisasa


Hali ya hewa nzuri


Utulivu wa moyo pako cool sana


Maisha mazuri ya kibepari hakunaga kufatiliana....kila mtu na maisha yake huku hakunaga kuvunja nazi njiani au kijicho au mambo ya uganga na majini hakunaga


Maduka ya kutosha huduma zipo zote mabenk, maduka makubwa masoko etc...


Ulinzi na usalama wa uhakika huku viwango vya uhalifu ni kidogo mnooo maisha yanaenda kwa amani


Sehemu nzuri ya kumuabudu mungu ndo maana wachaga ukimkuta kashika dini kashika kweli kweli maana nyumba za ibada na mazingira ni mazuri na yanafaa sana.


Kwa hoja hizi zote Kilimanjaro ndo eneo bora kabisa Tz nzima na East Africa kwa kwa kuishi na ustawi wa mwanadamu...
mvua ikinyesha tope lake si mchezo kuna siku tulikua na v8 na ilichemsha ilo tope
 
Namkosoa mtoa mada kwa haya yaliyomo kilimanjaro kwanza :
✍ moshi sio kote kunafaa kuishi sehemu kama

pasua, njoro, oysterbay, shabaha, new land, majengo, rau, getifonga, tpc, mijohoroni, kiboloroni, shiri mgungani, weruweru ya chini uswahilini na mbuyuni, magomeni, na huko kahe chekereni nanilipo pasahau,.

Niseme tu ukweli huko ni pakawaida na kuna taabu kama sehemu nyingine Tanzania, kwanza kuna ukora, uchokoraa, uswahili upo, kufuatiliana, mbanano wa nyumba za kupanga na hadha nyingine kama ujambazi, utapeli na ukabaji, watu huko ni hali ngumu na vumbi kama lote.

✍Sasa Uzuri wa baadhi ya kilimanjaro ni Machame, Kibosho, Rombo, Moshi ya Shanty town na KCMC via Usharika wa neema, Soweto area mpaka St. Joseph hospital, Sanya Juu, Marangu, Mbokomu ya kirua Vunjo pia japo kuna physical difficulties kama kwa wapare ugweno yaan milima kama yote afu no miundo mbinu sema kote ni uchaggani.
Changamoto ya hayo maeneo yamekaliwa na wachagga pekee, alafu kuishi huko kama wewe sio mwenzetu lazima utapata shida labda uje kama mfanyakazi wa nyumbani au msaidizi wa mifugo 😅😅 sijui kwa nini wale wa mama na wababa wakichagga walio soma wako kama wahindi hadi shape 🤣🤣 ukija mgeni unataka uhuru wa kuishi hayo hapo juu ndio favourable residences for you...

✍Maeneo ya uchira, sango na kawawa mpaka njia panda panakuwa miaka hii ya 20's kama ilivo miji ya dodoma, wachagga tuliitaga zamani ni poroni, waliozaliwa huku ni chasaka yaani ni wachagga koko 😅😅

Kwa hiyo mkuu habari ndiyo hiyo mtoa mada usije siku moja ukaona moshi pazuri mi ni mzawa na mwenyeji lakini nasema hivi moshi mpaka sasa pamechoka hapangestahili pawe hivi miaka hii 7 iliyopita pako vile vile tangu awamu ya kwanza ya J.K.

ndio maana Jamaa kwenye kampeni akasema Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla bado sana. Alisema Moshi mmechelewa na ni kwelii 🤣🤣🤣 pangetakiwa pawe half lond na arusha hivo hivo mpaka kushuka hiyo Tanga ya lushoto na Babati pia.

Asante mkuu nimetoa yangu kuhusu kilimanjaro.
 
Umeanza vizuri kuitaja Kilimanjaro kama mkoa kwenye heading, lakini umekuja kutaja Moshi ukisema kuanzia Rombo hadi Siha Sanya juu hapo si kweli. Moshi ni Wilaya na mji. Rombo ni Wilaya, Hai ni wilaya, Siha ni Wilaya, Mwanga ni Wilaya na Same ni Wilaya. Moshi unayotaka kuielezea inaanzia Himo hadi Maili Sita. Maili Sita ndipo mwanzo wa wilaya ya Hai.
Moshi mjini pabovu kabisa, shanty, kcmc na soweto tu ndio kuzuri
 
Back
Top Bottom