Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

CCM narudia tena Uwanja wa Chato usichukue sehemu za kampeni yenu. Wekeni sera mezani na sio kutetea kilichofanyika kwa sababu tayari vimeonekana. Watanzania wanataka kujua wanaelekea wapi baada ya ndege, airports, mabarabara, SGR za uchumi wa kati na ma fly overs.....
Uwanja ndiyo umeshajengwa na unatumika na watanzania na upo ndani ya Tanzania na hamuwezi kutufanya lolote.Wakiuongelea kwa kauli za ovyo tutasema vilevile ili hata wale wanaodanganywa wajue kwamba bado kuna watanzania wana chuki na mambo yanayofanyika ndani ya nchi yetu na yenye manufaa na nchi yetu .
 
Endeleeni kujibu spana tu....
 
Mambo ya makabila yametoka wapi??? Mbona unaweweseka
Kwa taarifa yako hata mie mama yangu ni msukuma ila sikubaliani na magufuli Kama anaongoza vizuri na Kama yeye ni kiongozi mzuri!

Kinachosababisha tuhoji ni kwa sababu wanadai wamelipa cash na kwa tunaojua hakuna sehemu zenye upigaji kama kwenye manunuzi ya serikali
Unawezaje kuwa JF kwa miaka 5 bila kuongeza ufahamu? Unajitangaza kwa yasiyohusika hapa? Sihitaji kujua kabila la mama yako! Ni msukuma, hongera basi!
Kwa hiyo unadhani Magufuli angetaka kuiba pesa za serikali alihitaji kupitisha pesa kwenye ununuzi wa ndege? Awamu ya 4 nchi hii ilinunua nini? pesa zilikuwa zinapelekwa wapi? Watu walisafiri dunia nzima na hakuna aliyehoji matumizi ya safari hizo.

Tatizo unaonesha udhaifu kwa kuimba wimbo wa watu wadhaifu wenzako. Wakisema ndege hatuzitaki, nawe unauliza hayo hayo. Unaanza kuhisi eti kwenye manunuzi kuna upigaji, hujui kwamba awamu ya 4 ilishindikana kununua ndege moja tu, kwa kuwa tu Boeing walikataa mtu wa kati. Acha kuropoka usiyoyajua. Ndege hainunuliwi kama shati!!
 
Kaniacha hoi kutetea 20,000 ya vitambulisho vya machinga wakati Raisi mwenyewe kaomba poo kasema si lazima 😂😂😂😂😂😂
Kuna Mkuu wa Mkoa aliondolewa kwenye nafasi kwa kuwa Mkoa wake uliuza vitambulisho vichache!!!!
 
Sasa Kama Polepole anaiharibia CCM si ndio vizuri kwa upinzani, Kimsingi Sasa hivi kila Lissu akiongopa, CCM hawasubiri aendelee kupotosha sasa inamfanya Lissu aonekane Mwongo.

Kuna siku Lissu akiongopa kuwa Uwanja wa ndege Mpanda umejaa majani, matokeo yake meneja wa kiwanja akaonyesha video za Uwanja ukionekana uko vizuri na kuna watalii wanashuka kutoka kwenye ndege.

Lissu ni Mwongomwongo.
Jibu chato....
 
Uchaguzi na propaganda ukaa pamoja siku zote. Lakini propaganda zisivyopangiliwa vyema zinaweza kuwa mwiba kwa anayesimuliwa.

CCM fanyeni maamuzi magumu, kubalini kuwa Polepole amepwaya kwenye hiyo nafasi, kubalini kuwa ni kipindi Cha kutafuta wabobezi waingie kazini si kuruhusu watu kama Polepole kukitetea chama...
Braza Kama bado hujaoa ebu fika mbeya nikupatie dada wa kinyakyusa buuuuuure🤗
 
Hivi CCM imekosa watu wa kufanya uenezi? Mtu hakijui chama, hajakulia ndani ya chama iweje leo apewe kazi ya kukitetea na kukijenga? Sasa huku ni kujenga?
Eti kwa vile ni tiss basi inatosha hiko chama kajaza matiss humo badala ya makada wa ccm, wao wanajari maguvu yao, tena maguvu yenyewe kwa vile polisi na jeshi lao, sasa upepo umebadilika, namna kutumia watu wasiojulikana imeshindikana.
 
Yaani hapo umesahau tu kuiponda stiglers gorge ili list yako ikamilike.
 
Ninacho amini, Polepole na Bashariru watakuja kujisifia kama walitumia utaalamu wa hali ya juu kuiuwa CCM kwa sababu ilikuwa inadunisha maendeleo.
 
Akitolewa na kuletwa anaefit si ndio kifo chenu cha mapema?

Kubalini tu PolePole anaitendea haki ofisi yake kiasi mnakosa nn cha kumpinga. Leo Hansard na taarifa ya CAG kawapa. Nasubiri mui-challange kitaalam sasa.
 
Uchaguzi na propaganda ukaa pamoja siku zote. Lakini propaganda zisivyopangiliwa vyema zinaweza kuwa mwiba kwa anayesimuliwa.

CCM fanyeni maamuzi magumu, kubalini kuwa Polepole amepwaya kwenye hiyo nafasi, kubalini kuwa ni kipindi Cha kutafuta wabobezi waingie kazini si kuruhusu watu kama Polepole kukitetea chama...
Wacha kupanic braza, ukijitigiza sidano itakatia tulia
 
Uchaguzi na propaganda ukaa pamoja siku zote. Lakini propaganda zisivyopangiliwa vyema zinaweza kuwa mwiba kwa anayesimuliwa.

CCM fanyeni maamuzi magumu, kubalini kuwa Polepole amepwaya kwenye hiyo nafasi, kubalini kuwa ni kipindi Cha kutafuta wabobezi waingie kazini si kuruhusu watu kama Polepole kukitetea chama...
Nilishaacha kumsikiliza polepole siku nyingi. Lazima niitendee haki nafsi yangu. Akili yangu haishibishwi na uropokaji wa dogo huyu mchumia tumbo.
 
Back
Top Bottom