Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Wasaalam hapa JF!
Kumekuwa na lawama nyingi sana kuhusu Mh Rais kutokuhudhuria physically tukio la kuaga miili ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Lucky Vicent ya Mkoani Arusha. Binafsi naona kama lawama zingine tunajitakia tu.
1. Serikali imetoa mchango wa majeneza na sanda kwa marehemu wote.
2. Serikali iliwakilishwa vyema sana na Mh Makamu wa Rais, mama Samia Suluhu Hassani, Mawaziri 5, manaibu mawaziri. Tukumbukuke hii tayari ni serikali. Mkuu wa Mkoa na safu yake nao walikuwepo mwanzo mwisho.
3. Majeshi yetu ya ulinzi na usalama yalishiriki kikamilifu kushughulikia swala hala hili mwamzo mwisho. Tumeona namna ambavyo wanajeshi wetu wa JW walivyoshiriki kikakamavu tukio hili.
4. Kuonekana kwa Mh Rais eneo la kuuaga miili pale Arusha, kungeongeza mhemko wa watu kuzimia, kuchanganyikiwa nk. Majonzi yangezidi sana kwa uwepo wa Mh Rais.
5. Rais alituma barua ya pole haraka sana mara baada ya tukio kutokea. Alionesha huzuni kubwa mno. Na pia akaunti yake ya tweeter amerudia kueleza hisia zake moyoni.
6. Kwa umati ule, kiusalama Mh Rais asingeweza kushiriki pamoja na makamu wa Rais pale uwanjani. Protocally haziruhusu kabisa.
7. Mh Rais alibaki ofsn kufanya mambo mengine ya kitaifa yaendelee. Hiyo siyo dharau kwa watanzania, yule ni binadamu mwenzetu ,hana moyo wa chuma jamani. Haiwezekani akatafsiriwa hana uchungu kwa kutokufika Arusha. Siyo kweli. Huyu ni Rais wa Wanyonge.
Tusijitakie kumlaumu Mh Rais kwa swala ambalo serikali yake imeshiriki kikamilifu.
Wasalaam.