Kwa nn baadhi ya wanawake wakipata pesa zaidi ya mumewe.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nn baadhi ya wanawake wakipata pesa zaidi ya mumewe..........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Runner, May 4, 2012.

 1. Runner

  Runner Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wapendwa wa JF, nimekaa nikafikiria sana hili swala nikaona bora niliweke jamvini tupeane mchango. Unakuta umeoa na mwanamke alikuwa anakutegemea kwa kila kitu ingawa kuwa nae anafanyaka kazi, mmeendelea na maisha ya kila siku lakini ikaja ikatokea kuwa mwanamke akapata mkopo ofisini kwao ambao ukiulinganisha na ile niliyokuwa nampatia kiukweli mkopo ni mkubwa kiasi chake, sasa kinachokuja hapa ni kwamba "BAADA YA KUPATA MKOPO AMEKUWA MTU WA NYODO, JEURI, MANENO YA KASHFA NA MAJIVUNO".

  Hata nikisema nimuulize lolote atanijibu kwa mkato......na mbaya zaidi sasa hivi tunaishi kama kaka na dada............,na mara ya kwanza alikuwa nawahi sana kurudi nyumbani lakini baada ya hiyo pesa kurudi kwake nyumbani ni saa 3 usiku?......

  Naomba wana JF mniambie hapa huwa inakuaje kwenye hili? Maana mimi nimeamua kuwa kimya bila kuzungumza chochote.....mbaya zaidi amekuwa busy na simu anaweza ku-chat hata mpaka saa 6 za usiku, wakati mara ya kwanza mm nikitumiwa sms hata moja saa 3 usiku ilikuwa ugomvi ntaambiwa niwaambie hao watu wasinisumbue nipo na mke wangu.

  Lakini leo yeye ndo amekuwa kinara wa kuchat, nikimwabia najibiwa "KILA MTU ANA UHURU WAKE WA SIMU",.........Wapendwa wa JF maneno ninayo mengi sana lakini kwa haya niliyoyatoa naamini mtakuwa mmepata picha halisi............NAWASILISHA
   
 2. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Samahani kwa wanawake, hasa wanaotambua nini maana ya kuwa mwanamke. Wanasema "untufu jalala, mbati yakwe fintasaa, yani, Masikini akipata, ****** ulia mbwata". Asili ya mwanamke ni kuwa chini ya mwanaume. Hii si adhabu bali ni asili. Ila kuna wanawake waliokengeuka wanaona hiyo kama adhabu. Kwa hiyo akipata fedha anaona hicho ndo kitakachomuokoa na mateso hayo. Ni upuuzi.
  Ila na wanaume wengine wanatumia asili hyo kuwanyanyasa, wanawake si sawa. Yote kwa yote, mwanamke hapaswi kuwa na nyodo, awe na hela au asiwe nazo
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mkopo anakuwa na nyodo? sasa atarejeshaje kama anatanulia?
  by the way mpo kwenye ndoa kwa nini kila mtu achukue mkopo wake
  sina ndoa lakini najua mkopo unachukuliwa kwa makubaliano maalumu eg mwataka kumalizia nyumba,kununua kiwanja nk... maana hela ya marejesho ikikosekana burden ya mkopo ni yenu wote. yaani unaacha mke anajichukulia tu mkopo apendavo... hata kama ana access na mkopo ... ungeact kiume bwana...loh
  iyo ndoa yenu naona kila mtu ana malengo yake....
  siwaelewi
   
 4. Evelyn Salt

  Evelyn Salt JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 45,114
  Likes Received: 31,981
  Trophy Points: 280
  lol! kweli wengine c wanawake ni kwekwerekwe
  labda hela zikiisha atajirudi,pole sana.
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kudos da smile kwa hilo inaonekana wote huwa wanasalitiana ila mambo ya mkuki kwa nguruwe ndio ishu..
   
 6. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Mkopo alichukua kwa ajili ya matumizi yake binafsi au biashara??
  Wakati anachukua alikushirikisha?sijaelewa aisee sasa hela ya mkopo ndiyo anatanulia au??
  Pole!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  jamaa ajiandae kulipa tu hilo deni kwani mkopo sio mchezo unaweza kufa kwa kihoro na ni ulimbukeni ndio una wasumbua wanandoa hao..
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Dawa ya moto ni moto jamaa yangu na sio ubaridi, andaa mtoto mzuri wa kusubstute mapenzi yako kwake, hawa ni jamii ya Wanawake washamba ambao wanasumbuliwa na Ulimbukeni na kama amenunuwa gari kwa pesa zake na wewe huna, umeumia jomba!!

  Fasta nakushauri No compromise ni yeye ndiyo ataangaika baadaye kuwaomba wapatanishi ili wanusuru ndoa yenu na ukiweza anza kurudi asubuhi hata kwa kwenda Muziki tu au kwenye Dubai

  Na kama una watoto nimegunduwa Wanaume wengi wanaingia kwenye mateso ya ndoa eti kisa watoto!! je na wale waliofiwa na wazazi na wanasurvive nao sio watoto? huu mchezo wa kugeuza watoto kama weapon ya kuwachapia wanaume usikubali ile kwako. Mwanamke mzuri akiwa na mtu lakini akiachika wasanii wote huwa wanasepa.
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wewe umemwelewa mwenzangu...
  just imagine upo kwenye ndoa...
  hvi unaweza kwenda benki kuchukua m 50 bila kumshirikisha mwenzako ili mjue mnazifanyia nini?
  mwanaume unaacha mke anaingia benki anakopa ... unajifanya huna time?
  na hapo huyo mama hela anatanulia na huyo mumewe ndo atakuja kulipa....
  au hicho kibanda chao kitapigwa bei live.....
   
 10. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Kukubali kufunga ndoa ni kukubali kuweka pembeni uhuru wako....inakuwaje unaambiwa ana uhuru nawe ukaishia kunywea? be a man enough usilalamike kiasi cha mwenzio kujua kuwa akifanya tofauti unaishia tu kublame, utadharaulika shemeji, take action (isiwe kwa kipigo)..anza na onyo...
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Kwa Matola ukileta pozi hizo imekula kwako mzima mzima, Vitoto vizuri vinavyozidi kuzaliwa ni kwa nini nisumbuliwe na Mzee mwenzangu?
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ahahaaa matola wewe mkeo anakohoa kweli....?
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Jaribu kumuita kwa upendo mkae mzungumze na zaidi kujua lengo la kuchukua mkopo na namna ya kuurudisha. Ukikaa kimya mkuu, hizo senti zitaishi na mwisho wa siku utakuta unalazimika kumsaidia mkeo kulipa madeni ambayo kimsingi hayana tija ndani ya familia yako.
  Ukishindwa kuongea naye wewe, unaweza kutumia ndg zake wa karibu au marafiki waaminifu ili mjadiliane kwa kina.

  Hii changamoto inaweza kuwa imetokana na labda wewe kumnyanyasa pale ulipokuwa ndo mfadhili wake mkuu au tu mkeo ni wakuja na kakosa ustaarabu wa kuwa na mtazamo sahihi juu ya familia yake na matumizi ya pesa! Unapaswa kufanya jambo baada ya huu mgogoro kuisha.

  Pole aisee!
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  samahani kusema hivi mzee but huyo mwanamke wako ni *****...yaani anatanua na hela ya mkopo?? hela ambayo itabidi airudishe...dah kweli wanawake wananifurahisha sana...au anakudanganya kapata mkopo usikute tayari kuna libuzi linamfadhili huko maana siamini kama mtu anaweza kuringia hela ambayo sio ya kwake ni ya benk:twitch:
   
 15. Runner

  Runner Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Smile nimekuelewa lakini amebadilika baada ya kupata mkopo,lakini mchakato tangu anataka kuchukua tulikuwa pamoja na malengo pamoja,ila baada ya kuutia mkononi ndo mambo yakawa hivi kama yalivyo sasa hivi
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Sina tatizo kabisa kama utanielewa kwa sababu mimi ni muelewa pia, na nina huruma sana kuliko maelezo ili kuna watu wanajifanya kama wamelose Memory, so is my duties to refresh their Memory.

  Mwanamke hapaswi kuwa juu ya Mwanaume otherwise ni kumkosea Mungu aliyekupa uwanaume, ukifatisha hizi slogan za kipuuzi kama kupinga mfumo dume na Ubeijing ni lazima vitu hivi vitakuangamiza, na ndio maana wanawake wanasiasa wengi wao kamwe hawawezi kuwa na ndoa imara.
   
 17. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...KWANZA HAPO KAKA KUNA ZAIDI YA MKOPO...PILI JE HUO MKOPO ALIUCHUKUA KWA MATUMIZI GANI?
  MAANA MKIWA KWENYE NDOA MNAKUA MWILI MMOJA NA KILA JAMBO NI SHARTI MSHIRIKISHANE...TATU baadhi ya wanawake wanatabia yakuota pembe sana wanapopata vijisent...nahisi kwao pesa ndio kila kitu...wewe tulia, huo ni mkopo tu ukiisha mtaenda sawa.
   
 18. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  pole aisee...
  hv unajua utahusika kuurejesha?... chukua hatua akupe hela mfanye mlivokuwa mmekubalana kama hataki ...piga chini wanawake tupo wengi bwana ....
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Jombaa wewe umetawaliwa na Mwanamke acha kupindisha maneno hapa, tulia tukupe darasa la jinsi ya kuondokana na utumwa huo, otherwise subiri kuna pati za kazini ataanza kukwambia anakwenda na rafiki zake wewe ubaki nyumbani ndio akili zako zitarudi.
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwani kwa hii thread huyu mama ameniaibisha kama mwanamke ..........
   
Loading...