Kwa recent perfomance ya bandari ya Dar na projections zilizopo kuna haja ya kujenga Bagamoyo

MduduWashawasha

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
1,653
601
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia habari juu ya kushuka viwango vya mizigo bandari ya Dar ingawa wanasema mapato yamekuwa makubwa sana.

Kwa sisi tunasema kwamba inasababishwa na kushuka kwa uchumi wa china na juzi tumesikia jipya la VAT.

Ukijaribu kulinganisha bandari yetu na za jirani utaona zao ziki steady katika perfomance na Beira inaonekana iki improve siku hadi siku.

Sasa najiuliza ni Tanzania tu ndio tunategemea uchumi wa China na hawa wanaotegemea bandari yetu au kitu gani? Maane tunakosa hata transit cargo !

Sasa hii hali ikiendelea kuna haja ya kujenga huko Bagamoyo ? Labda kama atajenga investor kwa risks zake kwa mtindo wa PPT sawa lkn sidhani kama kuna investor atafanya hivyo kwa trend tuliyonayo.
 
Kwa hali ya kisiasa ya sasa y Tanzania ambayo haitabiriki yani nchi haina vision sidhani kama kuna investors mpya ambaye atakuja kuwekeza..
 
Ndiyo! Haja ya kujenga Bandari ya Bagamoyo ipo kwa sababu kinachoendelea hivi sasa bandari ya Dar es salaam si kwamba kuna mizigo ya kutosha kwenye mbandari mkuuuuubwa hadi inapwaya na kuonekana kwamba mzigo ni mdogo lakini kilichopo Bandari ya Dar es salaam ni kushuka kwa mzigo kwenye kabandari kadogo kunakotokana na poor business strategies!

Angalia hao Msumbiji ambao ni wenzetu! Maputo na Beira kote kuna mzigo wa kutosha! Angalia Angola, angalia Namibia, angalia Cameroon... hawa wote wana bandari zaidi ya moja na kote huko kuna meli za kutosha!

Angalia kufuru ya South Africa na Nigeria... huko kote kuna traffic jam ya meli!!! Hata wewe unafahamu kwamba uchumi wa Nigeria na South Africa ni wa kawaida sana ni vile tu sie wengine ni maskini wa kutupwa ndo maana wanaonekana wana uchumi mzuri! Pamoja na uchumi huo huo wa kawaida wa SA na Naija, bado uchumi huo unatakiwa kuwa accommodated na traffic ya kutosha ya meli zinazo-facilitate import and export business!

Trust me, uchumi halisi wa Mtanzania ukipanda japo kwa 20% na hivyo purchasing power kuongezeka, ile bandari ya Dar es salaam itakuwa congested bila hata kutegemea nchi zingine! Itakuwa congested kwa sababu ile bandari ni ndogo sana ambayo inaonekana ni kawaida kwavile tu ina-accommodate small economies... ya Tanzania na nchi za jirani!
 
Back
Top Bottom