Kwa Rais Magufuli huyu, Bora Mfalme wa kusikiliza maneno ya watu.

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Kuna tofauti kubwa sana bila shaka kati ya rais na mfalme, Kwa uelewa mdogo Rais anakuwa na viashiria vya kiutendaji na ufuatiliaji pamoja na kutengeza mambo yanayoharibika. Dhana ya mfalme imejiiegemeza zaidi na ubwana na kunyenyekewa, kutiiwa na majukumu ya kiutendaji kubaki kwa wasaidizi.

Kuna kisa cha Mfalme wa kusikiliza maneno ya watu, Mfalme huyu alikuwa akisikilza nini watu wanasema basi hufuata. Siku moja alikuwa amepanda punda wake/ farasi watu wakati anapita barabarani na masuria wake, wananchi wakapiga kelele kwamba farasi kachoka, mfalme akashuka ili kumuacha farasi apumzike na akawa anaendelea na safari akiwa ameshuka kwenye farasi. Baada ya muda wananchi wakalalamika kwamba mfalme mzima anatembea kwa miguu basi akampanda tena.

Hii ilikuwa tabia ya mfalame huyu. Kusikiliza na wakati mwengine kuonekana mjinga ilimradi aridhishe watu licha ya ufalme wake.

Naam, hapa kwetu tuna rais, anaitwa JPM, Rais Magufuli, Mwanzo aliitwa tinga tinga, ikafika wakati akaitwa mtukufu na asiyepingwa. Sasa sisikii tena majina haya.

Yaani nakumbuka maneno yake kuwa hatawaangusha watanzania na kwamba yeye ni mcha mungu lakini naona mambo hayako hivyo.

Kwa uoni wangu kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja na miezi kadhaa kuna mambo muhimu Rais Magufuli kayabariki na yanaharibu umoja wa klitaifa kwa mfano, Kuna undumi la kuwili katika maamuzi mbali mbali, Suala la vyeti kwa baadhi ya wafanyakazi kuchukuliwa hatua za papo kwa papo lakini kwa baadhi hawaguswi. Jambo hili ni hatari linajenga visasi na chuki. Watu wangapi wameathirika kwa maamuzi ya vyeti ilihali wengine wanaerndelea kudunda? umoja na uzalendo utakuwepo kweli ?


Kuchaguwa watu wakutumbuwa na kuachwa wengine wakiendelea kutesa na kutumia madaraka vibaya. Kuna mifano ya Waziri kuondolewa kwenye nafasi kwa tuhuma za kuingia bungeni akiwa amelewa lakini kuna wakuu wa mikoa wanaendelea kulindwa licha ya kufanya jinai ya wazi ya uvamizi na kuharibu rasilimali, Si hayo tu masakata ya kisiasa ya hujuma kwa wapinzani na viashiria vya Dola kujitumbukiza katika migogoro (CUF POLISI na Lipumba) na ikawa mpaka sasa kuna ukimya fofofo.

Hili la Polisi sasa na vyombo vya dola kutumia silaha visivyo na baadhi ya wavunja sheria kutochukuliwa hatua mifano ipo mingi.

Kwa ufupi awamu hii ya rais magufuli inaonesha kutokujali baadhi ya mambo ilimradi tu kwa upande wa serikali na chama tawala hayawaathiri. Huo ndio ukweli.

Huyu rais akumbuke ni wa watanzania wote, Akubali kushauriwa na kushaurika nchi hii sasa inakokwenda siko. Wanasiasa wanapuuzwa na kufanyiwa kila hujuma, Mahakama inanyamazia malalamiko na kule bungeni ukihoji unatulizwa watanzania weaelekee wapi ?

Nchi ina viashiria vya ukatili na chuki, watu wanajichukulia hatua mikononi mwao, kuna mauaji ya kiholela baadhi ya maeneo tena mengine yakihusishwa na vyombno vya dola. Bado serikali iko kimya na gugu la chuki likiendelea kimya kimya.

Tunasubiri nini ? au mpaka majani yakauke ndio tuamini kuwa kuna kiangazi ? Nani ASEME ILI ASIKIKE?

Rais wangu Magufuli kweli ndio wewe au moyo wangu umenidanganya ? Hakuna umoja wa kweli na uzalendo. Nina hakika kuna umoja na uzalendo wa uoga na kulazimishana.

Rais Magufuli Amka sasa. Mbegu ya chuki na visasi inaota kwa kasi sikilza sauti hii ya mnyonge.

Ni lini wale mahabusu wazee wa watu watashtakiwa wale wanaitwa masheikh wa uamsho mwaka wa nne sasa hakuna ushahidi ? ni lini mauaji kule kibiti yatakoma ? Ni lini umoja na kusafiniana nia kwa wanasiasa kutapatikana ? ni lini mgogoro wa zanzibar uliojificha utapatiwa dawa? Unasubiri kuripuke ili iweje ?


Halafu huwa najiuliza kwa nini umechagua njia hii ya migogoro na visasi kuwa ndio staili yako katika uongozi ? Watu wamekosa furaha si wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara, wanasiasa, wasomi, wala malofa.


Ulisema unanyoosha sio ? nani ananyooshwa au ulikusudia kutukomoa ? mbona hatuoni ishara njema hadi leo bdala ya kunyooka ndio kwanza Tanzania inapinda.

Nchi inapinda kutoka Daresalaam kuelekea KOROMIJE. Kule lkwenye misitu na watu walikohama sisi ndio tunaelekea huko.


Ndugu Rais mungu akuhidi.



Kishada.
 
Back
Top Bottom