Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

Kweli kabisa elimu juu ya ufahamu wa ndoa yenyewe na yaliyopo katika ndoa bado inahitajika kwani kwa miaka ya sasa hivi watu wanaingia kwenye ndoa kwa matarajio ya kukuta vitu fulani ambapo mwisho wa siku wakiingia wanakuta ni kinyume chake hivyo kuzifanya zisiwe zenye kudumu.
 
> Uelewa finyu juu ya NDOA......
Nimeona ndoa nyingi za vijana zikivunjika na nyingi kukosa amani na furaha.....lakini ukiwasikiliza malalamiko yao.....utagundua kuwa wana uelewa mdogo sana wa jambo hilo.....na ndio maana wanashindwa kuwajibika nalo.....misukumo inayowafanya waingie kwenye ndoa ni ya kijinga sana.....ambapo naweza kusema kuwa ni ya kitoto.....
mkuu naomba uje uongelee hili swala kwa undani .. hayo mengine yatafuata ... tukiweza hapo mengine nadhani yatakuwa mepesi.. asante sana mtani barikiwa sikukuu njema
 
hizi POINTS nimezipenda sana

>UONGO & USIRI
>ELIMU FINYU YA NDOA
>FIRKA HASI

hizo ndio ugonjwa mkuu unaoshambulia hadi Ini la Ndoa..

Yaani tena hizo mbili.. ya juu na ya chini sio ndoa tu hata Urafiki wa kawaida haudumu kabisa kila siku utakuwa unabadilisha marafiki
 
Habari za muda huu wapendwa......bila shaka Mungu katujaalia uzima.....na wenye maradhi Mungu awajaalie afya njema.....

Kwa kawaida Ndoa ni tukio lenye furaha sana....lakini kwa bahati mbaya imekuwa sio furaha yenye kudumu......ambapo mwisho wake huwa ni majuto ya kwanini niliamua kuoa au kuolewa.......

Sababu hizi zinaweza kuwa chanzo cha migogoro au kuvunjika kwa ndoa nyingi sana....au mahusiano.....

>Matarajio yaliyopitiliza.....
Kwa kawaida kila mmoja wetu hutazamia mambo makubwa kutoka kwa mwenzie....katika mahusiano......matarajio hayo wakati mwingine hupitiliza na hata kumuona mwenza wake kama malaika.........matarajio yaliyopitiliza kwenye mahusiano yanaweza kukufanya ukakosa amani na kushindwa kulifurahia pendo......

> Fikra HASI juu ya mwenzio.....
Kawaida mahusiano yenye furaha na amani hayaji automatically bali hujengwa.....unapokuwa na fikra hasi au na wasi wasi juu ya mienendo ya mwenzio.....na ukaamua kukaa kimya juu ya hilo ni wazi kuwa badala ya kujenga.....unabomoa utamu wa penzi lako wewe mwenyewe....kwa hisia zako mbaya.......inawezekana unavyowaza sivyo ambavyo mwenzio alivyo......

Vile vile kati yenu hakuna mkamilifu....kwa hiyo kukosea au kutoka nje ya mstari ni mambo ya kawaida....ambayo yanawezekana kuwekwa sawa kwa maongezi tu ya kawaida kwa wapendanao.....

> Usiri uliopitiliza......
Ni ajabu kuona kuwa wapenzi wa siku hizi wanaweza wakaishi hata miaka mitano....lakini bado wakawa hawafahamiani kabisa....hii inatokana na ukweli.....kuwa wanandoa wengi hawapo huru......wanafichana mambo mengi sana.......hata yale ambayo ni ya kawaida kabisa......mwisho mambo yatakapoanza kujulikana hadharani.....inashusha kiwango cha uaminifu baina yao....na hatimaye mikwaruzano isiyokwisha na ndoa kukosa amani......

Kuwa muwazi kwa mwenzio ili kuondoa mashaka kwa mwenzio......

> Hali ya kiuchumi.....
Hakuna asiyejua nguvu ya pesa kwenye mahusiano kwenye nyakati hizi......

Na bila ya shaka kuna nyakati mambo yetu kiuchumi.....huyumba.....na ndio kipindi ambapo migogoro mingi huzuka kwenye Ndoa kukosa amani.......ni kipindi UPENDO baina ya wanandoa unawekwa kwenye mizani.....kuwa uzito unaanekana wakati wa furaha ni original au ni fake.....!!!

> Uongo.......
Bila ya shaka uongo ni kitu chenye kukera sana.....lakini mwanzo unapoutumia kufanikisha mipango yako unakuwa ndio silaha kuu........
Lakini bila ya kujua kuwa silaha hiyo hiyo ndio itakayokuja kukuhukumu......

Mahusiano au ndoa iliyojengwa katika misingi ya UONGO na ulaghai....huwa haiwi imara na haishiwi na migogoro....kwani uongo hauna sifa ya kudumu bali maisha yake ni mafupi sana.....

Kuishi ndani ya dimbwi la uongo ni kazi....kwa kuwa tangu siku utakayoongopa ndipo utakapoanza vita ya kuulinda uongo.....hakika ni maisha ya mashaka sana...kama sio ya wasi wasi......
DAIMA UKWELI UTAKUWEKA HURU........
Sema kweli japo inauma......

>Kutokutimiza wajibu...
Kama nilivyosema kuwa ndoa imara au mahusiano mazuri hujengwa wenyewe waliopo kwenye mahusiano....na wanaobomoa ndoa ni wanandoa wenyewe....
Lakini pia ndoa imara inajengwa na kila mwanandoa kutimiza wajibu wake kwenye ndoa.......

Kama dhumuni la ndoa ni kuwa na furaha na kuleta amani basi kila mmoja wetu na apiganie hilo....kwa nafasi yake.....na sio kutegemea mwenzio akutimizie hilo.....kama wewe una haki ya kupata furaha kwenye ndoa....basi vile vile una wajibu wa kuhangaikia furaha.....hiyo.....

> Uelewa finyu juu ya NDOA......
Nimeona ndoa nyingi za vijana zikivunjika na nyingi kukosa amani na furaha.....lakini ukiwasikiliza malalamiko yao.....utagundua kuwa wana uelewa mdogo sana wa jambo hilo.....na ndio maana wanashindwa kuwajibika nalo.....misukumo inayowafanya waingie kwenye ndoa ni ya kijinga sana.....ambapo naweza kusema kuwa ni ya kitoto.....

Hivyo ni vyema vijana wakajitahidi kupata habari na taarifa juu ya jambo hilo....kabla ya kuliendea......


Kwa leo ngoja niishie hapa....

Nawasilisha......
mkuu huwa hukoseagi...nimejifunza kitu apa kwass ambao bado tunatangatanga na dunia...
 
mwanamke au mwanaume kuendelea kimapenzi na mtu ambae ameanza nae muda mrefu lakini mwisho wa siku asimuoe!akaendelea nae ijapokuwa ana ndoa au wote wako katika ndoa!kutoachana na X ndio chanzo kikubwa cha kuvuruga ndoa
 
Back
Top Bottom