Kwa Pogba tumelamba Jokeri

Kilityme

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
218
574
Ama hakika majuto ni mjukuu..! Tunajuta kukusajili Pogba, tumejichanga sana kupata hela ya kukusajili kipindi kile tukitegemea utakuja kuipa timu mafanikio......tulipigana kwa jasho na damu kupata ile hela ya usajili aisee.....nakumbuka mpaka hela nyingine ilibidi tumpige fix yule mnywa maji angalau tupate saini yako.....Laahaulaa..!!! Kumbe tulilambishwa jokeri na mchezo ukaisha.....Pogba nikukumbushe kwamba mpira pasi sio butubutu.....hii ligi inataka akili sio miguvu...,Na sasa hivi unaonekana umechanganyikiwa ndio maana unagombana na kila mtu.....Juzi from no where umegombana na wale jamaa wanaokusanya kiingilio kwenye mageti ya uwanjani.....yaani umegombana nao bila sababu ya msingi.....kama sababu ni kuwa ulihisi kwamba wale wakusanya kiingilio wanaweza kuitapeli timu mbona wewe ulikula hela za jezi za wale mashabiki wa jukwaa la kaskazini magharibi na tukakukaushia na wala hukuona aibu?......wale mashabiki wanalia hadi leo na jukwaa lao tangu litikisike hakuna juhudi yoyote ya kuwasaidia kulijenga....Pogba tumekusajili kwa hela nyingi tena bado huchezi vizuri, huku unawatapeli mashabiki hapohapo tena unajifanya mjuaji unagombana na kila mtu yaani full vurugu huku timu inazidi kuyumba....malipo ni hapa hapa ndugu yangu pogba...watch this space
 
Daah. Wenye akili ndiyo wataelewa hii. Hii ndiyo raha ya fasihi.

Cha kushangaza, Pogba anakejeli hadi watoto wa bosi aliyemnunua
 
Halafu ubaya ni kuwa Pogba anafurahia washabiki tunavo sikitika akiwa ana cheza vibaya, pogba anasema tulivo kuwa tuna shinda tulizoea ushindi wa dezo.
Hivi pogba kwa nini mwisho wa nusu msimu tusimpeleke hata timu nyingine huko akacheze, hata kwa mkopo tu!!?
Maskin timu yetu.
 
jokeri kwenye Europa league Ila kwenye premier league ni Kama ommy dimpoz wanampumulia tu
 
Pogba watazamaji tunamuona anavurunda uwanjani,lakini mwenyewe anajiona bonge la striker japokuwa kafunga bao mbili tuu msimu mzima
 
Halafu mashabiki wa Pogba utawakuta mitandaoni wanavyomtetea utadhani mshahara wanakula wote.
Wanadai Pogba hafungi magoli kwakua kila namba anataka acheze yeye, unaweza kumuona karudi kukaba mpira ukichanganya unakuta kapanda mbele.
 
Mkuu kweli Pogba hafungi magoli na mpira wa miguu ni magoli. Ila jamaa huwa ananipa raha akikamata mpira anajua kuuchezea. Pia angalia pasi za mwisho anazotoa mimi huwa naamini wamalizia ndio hamna kitu. Mzee Ibra makali bado hayajakaa sawa. Naamini soon Man watakuwa vizuri bado wana vijana hodari sana wanajua.
 
Pogba hatareee. Kazi yake ni kutumbua majipu ya wachezaji wenzake uwanjani kasahau kutoa pas na kufunga
 
Mkuu kweli Pogba hafungi magoli na mpira wa miguu ni magoli. Ila jamaa huwa ananipa raha akikamata mpira anajua kuuchezea. Pia angalia pasi za mwisho anazotoa mimi huwa naamini wamalizia ndio hamna kitu. Mzee Ibra makali bado hayajakaa sawa. Naamini soon Man watakuwa vizuri bado wana vijana hodari sana wanajua.
Uko op
 
Upo nje ya mada
 
Back
Top Bottom