Elections 2010 Kwa sasa kheri zimwi lisilonijua!

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,751
7,535
Nimekuwa nikifanya kazi za maendeleo ya jamii katika miji mikuwa na midogo; vijiji vikubwa na vidogo. Nimeona maeneo katika vijiji vidogo na vikubwa ambako mpaka leo kuna watoto wanakenda shule bila viatu kabisa.

Hivi karibuni nimesikia kupiti vyombo vya habari kuwa, miaka baada ya uhuru wa mtanganyika, bado hata katika miji mikubwa kuna watoto ambao hadi leo wanakwenda shule bila viatu. Baba yangu asiye mtembeaji kama mimi anaweza kufikiri miaka ya 47 alipokuwa akisoma yeye haya yalikuwa ya kawaida. Miaka 49 baada ya uhuru maisha bora kwa kila mtanzania yanabakia kuwa ndoto.

Maisha bora kwa kila mtanzania bado yanawezekana? Mimi nasema bila kigugumizi ndiyo. Watanzania wenzangu inatupasa mwezi October tuchague zimwi lisilotujua kwa maanahili litujualo, kinyume na imani za wahenga, lina tula na tukilipa nafazi ya miaka mitano zaidi litatumaliza. Kwa sababu ya hali tete ya kisiasa na uchumi nchini wengi wamediriki kusema kuwa hawaoni sababu ya kupiga kura! Mimi nasema, kura ndiyo sauti pekee na fimbo aliyo nayo mnyonge kama mimi na watanzania walio wengi. Nawatia moyo watanzania wenzangu tuitumie vema fimbo hii tulichape ziwi na kuliondosha kabisa.

Maisha bora kwa kila mtazania yanawezekana; Mimi nashauri: tulijaribu zimwi lisilotujua! heri hilo kuliko hili! Mungu ibariki Tanzania

icon14.gif
 
Kwanza nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana kwamba ifike mahali tukubali mabadiliko bila kujali yatakuwa na faida au hasara kiasi gani. Lakini ni dhahiri kwamba CCM watamsimamisha JK. Hapo zimwi lisilokujua atabaki kuwa Lipumba. Kama kwa zaidi ya mara tatu anaendelea kugombea, na hayupo tayari kumwachia na mwingine agombee ndani ya CUF, ataweza kuwa kiongozi mzuri kweli? Si kwamba ana uchu wa madaraka? Kitendo chake cha kuchukua form tena mwaka huu kimenifanya nimwondoe kabisa katika idadi ya viongozi wa kutegemewa nchini. Labda tusubiri hilo zimwi lisilotujua kutoka CHADEMA.
 
Back
Top Bottom