Elections 2010 Kwa Picha Hii Ahadi za CCM kuwapatia huduma bora watanzania itawezekana?!

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,232
24,094

Waziri wa Afya Mh. Mponda (Mb) wa kwanza kushoto mwenye suti nyeusi akitembezwa kuangalia huduma za afya katika hospitali kubwa kuliko zote na ya kisasa ya Muhimbili Dar-es-Salaam.

Hapo tunaona Hospitali ya Taifa ilivyofurika na wagonjwa wakiwa wamelala chini kwa kukosa vitanda na wodi za kutosha.

Katika uchaguzi CCM iliahidi kuboresha zaidi huduma na kuongeza huduma za tiba za kisasa zaidi kwa Watanzania. Hapo waziri na timu yake lazima watakuwa wamewasili na magari ya bei mbaya ( mashangingi) huku wagonjwa na watoa huduma za afya kama madaktari, manesi, wafamasia n.k wakiwa na wakati mgumu.
http://api.ning.com/files/6HcaJW81b...D9QTq7ge6IGxDUediD8RdiC9ypWACCceVP/Wodini.jpg
 
wote wanaangalia chini baadala ya kuangalia wagonjwa walilala hapo pembeni.

mitanzania ndivyo tulivyo na tunataka iwe hivyo milele!!
JENGO LINAONEKANA NI JIPYA HALAFU ZUURI KUMBE NDANI DUU!
 
Waliolals chini sio watu ni mbwa wanaonuka ndio maana jamaa wanaangalia chini wasichafue viatu vyao
 
Mimi nasema watanzania matatizo wanajitakia wenyewe. Hawajui kutumia haki yao ya katiba kupitia kura zao. Tarehe 30 pale Jangwani watu walijazani sana kwenda kusikiliza hotuba za CCM, uwanja wa Jangwani hauko mbali kutoka Muhimbili. CCM sio chama cha kuchagua tena kwani imeshindwa kusaidia kutatoa matatizo mengi ya wananchi. Sasa vitanda ni shinda kubwa jamani, si wangewaambia VETA watengezene angalia vitanda simple tu. Huyu waziri hana jipya kwani ni CCM ile ile ya miaka 50 iliyopita. Uchaguzi wa mwaka 2015 utafika na bado wagojwa watakuwa wanalala chini.
 
lakini ndio hawa hawa wananunua gari moja kwa tzs mil 280!
ndiyo na wao wakiumwa ni kutibiwa nje! Hv unadhani ni kiongozi gani atibiwe nchini kwa hali hii! Hata madaktari mazingira ya kufanyia kazi wito unakwisha! Halafu eeti ofisi za serikali wanabadilisha furniture kila mwaka! Na okienda huko watu hawapo ofisini, haya yoote tunayaona!
 
Waziri wa Afya Mh. Mponda (Mb) wa kwanza kushoto mwenye suti nyeusi akitembezwa kuangalia huduma za afya katika hospitali kubwa kuliko zote na ya kisasa ya Muhimbili Dar-es-Salaam.

Hapo tunaona Hospitali ya Taifa ilivyofurika na wagonjwa wakiwa wamelala chini kwa kukosa vitanda na wodi za kutosha.

Katika uchaguzi CCM iliahidi kuboresha zaidi huduma na kuongeza huduma za tiba za kisasa zaidi kwa Watanzania. Hapo waziri na timu yake lazima watakuwa wamewasili na magari ya bei mbaya ( mashangingi) huku wagonjwa na watoa huduma za afya kama madaktari, manesi, wafamasia n.k wakiwa na wakati mgumu.
http://api.ning.com/files/6HcaJW81b...D9QTq7ge6IGxDUediD8RdiC9ypWACCceVP/Wodini.jpg

Angalia linganisha ni hii picha, wakati watanzania wengi wanapata taabu, baadhi ya wabunge wamejifunga minyororo ya dhahabu kwenye miguu.
 
mimi nasema watanzania matatizo wanajitakia wenyewe. Hawajui kutumia haki yao ya katiba kupitia kura zao. Tarehe 30 pale jangwani watu walijazani sana kwenda kusikiliza hotuba za ccm, uwanja wa jangwani hauko mbali kutoka muhimbili. Ccm sio chama cha kuchagua tena kwani imeshindwa kusaidia kutatoa matatizo mengi ya wananchi. Sasa vitanda ni shinda kubwa jamani, si wangewaambia veta watengezene angalia vitanda simple tu. Huyu waziri hana jipya kwani ni ccm ile ile ya miaka 50 iliyopita. Uchaguzi wa mwaka 2015 utafika na bado wagojwa watakuwa wanalala chini.

mkuu hata magereza wanatengeneza furniture nzuri saana na hata jeshi but kinachotekea wanaagiza toka nje! China na uk upumba$$$$$$$fuuuu sana senzi zao!
 
Mimi nasema watanzania matatizo wanajitakia wenyewe. Hawajui kutumia haki yao ya katiba kupitia kura zao. Tarehe 30 pale Jangwani watu walijazani sana kwenda kusikiliza hotuba za CCM, uwanja wa Jangwani hauko mbali kutoka Muhimbili. CCM sio chama cha kuchagua tena kwani imeshindwa kusaidia kutatoa matatizo mengi ya wananchi. Sasa vitanda ni shinda kubwa jamani, si wangewaambia VETA watengezene angalia vitanda simple tu. Huyu waziri hana jipya kwani ni CCM ile ile ya miaka 50 iliyopita. Uchaguzi wa mwaka 2015 utafika na bado wagojwa watakuwa wanalala chini.

Zamani hata mimi nilikuwa nadhani ni hivyo (kwenye red), lakini kumbe hata tusipowachagua WATACHAKACHUA TU!! Inauma sana wanapotawala kwa mabavu wakati sisi hatuwataki!
 
Zamani hata mimi nilikuwa nadhani ni hivyo (kwenye red), lakini kumbe hata tusipowachagua WATACHAKACHUA TU!! Inauma sana wanapotawala kwa mabavu wakati sisi hatuwataki!
mweeee sasa tufanyeje!??
 
ndiyo na wao wakiumwa ni kutibiwa nje! Hv unadhani ni kiongozi gani atibiwe nchini kwa hali hii! Hata madaktari mazingira ya kufanyia kazi wito unakwisha! Halafu eeti ofisi za serikali wanabadilisha furniture kila mwaka! Na okienda huko watu hawapo ofisini, haya yoote tunayaona!
Kama Muhimbili hali ndiyo hii, je huko Ngudu na Nkasi hospitali zao zina hali gani? Inauma sana ninapoona matumizi makubwa fedha yasiyo na tija kwa Umma wa Watanzania walio wengi na hoi kwa kipato huku watawala wa inchi hii yakigharimu maisha bora ya wapiga kura wao.

Eee Mwenyezi Mungu tusaidie!
 
Tusiilaumu sana Serikali kila muundo mbinu unauwezo wake wa kuhudumia, hivi idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa muhimbili iko juu ya uwezo wake au chini ya uwezo wake wa kupokea wagonjwa? Maana kama hospitali imejengwa iwe na vitanda 500 huwezi kulazimisha ifungwe vitanda 600 ili kukidhi idadi halisi ya wagonjwa. Muhimu ni kuimarisha hospitali nyingine kama Temeke na Mwananyamala kwa kuweka vifaa vya kisasa na madaktari ili wagonjwa wasikimbilie Muhimbili kwa matatizo ya mwanzo.
 
Mimi kura yangu nilimpa Dr.Slaa ilikuaje wewe ulimpa JK tafadhali hakuna haja ya kusikitika hapa mwenye maamuzi alikua ni wewe mpiga kura je ilikuaje ukakipigia chama cha ccm? kumbuka ule usemi wa Dr.slaa NIPENI KURA ZENU MUWACHE KUTUMIA NYUMBA ZA TEMBE!!
 
Tusiilaumu sana Serikali kila muundo mbinu unauwezo wake wa kuhudumia, hivi idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa muhimbili iko juu ya uwezo wake au chini ya uwezo wake wa kupokea wagonjwa? Maana kama hospitali imejengwa iwe na vitanda 500 huwezi kulazimisha ifungwe vitanda 600 ili kukidhi idadi halisi ya wagonjwa. Muhimu ni kuimarisha hospitali nyingine kama Temeke na Mwananyamala kwa kuweka vifaa vya kisasa na madaktari ili wagonjwa wasikimbilie Muhimbili kwa matatizo ya mwanzo.

Sasa nani wa kulaumiwa kama sio serikali? Hizo hospitali nyingine ni nani anatakiwa kuziimarisha kama sio hao wanao kusanya kodi za wananchi na kupokea misaada ya wafadhili?
 
Hii ni laana.Haiwezekani mtu wakati wa uchaguzi asahau yote haya halafu baadae analalamika taabu.
 
Walishindwa kuweka mazingira bora kwenye hizo hospitali kwasababu wao huko hawaendi mpaka siku za kuomba kura za kuwaingiza madarakani.wao matibabu yao kama sio ulaya ni india.muhimbili ni sehemu yakujionyesha kua wako kazini tu.angalia mzee mkubwa kashaanza safari zake.hakuna cha mkutano wala nini,ameenda kupumzika baada ya kazi ya wizi wa kura kumalizika.wabongo mtabaki lalama mpaka kufa mmeridhika na jezi ya brazi,badilikeni hamtali,haya sasa.
 
Wote wanaangalia chini baadala ya kuangalia wagonjwa walilala hapo pembeni.

wanaangalia chini kwa aibu,yaani i wish mmoja wa hao wagonjwa angekua na copy ya ahadi zao ampe uyo waziri esp ktk kipengele cha afya,ili waziri ajue lile shangingi lake can do alot for these people
but atleat siku mheshimiwa anaenda tembelea hawakuficha ilo tatizo la kulala chini ili ajionee hali halisi,mhhhh am sure wakirudi ofisini wamesahau kila kitu
 
Back
Top Bottom