Kwa rushwa ilivyotamalaki, PCCB na wengine wa hivyo wana umuhimu gani kuendelea kuwapo?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Nilileta uzi huu:

Aibu! Boda ya Rusumo Mgeni haingii nchini bila rushwa

Nimetembelea boda nyingine mkoani Kagera, kote ni mwendo mdundo! Watu wanakula kwa urefu wa kamba zao.

Hata hivyo wapi au idara ipi yenye ahueni?

Polisi? Wapelelezi, trafiki nk? Rushwa si ni sehemu ya malipo yao halali?

Kuingia polisi bure, ila kutoka. Barabarani ndiko uliko uozo halisi. Kuvunja ukimya kwa Mh. Kinana si bure.

Nani asiyejua rushwa inaendeshwaje barabarani? Kwani PCCB au wale wengine hawajui? Kwa nini hawachukui hatua zozote za kusimamisha hali hizi?

Kwani wasemapo usalama wa nchi ni upi basi? Tukidhani si ndiyo huu sasa?

Nani asiyejua rushwa zilivyo Tanesco, Tarura, tanroads, TPA, TRA, mahakamani, nk? Au hata zinavyowezeshwa?

Wananchi wa kawaida wanajua. Ila PCCB, Tiss, Polisi na wenzao walio na dhamana ya kutulinda kama serikali?

Za nini taasisi hizi au watu hawa kama hawawajibiki vilivyo na kwa mujibu wa sheria tu?
 
Jamani hebu tutoe ushuhuda humu; ni yupi miongoni mwetu amewahi kuwa sued na trafiki kwa kosa ambalo hajalitenda? Please, be honest na nafsi yako ishuhudie usemayo!
 
Hiyo ni kazi ngumu sana Rushwa ndogo ndogo inaweza kupunguzwa ila Rushwa kubwa kubwa ni vigumu sana tusidanganyane.
Ugumu hauwezi kuhalalisha bado uwepo ulaji holela kwa majina ya ku brush viatu au hata kwa ulaji wa urefu wa kamba kwa mtu au taasisi.
 
Ugumu hauwezi kuhalalisha bado uwepo ulaji holela kwa majina ya ku brush viatu au hata kwa ulaji wa urefu wa kamba kwa mtu au taasisi.
Kumbuka hii ni TANZANIA Nchi ya Kiafrika, cha muhimu ni kuangalia kwenye Rushwa Index nani anaongoza na sisi tuko namba ngapi.
 
Jamani hebu tutoe ushuhuda humu; ni yupi miongoni mwetu amewahi kuwa sued na trafiki kwa kosa ambalo hajalitenda? Please, be honest na nafsi yako ishuhudie usemayo!

Wewe hujui kuwa hao ndugu ni wala rushwa wabobezi?

Polisi lawamani, Kinana amng’ata sikio Wambura

Kwa taarifa yako hao ndugu Wana hata ratiba zilizo rasmi za kukusanya viwango vya pesa walivyowekea tokea kwenye magari ya biashara kwa wiki ili kupita salama kwenye himaya zao.

Wewe wayaona ya namna hiyo kuwa ni halali?

Wananchi wa kawaida wanayajua ila PCCB na wale wengine wote wenye dhamana ya kuyapiga hayo vita?

Kwani kuna hata cha kumung'unya maneno?

Watu hawa hawatufai!
 
Kumbuka hii ni TANZANIA Nchi ya Kiafrika, cha muhimu ni kuangalia kwenye Rushwa Index nani anaongoza na sisi tuko namba ngapi.

Kwamba ni nchi ya kiafrika? Kwani kuwa nchi ya kiafrika kuna husiana nini na mamlaka kupora haki za watu?

Kwa mamlaka kutokutulinda dhidi ya rushwa ni mwendelezo ule ule wa kutupora haki zetu za Msingi.

Kama taasisi zake hazifanyi kazi hii, ni za nini?
 
Wewe hujui kuwa hao ndugu ni wala rushwa wabobezi?

Polisi lawamani, Kinana amng’ata sikio Wambura

Kwa taarifa yako hao ndugu Wana hata ratiba zilizo rasmi za kukusanya viwango vya pesa walivyowekea tokea kwenye magari ya biashara kwa wiki ili kupita salama kwenye himaya zao.

Wewe wayaona ya namna hiyo kuwa ni halali?

Wananchi wa kawaida wanayajua ila PCCB na wale wengine wote wenye dhamana ya kuyapiga hayo vita?

Kwani kuna hata cha kumung'unya maneno?

Watu hawa hawatufai!
Mimi pale karibu na Dodoma Chamwino nimepigwa tiketi ya kuonewa ati nimeingilia msafara wakati kulikuwa hamna ishara yoyote.

Nikamlaani yule Trafiki Polisi iliniuma sana hela yangu 😤
 
Mimi pale karibu na Dodoma nimepigwa tiketi ya kuonewa ati nimeingilia msafara wakati kulukiwa hamna ishara yoyote.

Nikamlaani yule Trafiki Polisi iliniuma sana hela yangu.
Manyoni na Bahi wapo wanaosubiria kuona asiyesimama kwenye railway crossings. Zipo railway crossings ngapi uko safarini? Kwanini mbili hizi tu?

Hawa jamaa ni janga. Zao ni kutafuta visingizio tu.
 
Manyoni na Bahi wao wanaosubiria kuona asiyesimama kwenye railway crossings. Zipo railway crossings ngapi uko safarini? Kwanini mbili hizi tu?

Hawa jamaa ni janga. Zao ni kitafuta visingizio tu.
Wale huwa wanakesha wakitafuta pesa lakini afadhali wa Manyoni wa Bahi wana njaa tena mara nyingine huwa wamelewa.
 
Wale huwa wanakesha wakitafuta pesa lakini afadhali wa Manyoni wa Bahi wana njaa tena mara nyingine huwa wamelewa.
Haya wananchi wanayajua ila hao wenye dhamana walio na mishahara, marupurupu na vitendea kazi?

Ikumbukwe zaidi ya 90% ya matatizo yetu kama nchi chanzo na sababu ni kutokana na rushwa iliyo tamalaki.

Kwa vile hakuna uwajibikaji dhidi ya rushwa taasisi husika na wote wenye dhamana iwe ni mawaziri, taasisi, vyama au hata mkuu wa nchi ni muhimu kujitafakari.

Kwa hali hii ya nini kuendelea kuwapo madarakani?
 
Ukitembelea vituo vingi vya polisi utakuta tangazo mlangoni "rushwa ni adui wa haki" hivyo utajipa moyo unaenda kupata haki yako.

Lakini ukiingia ndani uanze kuhudumiwa, ndipo utagundua kumbe lile tangazo pale mlangoni halina uhalisia wowote na mentality ya polisi wenyewe, bila rushwa hupati huduma unayohitaji.
 
Mimi pale karibu na Dodoma nimepigwa tiketi ya kuonewa ati nimeingilia msafara wakati kulukiwa hamna ishara yoyote.

Nikamlaani yule Trafiki Polisi iliniuma sana hela yangu 😤
Haya mambo Tz wakati mwingine ni mambo ya police kupenda ' kujimwambafai' tu bila ulazima.... niliwahi ishi SA, msafara wa Rais unakuwa na gari mara nyingi zisizozidi 6, na unakuta mnapishana tu kwenye barabara......bila ya hata ku- cause inconvenience' kwa watumiaji wengine wa barabara ........ yaani huko mkubali tu yaishe in African way....
 
PCCB Ingefutwa kabisa tumwombe Chande na SEFUE kwemye tume yao ya kuangalia utendaji wa vyombo vya Dola hao PCCB wangesitishwa kwanza kufanya KAZI Ili tuwe uhuru kupeleka maoni ya utendaji wao kwenye tume na tukawaeleze tume jinsi PCCB ilivyokuwa ya hovyo na inavyochochea rushwa
 
Kwani huwa mnalazimishwa kutoa rushwa na polisi si unakataa wabongo bwana watu wa ajabu, mfano ukikamatwa na Trafiki si upgwe faini tu.

Sisi ndio tunakimbilia kutoa hela kwani wanachukua kwa nguvu mfukoni It begin with you. Tuungane pamoja kutokomeza vitendo vya rushwa anza wewe kukataa kutoa rushwa acheni kulalamika hovyo.
 
PCCB, NEMC TBS, zingefutwa tu wanakula mishahara for nothing
Ninakazia: "za nini taasisi hizi na wa nini wanao weka watendaji katika taasisi hizi?"

Za nini kamati za ulinzi na usalama bottom - up?
 
Back
Top Bottom