Kwa Rasimu hii nani kuwa Rais kwa tiketi ya CHADEMA??

MdugeH

Member
May 25, 2013
61
23
Nimesoma Rasimu ya Katiba Mpya- 2013 hasa katika vipengele vya sifa za atakayekuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri na Naibu waziri nikajiuliza nafasi ya Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika na Sugu katika Serikali ikiwa CDM watataka kudhibiti dola mwaka 2015..!!!?? Kwani Ibara ya 75, 88 na 94 ya Rasimu ya Katiba inasema moja kati ya sifa za watajwa hapo juu ni kuwa angalau ana shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu kinachotambulika kwa mujibu wa Sheria za nchi.

NB: Naomba majibu au hoja zisizo na ushabiki wa kichama katika hili..!!
 
Ni kama vile umedandia mbele ya treni. Ngoja katiba ipitishwe kwanza. Kuna maswali mengi bado yanayohitaji majibu.
 
Ni kama vile umedandia mbele ya treni. Ngoja katiba ipitishwe kwanza. Kuna maswali mengi bado yanayohitaji majibu.
Maswali hayo ni kama hili hasa... Usikimbie moshi unaounguza ni moto..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom