Kwa propaganda ya udini: Ni vyama vipya tu au Vichanga vyenye uwezo wa kuiondoa CCM Madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa propaganda ya udini: Ni vyama vipya tu au Vichanga vyenye uwezo wa kuiondoa CCM Madarakani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kakakuona40, Feb 25, 2012.

 1. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba wananchi wengi wanaonekana kukata tama na maisha na mzigo mkubwa wa lawama unakwenda kwa watawala, na unapogusa watawala umeigusa CCM, hivyo ni dhahiri CCM inashuka popularity na hilo ndio linalopelekea wananchi kuhisi kutafuta altenative.

  Currently, japo kuna vyama vya upinzani vimeonyesha nguvu kwa kiasi fulani katika baadhi ya maeneo lakini kuna matatizo makubwa kiasi yanatokana na muundo wa hivyo vyama na propaganda za UDINI ambazo mimi binafsi naamini katika hivyo vyama hakuna chenye sera ya UDINI ila kama chama ila individually upo ushahidi wa baadhi ya viongozi kuwa nalo hilo tatizo.

  Ingawa wapo baadhi ya watu hawatakubaliana na mimi lakini propaganda hizo za udini zimevijeruhi hivi vyama kwa kiasi kikubwa na kukosa imani kwa upande wa pili.

  Kwanini nini vyama vipya/vichanga?
  Vyama vipya vinavyochipukia nchini vina nafasi kubwa sana ya kukubalika mbele ya watanzania kama watalitathmini hili jambo mapema, kwa kuwa ingawa tunaambiwa hakuna utaratibu wa kuuliza dini ya mtu kwenye sensa za kitaifa kwa kuwa dini ni suala sensitive (sensitive in what sense?) lakini source nyingi zinasuggest idadi sawa ya waumini wa hizi dini kuu mbili na nyingine zinasuggest waislam kuwa ndio wengi (angalia link hapo chini). Assuming information kuwa waumini wa hizi dini mbili wapo sawa ni sahihi , Basi hakuna chama chochote kinachohusishwa na UDINI kitaiondoa madarakani CCM, na kutokana na hili ni vyama vipya tu na vichanga ambavyo vipo neutral au havijakumbwa na propaganda hii au vitakavyoweza kuweka mikakati ya kukwepa propaganda hii ndio vyenye chance kubwa ya kufanya mageuzi ya uongozi katika taifa hili.
  links:
  Religion in Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia
  Tanzania - History Background - Percent, Education, People, and Tanganyika - StateUniversity.com
  Muslim Population Statistics
   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii thread yako ni nzuri, ila kwa kuwa husifii CDM, tarajia upinzani mkali kutoka kwa VINEGA!
   
Loading...