Kwa sababu hizi sisi sote ni wezi,sasa mwisho wake nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa sababu hizi sisi sote ni wezi,sasa mwisho wake nini??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zamazamani, Sep 1, 2010.

 1. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  JAMANI
  Najua hili neno 'WEZI' litaleta mtafaruku lakini huo ni unafiki mtupu ...Nimekuwa nikijiuliza,asilimia kubwa ya wabongo ,tuchukulie mfano wafanyakazi wa serikali ukiwauliza kuhusu maisha watakuambia maisha magumu na mshahara hautoshi...lakini nyumba anazo ,magari,bia kila siku kama kawaida,fujo za mjini karibu kila siku kujichanganya nk....pamoja na hayo,watoto wanakwenda shule English Medium ambazo zipo very expensive,..ndugu kibao wa kuwaaangalia,anapiga pamba za uhakika na za familia,,..ku take care ya nyumba ndogo kama kawaida,..ukikutana na mtu huyu mtaani atakwambia aah nipo kwenye mishemishe bwana ..au bila ya mishemishe hauwezi kuishi hapa town,si unajua ukisubiri mshahara mwisho wa mwezi utaadhirika hapa mjini.....sasa hizo mishemishe ni kitu gani kama siyo timing ya wizi???...........
  Kwa wanasiasa hali ni kama hiyo...kampeni (kama zinazoendelea) mtu anatumia zaidi ya milioni 100 ...hizi zitarudije?? na ata maintain vipi status???..Hali kadhalika kwenye nyanja ya sekta binafsi...watu wanafanya mambo kama hayo...Vilevile katika Level ya uongozi wa juu,wenye madaraka nao sina haja ya kuwaongelea hapa....
  Sasa nimefikiri nikaona kwamba kwa kweli hakuna wa kumlaumu kwamba ni mwizi wa EPA ,Bank fulani etc ,sisi karibu wote ni wezi ila tu inategemea na nafasi uliyonayo,timing, na watu waliokuzunguka nk ..ukimchukua yule niliyemzungumzia hapo juu ,ukampa mchongo kama wa EPA atauacha?? au wewe msomaji sema kutoka rohoni kila siku kuna michongo mingapi unakimbiza mingine ina bounce na mingine ndio inakuweka mjini???lakini ukiangalia kwa undani ni kwamba umedanganya,au umemzidi mtu akili,au umemuwahi mtu,umechomeka,umekula rushwa nk...Haya ndiyo maisha yetu ya kila siku jamani..nafikiri ni mfumo wa maisha ndiyo unatufanya tuwe wezi...Sasa tufanyaje ili tuache au ndio mwendo huu mpaka mwisho???nawasilisha jamvini
   
Loading...