Ama hakika majuto ni mjukuu..! Tunajuta kukusajili Pogba, tumejichanga sana kupata hela ya kukusajili kipindi kile tukitegemea utakuja kuipa timu mafanikio......tulipigana kwa jasho na damu kupata ile hela ya usajili aisee.....nakumbuka mpaka hela nyingine ilibidi tumpige fix yule mnywa maji angalau tupate saini yako.....Laahaulaa..!!! Kumbe tulilambishwa jokeri na mchezo ukaisha.....Pogba nikukumbushe kwamba mpira pasi sio butubutu.....hii ligi inataka akili sio miguvu...,Na sasa hivi unaonekana umechanganyikiwa ndio maana unagombana na kila mtu.....Juzi from no where umegombana na wale jamaa wanaokusanya kiingilio kwenye mageti ya uwanjani.....yaani umegombana nao bila sababu ya msingi.....kama sababu ni kuwa ulihisi kwamba wale wakusanya kiingilio wanaweza kuitapeli timu mbona wewe ulikula hela za jezi za wale mashabiki wa jukwaa la kaskazini magharibi na tukakukaushia na wala hukuona aibu?......wale mashabiki wanalia hadi leo na jukwaa lao tangu litikisike hakuna juhudi yoyote ya kuwasaidia kulijenga....Pogba tumekusajili kwa hela nyingi tena bado huchezi vizuri, huku unawatapeli mashabiki hapohapo tena unajifanya mjuaji unagombana na kila mtu yaani full vurugu huku timu inazidi kuyumba....malipo ni hapa hapa ndugu yangu pogba...watch this space