Kwa Paroko wa Parokia anayosali Benjamin Mkapa na viongozi wengine wakatoliki CCM

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,309
7,502
Tumsifu Yesu Kristu,

Naanza ujumbe huu Kwa Jina La Baba na La Mwana na La Roho Mtakatifu. Amina.

Ndugu katika Kristu Yesu,
Ni matumaini yangu kuwa waendelea vizuri na utume wako. Tumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa afya njema.

Mara kwa mara mambo mengi yameibuliwa na kuwatuhumu viongozi wa chama cha CCM wakiwamo marais ambao ni wakatoliki kuhusishwa na kashfa mbali mbali za Ufisadi, Uhujumu Uchumi na Mauaji katika ngazi mbali mbali.

Yawezekana wameungama dhambi zao pale ambapo wametuhumiwa ukweli na wakaungama.

Taratibu za maungamo katika kanisa katoliki zajulikana kwa Wakristu wakatoliki popote ulimwenguni. Hapa nitazungumzia kipengele cha "Kutimiza Malipizi". Je Viongozi hawa wametimiza malipizi ya dhambi zao? Au wamekuja kuhitaji baraka za Mwenyezi Mungu kwa ile sala ya "Baba wasamehe, hawajui watendalo" kwetu sisi tunaowatuhumu?

Ni wakati sasa wa Kanisa kuwataka viongozi wa Nchi ambao ni wakatoliki kujisafisha Hadharani. Ni aibu kwa kanisa endapo kiongozi asiyejisafisha kuhudumiwa nalo. Yawezekana kusubiri wakati ambapo Roho Mtakatifu atawahimiza kufanya hivyo na Muda ndo huu ambapo Roho mtakatifu ameniagiza kutoa tamko hili.

Roho wa Bwana anataka kanisa liingilie kati mambo yanayoendelea Nchini. Kanisa lisifunge Mdomo.

Kanisa liwe na takwimu ya viongozi wa Nchi ambao ni wakatoliki na liwapatie mafunzo ya Uongozi wa Kimungu ili waweze kuhudumia kuhudumia watu wa Mungu kama apendavyo Mungu.

Kwa Jina La Baba na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.
 
Kumbuka hata askofu wetu Methodius Kilaini alivuta za Escrow ni bora tujikite kujiimarisha kiimani binafsi kuliko hawa viongozi wetu wa dini. Sio Mkapa tu, hata walioamuru Lissu amiminiwe risasi saizi wako kanisani wanasali na watasema tuwaombee
 
mada yako ina uchadema ndani ! ulikua unataka ajekukuambia malipizi aliopewa,.kama aliambiwa asali salam maria 3 kama amalipizi yake na akasali unadhani Roho atakuja kumbua kwamba hakusamehewa, uchadema na imani za dini haziendani mkubwa.
 
Kwa bahati mbaya sana, hata huyu anayehukumu wenzake kana kwamba kashuka toka mbinguni juzi, akichunguzwa hawezi kuwa salama!
 
Yaani unataka wanaoongoza nchi kwa mlango wa nyuma, wawaambie vibaraka wao wafanyeje? Waombe msamaha hadharani? Kwa lengo lipi, au kujionyesha kuwa hawatumikii nafasi zao kwa maelekezo ya kanisa?
 
mkuu hongera kwa kupoteza muda wako kuandaa mada nzuri kama hii


ila wakuungamisha na kukemea wenyewe ni wapokeaji wazuri wa vipande 30 ulidhani wataeleweka?


TUMSIFU YESU KRISTO
 
Kumbuka hata askofu wetu Methodius Kilaini alivuta za Escrow ni bora tujikite kujiimarisha kiimani binafsi kuliko hawa viongozi wetu wa dini. Sio Mkapa tu, hata walioamuru Lissu amiminiwe risasi saizi wako kanisani wanasali na watasema tuwaombee
Mungu hadhihakiwi
 
Kumbuka hata askofu wetu Methodius Kilaini alivuta za Escrow ni bora tujikite kujiimarisha kiimani binafsi kuliko hawa viongozi wetu wa dini. Sio Mkapa tu, hata walioamuru Lissu amiminiwe risasi saizi wako kanisani wanasali na watasema tuwaombee
Nani aliyeamuru Lissu aligwe risasi? Umeenda kutoa hiyo taarifa polisi? Vibginevyo ni mzushi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...ni bora tujikite kujiimarisha kiimani binafsi kuliko hawa viongozi wetu wa dini.


Kutoka sakafuni mwa moyo wangu, nimepapenda sana sana sana narudia tena sana sana sana, "patamu hapo naomba urudie tena" kwa msisitizo
 
Mtu ni mtu na kanisa ni kanisa.
Mtu anaweza hama na kusali kokote atakapo. Ila kanisa litabaki lilipo.
Huwez husisha madhambi ya mtu na anaposali
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom