Kwa 'Saa Za Afrika Mashariki' nadhani sentensi hii inamakosa

AG

Member
Jun 11, 2007
82
54
Jana nasikiliza redio mtangazaji anasema "sasa hivi ni saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki"
Mimi naona hapa kuna kasoro. Mtangazaji hajatofautisha kati ya Wakati Na Saa. Saa ni kipimo cha wakati, hivyo saa yangu na saa ya Mwanakijiji zote ziko sawa isipokuwa wakati wa alipo yeye na mimi si sawa. Hivyo hapa mtangazaji anatakiwa aseme "Saa mbili na nusu kwa nyakati za Afrika mashariki"
 
Jana nasikiliza redio mtangazaji anasema "sasa hivi ni saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki"
Mimi naona hapa kuna kasoro. Mtangazaji hajatofautisha kati ya Wakati Na Saa.Saa ni kipimo cha wakati, hivyo saa yangu na saa ya Mwanakijiji zote ziko sawa isipokuwa wakati wa alipo yeye na mimi si sawa. Hivyo hapa mtangazaji anatakiwa aseme "Saa mbili na nusu kwa nyakati za Afrika mashariki"

..unaonaje kama angesema "hivi sasa ni saa mbili na nusu,afrika mashariki"
 
Kwa uelewa wangu, nyakati ni kama vile Asubuhi, Mchana, Jioni, mwezi hata mwaka. Hapa unazungumzia nyakati. Lakini linapokuja suala la muda (yaani saa za wakati) ni sahihi kabisa kusema Kwa saa za Afrika mashariki. Hapa unakuwa unalenga saa za maeneo fulani tu,kwani muda umegawanyika katika kanda mbalimbali zinazotambulika kimataifa.Kwa mfano tunatambua kwamba Afrika mashariki (TZ,KN, na UG) ziko +3:00 (GMT au UTC) yaan ziko masaa matatu mbele kutoka mstari wa Greenwich au Universal Time Coordinated (UTC)(rejea jiografia yako ya sekondari).

Hivyo basi, saa mbili kamili za afrika mashariki maana yake ni kwamba, Kenya, Uganda na Tanzania ni muda uleule, lakini kwa saa bili hiyo ya Tanzania Uingereza itakuwa saa 11 jioni.

Kwa hiyo ni sawa kabisa
 
Jana nasikiliza redio mtangazaji anasema "sasa hivi ni saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki"
Mimi naona hapa kuna kasoro. Mtangazaji hajatofautisha kati ya Wakati Na Saa.Saa ni kipimo cha wakati, hivyo saa yangu na saa ya Mwanakijiji zote ziko sawa isipokuwa wakati wa alipo yeye na mimi si sawa. Hivyo hapa mtangazaji anatakiwa aseme "Saa mbili na nusu kwa nyakati za Afrika mashariki"

Nifahamuvyo ni kuwa, kuna saa 'kifaa cha kuonesha wakati' (kwa mfano, saa yangu imekatika mkanda), na saa 'majira' (kwa mfano, Alifika nyumbani saa mbili (za) usiku).

Nyakati (wingi wa wakati) hutumika kuonesha kipindi fulani, kuanzia muda fulani hadi muda mwingine. Kwa mfano, wakati wa/nyakati za masika, kipupwe, n.k.

Nadhani huyo mtangazaji alikuwa sahihi. Angeweza, vilevile, kusema: "saa mbili na nusu, kwa majira ya Afr. Mash."
 
Jana nasikiliza redio mtangazaji anasema "sasa hivi ni saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki"
Mimi naona hapa kuna kasoro. Mtangazaji hajatofautisha kati ya Wakati Na Saa.Saa ni kipimo cha wakati, hivyo saa yangu na saa ya Mwanakijiji zote ziko sawa isipokuwa wakati wa alipo yeye na mimi si sawa. Hivyo hapa mtangazaji anatakiwa aseme "Saa mbili na nusu kwa nyakati za Afrika mashariki"

Ag,
Unaweza kutafuta kamusi ya kiswahili au urudi nyuma kidogo, ujaribu kure-vise kiswahili cha kuanzia let's darasa la 12 kurudi nyuma mpaka kwenye darasa kama la tano hivi?
 
Tumekupata mkuu,sidhani kama watangazaji wanakosea kwani saa inayosemwa pale sio saa kwa maana ya clock, ni saa kwa maana ya time na athari ya tafsiri hiyo inatokana na neo East African Time ambayo ni Local Mean Time(LMT) ambayo tunatofautiana dunia nzima, labda ungependa mtangzaji kwa nyakati za africa mashariki lakini pia neno nyakati sio saa.Linaashriria kitu kingine kabisa.Kwa hiyo ni sahihi tu kusema kwa saa za afrika mashariki.Labda aseme kwa muda wa afrika mashariki, Hii ikiwa na maana kuwa hata hizo saa unazosema zipo sawa kitaalamu zimetengenezwa kwa majira tofauti na ndio maana zinarekebishwa japo zipo zinazojirekebisha zenyewe kulingana na time zone(ukanda wa muda) ulipo.
 
Ag,
Unaweza kutafuta kamusi ya kiswahili au urudi nyuma kidogo, ujaribu [B]kure-vise [/B]kiswahili cha kuanzia let's darasa la 12 kurudi nyuma mpaka kwenye darasa kama la tano hivi?

Maneno hayo hayana Kiswahili chake? Kwanini tunakoroga lugha hivi?
 
Jamani, "nyakati" ndio dudu gani tena? Kwani, "wakati" una umoja na wingi? Au ndio mambo ya waya na "nyaya?" Au moyo na "nyoyo?" Au upungufu na mapungufu? Au uhusiano na mahusiano?" Maana siku hizi Kiswahili, kila mtu anakijua kivyake!

Aulizaye, ni mwenye kutaka kujua.
 
Back
Top Bottom