Kwa ripoti hii ya CAG, ingekuwa nchi kama China kuna watu wangenyongwa

Thadei Ole Mushi

Verified Member
Oct 13, 2018
26
100
Na Thadei Ole Mushi.

Someni Ripoti ya CAG, Kuna madudu mengi mno mengine yanatia kinyaa kabisa. Ukurasa wa 70 wa Ripoti hiyo unazungumzia issue ya Kucheleweshwa ujenzi wa kiwanda Cha Pamba kule Simiyu. Naomba kuinukuu hiyo Ripoti neno kwa neno:

"Mnamo tarehe 11 Novemba 2016 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba Tanzani (TMDA) (kabla ilikuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA)) walisaini Randama ya Makubaliano kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha vifaatiba vitokanavyo na zao la pamba katika eneo la Dutwa mkoani Bariadi.

Katika makubaliano hayo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ilikubali kutoa Ardhi kwa ajili ya kiwanda bure, MSD ilikubali kuwa mteja
mkuu wa bidhaa hizo, TMDA walikubali kutoa ushauri wa uzalishaji wa bidhaa hizo ili ziwe na ubora unaotakiwa, TBS walikubali kutoa
ushauri wa viwango vinavyohitajika ili bidhaa hizo ziwe na ubora unaotakiwa, na Benki ya Maendeleo ya TIB ilikubali kutoa ushauri
wa kifedha pamoja na mkopo wa mtaji.

Aidha, mnamo tarehe 13 Juni 2018 WCF na NHIF zilifungua kampuni inayoitwa Simiyu Medical Products Company Limited kwa ajili ya
usimamizi wa shughuli zote za uanzishaji wa kiwanda. Kufuatia Randama na Hati ya Ushirikiano ya Kampuni, mnamo tarehe 12 Juni 2019, Bodi ya usimamizi wa Kampuni hiyo iliteuliwa na Waziri wa Afya.

Aidha, nilibaini kuwa timu ya uchunguzi wa teknolojia ya kiwanda ilienda Uturuki mwezi Machi, 2019 na India na China mwezi Disemba 2019. Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi gharama za mashine pamoja na mtaji unaohitajika ni shilingi bilioni 69.2.

Aidha, kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa 19 zinazotokana na pamba. Pia, mpaka muda wa ukaguzi nilibaini jumla ya shilingi milioni 915.98 zimetumika katika maandalizi ya mwazo ya kiwanda ikiwemo kufanya upembuzi yakinifu.
Pia, kwa mujibu wa taarifa ya upembuzi yakinifu uliofanywa na TIRDO, kiwanda kitatoa jumla ya ajira za moja kwa moja zaidi ya
600 pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 1000.

Pamoja na hayo kitasaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa za hospitali kutoka nje ya nchi zinazotokana na pamba, hivyo, kusaidiakupunguza mahitaji ya fedha za kigeni.

NHIF na WCF kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto iliomba kibali cha ujenzi wa kiwanda hiki kutoka Wizara ya Fedha na Mipango mnamo tarehe 26 Juni, 2019 ila mpaka ninakamilisha ukaguzi wangu katika mashirika haya mnamo tarehe 15 Disemba 2020 kibali hicho kilikuwa bado hakijatolewa, hivyo, kibali hicho kimechelewa kutolewa kwa siku 538 toka kiombwe mpaka kufikia tarehe ya kukamilisha ukaguzi huu." MWISHO wa kunukuu......

Haya maelezo yapo kwenye Ripoti ya CAG kuanzia Ukurasa wa 70. Sasa turudi kwenye Hoja.

Faida za kujengwa kiwanda hiki ni Kubwa mno, kwa mwaka Tanzania huagiza nje ya nchi vifaa tiba vinavyotokana na Pamba vifaa vyenye Thamani ya Shilingi bilioni 79 hadi 75. Gharama za kujenga kiwanda hiki ni Shilingi bilioni 69 tu na kingeokoa bilioni 75 zingebaki hapa nchini. Fedha zipo kila kitu kimeshafanyika ni Mtu alitakiwa asaini tu pale Wizara ya Fedha lakini hakufanya hivyo.

Nani hajui kilio Cha Wakulima wa Pamba waliopo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa? Kila siku wanalia kukopwa pamba au Pamba kuozea kwenye magodown. Nani anayejali as Long as yupo kwenye kiyoyozi Cha V8? Kiwanda hiki kingefyonza Pamba yote na Wala isingetosha na Wakulima wangelikuwa wamenufaika Sana.

Tanzania ilipewa tenda ya kusambaza vifaa tiba kwenye nchi za SADC Kama kiwanda hiki kingejengwa ukiachana na Soko la ndani bado tungepata Soko Kusini mwa Africa Soko la uhakika kabisa.

CAG amesema kingetoa ajira kwa vijana wetu nk.

Nani anajali?

Cha kushangaza watu hao hao walioacha kusaini kibali Hicho bado wapo Serikalini. Hakuna aliyewajibishwa..... Ingelikuwa Mataifa ambayo yapo Serious kabisa Hawa watu walisakula Kitanzi mapema Sana. Yaani kusaini tu.

Ole Mushi
0712702602.

images (1).jpeg
 

The wave

Member
Feb 27, 2021
91
125
Huu ni uzembe wa hali ya juu, haistahili kuuvumilia. Kuna watu huko maofisini wanajiona Miungu watu.
 

Omera Yawa

JF-Expert Member
May 5, 2016
947
1,000
kutoweka maslahi ya taifa mbele ndiko kunakoturudisha nyuma, mtu anaona tukiruhusu kiwanda kujengwa, kwenye kuagiza hatutopata faida maana watu watakuwa wananunua humu humu nchini hivyo kandarasi zetu zitakufa, bora utoe milioni mia kadhaa mkataba ucheleweshwe ili tuendelee kuagiza na kuwauzia watumiaji
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
16,534
2,000
Kiwanda kingejengwa wanyonge wasingekuwepo. Sasa ingekuaje wakati yeye alisha sema ni rais wa wanyonge?
 

Said S Yande

Verified Member
Mar 16, 2013
669
500
Tatizo LA kuzuia nchi kuongozwa kitaasisi.nchi ilikuwa inaongozwa na mwendazake utazani familia he causative of all this happened
 

dumbi

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
865
1,000
Wanyongwe kama hawawezi hiyo kazi ya kunyonga watu wanipe mimi,natamani niwe nashuulikia wahalifu moyo unaniuma sana nikiona mtu anaonewa.
 

Immanuel Simon Mathew

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
501
1,000
Mambo mengine ni ya hovyo kweli! The government corporations i.e ATCL are operating at loss, then you will find that There are some few top government officials, deceiving the public that the corporations are making supper-normal profit to the government 😕😕 It Is shame of the highest order!!
 

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,574
2,000
Sasa yule mzee alikuwa anafanya nini miaka yote kazi kujisifu tu daah. Hasira sana unaenda jenga daraja la salenda unaacha kujenga KI-WONDER?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom